Uchaguzi 2020 Je, Unaweza kupita Ubungo Interchange usiseme asante Magufuli? Mtakubaliana na mimi, asante stahiki ni kura zote kwa Magufuli

Yani majukumu ya serikali leo hii inageuka fadhila? Halafu huyu anaesema haya ni mtu mwenye LL.b hahahah...πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
kwa hiyo umekubali kuwa serikali inafanya majukumu yake vizuri; Mwambia Lissu na Zitto wasikejeli serikali inayotimiza majukumu yake kwa kudai hayo ni "maendeleo ya vitu." Miaka yote huwa tun serikjali kwa nini vitu hivyo havikujengwa huko nyuma kwa kasi hiyo?
 
Yani majukumu ya serikali leo hii inageuka fadhila? Halafu huyu anaesema haya ni mtu mwenye LL.b hahahah...πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
Likes za comment hii zimezizidi za uzi wa mleta mada kwa mbali!Hii ni dalili kuwa bandiko halijaungwa mkono na wadau wa JF wanaojitambua!
 
Watu kama nyie tunaotegemea mmeshaelimika na kuwa na uelewa mpana ili mtumie uelewa wenu kuwaelewesha wengine Kama bado mnamawazo ya namna hii, basi maendeleo yatachelewa sana

Yaani leo serikali kutimiza wajibu wake asante iende kwa Magufuri? Sasa Kama mtu Kama wewe unasema hivi, je Mama yangu aliyeko nyarugusu ndani ndani huko siku akiona gari la kubeba wagonjwa linapaki kijijini kwake kusubiri wagonjwa wa kupelekwa hospital kubwa kwa matibabu zaidi si ndio atasema Magufuri ni Yesu wa pili? Maana huko Kuna mtu amezaliwa hadi anafika miaka 50+ hajawahi kupanda gari, sasa aje aipande (hata Kama ni ambulance) kwenye awamu ya Magufuri atasemaje sasa Kama nyie wasomi mna mitazamo hii
 

Mwaka huu usipopata uteuzi nahama muji.
 
Yani majukumu ya serikali leo hii inageuka fadhila? Halafu huyu anaesema haya ni mtu mwenye LL.b hahahah...πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
...Hata mie nashangaa..Yani mtu kafanya anachotakiwa kufanya, then wewe ukamwambie asante...why??
 
Bado safari ndefu kama wasomi wetu ndio hawa inasikitisha sana, kingine hapo ubungo hakuna interchange ramps
 
Mbona Kikwete alikua hashukuriwi hivi na wakati amejenga barabara za lami kuliko Rais yoyote Tanzania? Hizi ni kazi za kawaida za serikali yanini ku-seek personal glory? Mbona majanga na blunders huwa hamhuahishi Mzee magufuli?

Kaka Pasco ulikua unalia kwamba biashara ya matangazo imekata kwenye media mpaka umepunguza wafanyakazi.,Sifa/malalamiko ni kwa Mzee magufuli? Ulilalamikia serikali tu. Ujenzi wa miundombinu ni kazi za kawaida za serikali tu.
 
Duh!
 
tushukure niametumia pesa zake pale?? acheni ujinga
 
Wanabodi

Hili ni bandiko la swali, Jee ukitendewa wema, unatoa shukrani? Jee Sisi Watanzania ni watu wa shukrani?. Kwa wema wote tuliofanyiwa na serikali ya awamu ya 5 katika kutuletea maendeleo, tarehe 28 October tutatoa shukrani au?...
Kwakweli nchi haikutendea haki pale Ubungo kwa kujenga kadaraja kama kale. Vidaraja kama vile vinapaswa hata Chalinze visijengwe vile vingepaswa kujengwa Tunduru, Korogwe, Kasulu, nk. Watanzania bado sana akili zetu.
 
Hivi mngeona mibarabara ya US si mngetembelea watu vichwani hiyo ubungo ni msaada wa wTu wa japan.
 
Wito kwa wana JF tuliojiandikisha, Tarehe 28 October, tujitokeze kwa wingi tukapige kura kwa ama kutoa shukrani zetu kwa mazuri tunayo tendewa na serikali ya awamu ya tano ama.
Tuseme Ahsante Magufuli kwa kazi gani kubwa aliyoifanya wakati mradi kaukuta umeshatafutiwa hadi pesa?!

Kuna siku niliweka thread hapa kuhusu kwanini Mzee wa Msoga alitaka sana JPM ndie awe rais tofauti na wengine wanavyodhani kwamba ni Mkapa ndie alisababisha JPM awe rais, au kama wengine wanavyodhani kwamba Mzee wa Msoga alimtaka Membe ndie angekuwa rais!!

Sababu kubwa ya Mzee wa Msoga kumtaka JPM awe rais ni kwa sababu tayari alishaonesha uhodari wa Unyapara... kwamba yeye JPM ni nyapara mzuri sana! Ni kutokana na ufanisi wake kwenye unyapara ndio maana JK alikuwa anaipendelea sana wizara ya JPM!

Mzee wa Msoga alikuwa amebuni miradi mingi sana ambayo alifahamu miaka 10 yake ingeisha bila ya kuimaliza kwahiyo alitaka msimamizi mzuri atakayemalizia miradi aliyokuwa ameasisi!!

Moja ya hiyo miradi, ni TAZARA and Bandari Flyovers, Ubungo Interchange pamoja BRT !

Danganyeni wengine lakini sie tunaofuatilia tunafahamu JPM hakufanya chochote kwenye kufanikisha hili zaidi ya kusimamia tu! Lau kama Urais wa TZ ingekuwa miaka saba saba, hizi flyovers ingekuwa zimejengwa na aliyebuni huo mradi manake hadi JK anatoka madarakani na pesa tayari ilishapatikana!


Magu m

Magu mwenyewe, enzi hizo akiwa Waziri wa Ujenzi, kwenye kikao cha bajeti cha 2015/2016 anawasilisha bajeti kwa kusema:-

Utaona hapo juu wasioogopa Wazungu tayari walishachukuwa mpunga wa Wajapan kwa ajili ya TAZARA Flyover na kuhakikisha Bretton Woods wanatoa greenlight ya mpunga kwa ajili ya Ubungo!

Sasa sijui unataka watu waseme "Ahsante Magufuli" kwa kuwa Nyapara Bora!!

Na kama Nyapara tu inatakiwa ashukjuriwe kiasi hicho, what about wale waliowezesha ku-identify problem, kufanya assessment na hadi kutafuta pesa?!

Na itoshe tu kusema kwamba, miradi mingi ambayo JPM anadanganyia mazwazwa, yeye kaikuta tu, including mradi wa uboreshaji wa barabara za Dar es salaam ambao mpunga ulikuwa approved on March 2, 2015... habari zaidi, hapa!

Kwa bahati mbaya sana, miradi aliyoanzisha au kutafuta pesa JPM mwenyewe ndiyo hiyo hiyo inayoongoza kwa kulalamikiwa:-

1. Ndege,
2. Chato International Airport,
3. SGR
4. Bwawa la Umeme!!!

Hiyo ndiyo miradi aliyoipigania JPM mwenyewe!! Ingawaje SGR Project ilikuwepo, lakini mradi huu nampa yeye kwa sababu plan ya mwanzo aliipiga chini nakuileta ya kwake mwenyewe including how to fund the project!!
 
Chadema ruzuku Yao ni Milion 250, ccm no BILIONI +
There are some powerful people in our country trying to make it difficult for us to vote for Tundu Antipas Lissu. You know why? Because they know when we vote, things change.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…