Je unene husababisha mwanamke kushindwa kushika ujauzito?

big fish

Member
Joined
Jul 19, 2013
Posts
7
Reaction score
0
Wanajamvi

Nimeoa mwaka mmoja uliopita.Tumefanya juhudi za kupata mtoto mimi na wife wangu lakini bila mafanikio. Tulijaribu kumuona doctor akasema mke wangu ni mnene na kizazi chake kina mafuta mengi hivyo itakua ni vigumu kupata mimba. Sasa hivi ameanza mazoezi ya kukata uzito japo mafanikio bado ni madogo. Toka tumuone doctor it is about 4 months now na mpaka sasa amefanikiwa kupunguza only 2kg. Tulipomwona doctor alikua na kilo 85.

Swali langu ni je unene unaweza kumfanya mwanamke ashindwe kushika ujauzito. Mbona naona wanawake wengi ni wanene lakini wanashika mimba.

Ushauri wenu tafadhali.
 
Mmh, mbona kilo 85 ni za kawaida sana kwa wanawake walio wengi? Kuna watu wanasema unene ni tatizo, lakini nakuhakikishia kuna wanawake wenye unene kama huo wanatoa mimba kila kunapokucha. Maana wamezaa watoto wametosha lakini kila siku mimba zinaingia.

To be frank mtoto ni zawadi kutoka kwa Mungu, utampata itakapompendeza Mungu. Maana kuna wanawake ambao wana kilo 50 na bado hawapati watoto na wakipima hospitalini wanaonekana wapo salama. So naweza kusema haya mambo ni magumu sana kuyaelewa wakati mwingine. Na hasa kwa context ya Tanzania ambako kumekuwa na ongezeko kubwa sana la couples zisizoweza kupata watoto.

Nafikiri kuna haja ya serikali kulifanyia utafiti jambo hili ili kujua ni nini hasa kinachopelekea wanandoa wengi kushindwa kupata watoto. Ofisini kwangu pekee kuna couples kama nne hivi zina zaidi ya miaka mitano tangu ziingie kwenye ndoa, lakini hazijawahi kupata mtoto hadi leo. Ni suala la kumuomba Mungu zaidi.
 
Swala la kupata mtoto lina factor nyingi sana swala la unene ni minor sana kuna mama namjua anakilo kama 140 hv na amejifungua mtoto ana miaka kama mi4 hv mtoto kwa sasa yani huyo mama ukimuona mcheza sumo anaingia mara moja na nusu.
 
At least mnaponiambia hivyo mnanipa matumaini maana nilikua nimeanza kuogopa. Thanx mkuu
 
Unene hauna uhusiano na kupata au kutokupata mimba. Nenda ForePlan clinic Ilala kwa ushauri zaidi, au angalia kipindi chao kila J4 Chnl 10 jioni utawaelewa. Usijali watoto utawapata mpaka useme baaasi.
 
duh hata nami nafarijika kuona thread hii maana ni mwaka wa 5 sasa sijabahatika kupata mtoto ila naamini kila jambo na wakati wake, na Mungu aliyewapa wengine watoto ndio huyo aliyetunyima sisi...so mi naona wenye tatizo hili tuzidi kumuomba Mwenyezi Mungu...labda ametunyima watoto huku ametuandalia pepo jamani! Inshaallah atufanyie wepesi.
 
Unene kama unene sio sababu isipokuwa inatokea mara chache, kwa wale wenye mafuta mengi kwenye kizazi yaweza kuwa sababu.
 
big fish,.

Pole kwa tatizo lako.

Kiukweli Ingawa kilogramu 85 si 'nyingi sana' inategemea pia uzito huo uko kwa mtu wa urefu kiasi gani.

Pili, Sijajua ni vipimo vingapi na vya aina gani mlivifanya (WOTE WAWILI) na kupata majibu gani kufikia hitinisho hilo.

Ila ningesema, Unene unahusianishwa na ongezeko la mafuta katika mwili hasa sehemu mbali mbali za mwili, kitaalamu unene unuhusianishwa na Ugumba hasa kwa tatizo la kitaalamu liitwalo Polycystic Ovarian...ama Polycystic Ovarian Syndrome. (Nimekosa namna ya kueleza kwa lugha ya Kiswahili) Tatizo hili hasa kuchangiwa na kuwa na mzunguko wa siku (mwezi/hedhi) usio rasmi! Pili husababishwa kutolewa kwa mayai yasiyopevushwa/au kutopevushwa kabisa kwa yai wakati wa mzunguko(Anovulation) , Sababu ikiwa kuwepo kwa mafuta mengi (hasa tumboni) huchangia kutolewa kwa vichochezi vya kiume (hormones) ambazo nazo huchangia katika kutopevushwa kwa mayai ipaswavyo.

Sababu hizi na nyinginezo huweza kusababishwa mwanamke kutopata mtoto/watoto.

Tofauti na hapo kuna madhara, uhusiano wa karibu wa unene na kisukari, kifafa cha mimba,kuharibika kwa mimba n.k hata hivyo hii hatuiti kuwa ni ugumba.

Jambo la muhimu ni kutambua uzito uko kiasi gani kwa ulinganifu wa urefu wake pia. Pili kufanya vipimo vyote muhimu kubainisha tatizo liko wapi (Primary or Secondary Infertility).
 
Last edited by a moderator:

unene sio tatizo
 

mtafute huyu mama atakusaidia 0656380744
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…