Kwangu ni Mwanza, nafanya kazi Arusha, ni miaka sasa, narejea kwangu kuona familia kila baada ya mwezi 1 au miezi miwili, swala la utafutaji kwa Dunia ya sasa tunaenda popote na tunarejea baada ya muda, kuhusu maswala ya familia kwa maana ya nyumbani kwetu kwenye uzao wa baba au mama, hua tunaangalia mazingira na nyakati ambazo matukio hutokea, kwamba unaweza kwenda au utaenda baadaye.
Dunia imekua na vifo, sherehe na matukio kadhaa, ukijajali yote eti kisa ni ndugu, hutoboi, utatumia pesa nyingi karibu kila mwezi huku maendeleo ya familia yako yanakukabili, binafsi hua sijali sana maana sometimes kipato chako ili kikidhinmaisha yako na familia yako, pia na ndugu ktk matukio yao,yakupasa kua na kipato kikubwa sana, na hiyo ni kwa watu wachache sana, ambao wakisikia msiba wa mjomba wa mjomba wake wanapanda ndege kwenda msibani kuzika na anarudi jioni.
Mwenzangu una mshahara wa laki8 una familia, ukisikia tukio unaanza kutafuta ticket ya bus, na ruhusa za kazini ambazo ni ngumu, maana kazi inatambua misiba ya Baba, Mama, mtoto, mke na mume, unashindwa kwenda kwa sababu unatumia bus siku nzima, ukae msibani siku mbili, uanze kurudi job siku nyingine nzima, siku ya nne ndo urejee ofisini, ni ngumu sana.
So sometimes mambo mengi kwa sasa kuhusu familia zetu hizi yapotezee na mengine yashiriki.