Je, unaweza kutumia Tsh 15,000 Hotelini Kwa Menyu ya Mchana tu? Toa mchanganuo wako hapa!!

Je, unaweza kutumia Tsh 15,000 Hotelini Kwa Menyu ya Mchana tu? Toa mchanganuo wako hapa!!

Mimi sio mpenzi wa Mahoteli maana ndiko vyakula bei ghali....

KFC Zinga wings kaa sikosei ni elfu 9. Hapo juisi ni elfu 2500. Haujanywa maji....na ice cream ukiwa unaondoka.

Colonel burger nadhani ni elfu 12...bado juice na ice cream....15 000 ishakata hiyo.
👐👐
 
Kama unazungumzia Chakula cha Hotelini basi unatakiwa kufahamu kuwa bila mbwembwe zozote 15,000/= Cash ni wali mbogamboga na viambata vyake kama Maji ndogo,tunda n.k au labda kama unazungumzia Cafeteria za huko Uswazi kwenu ndo utaanza kuagiza zaidi ya vitu vitatu kwa hela hiyo.
duuuh🤔🤔
 
Hiyo pesa unaweza umudu tuu kununua vitafunwa na soda au maji ukiingia Hotel za kweli. Kwenye mahotel mlo mmoja (simple menu) siyo chini ya US$ 15 ambayo ni sawa na TZS 35,000.

Ukienda kwenye migahawa mfano unapiga mwenu nzuri kwa TZS 6,000 (Pilao mbuzi, Biriani au mlo wowote wa kuku) na Juice nzuri ya 1,000 unabakiwa na pesa ya kesho
hapo kwenye pilau mbuzi patammm mkuu
 
Mimi haizidi 4,500/= chakula changu . Tena Zege(Mishikaki miwili 2,500 zege+1000 Mishikaki) + Soda(500) + Hill water(500) hapo kama nina hamu na chips ila kama kawaida naagiza Pilau kwa Tsh 1,500/= na Hili water 500...Haizidi hapo ,Asubuhi ni Supu ya Buku jero na chapati mbili(2,100/= na Pepsi baridi 600 = 2,700/=) ,Usiku nakuwa home nakula ndizi bukoba mbili za kumchesha na kiazi mbatata kimoja +kipande cha sangara wa kuchemsha.(Sangara kipande buku+ndizi 500 kiazi 100 =1,600/)

Kwahiyo bajeti yangu ya siku ni kati ya elfu 6 hadi elfu 8.
 
Chips samaki na mirinda nyeusi, kahela kanaisha. Hotel hapo

Restaurant hela inatosha na chenji inabaki.
Kama ni ijumaa, Biriani kuku 6000
Wali samaki 7000
Chips mishikaki ya kuku 2 = 5000
Wali nyama 3000
Machalari 3000 nk
 
Me nakula kwa 1600 kwa siku nzima, naskip breakfast mchana nakula wali wa buku kwa mama ntilie, jion chapati 2 na chai ya rangi 100.
 
Back
Top Bottom