Kwaza nakushukuru kwa kutoa sehemu hii ili tusamue kidogo kuhusu katiba,muungano ni kitu kimoja kizuri sana na mtu yoyote anaekataa muungano huwa haoneshi kukamilika ,lakini jee kwa aina hii ya muungano kweli ni haki kuukubali? Mimi binafsi siupendi tena na nauchukia ndani ya nafsi na sio nauchukia tu la! Bali ninazo hoja za kutoa kama ifuatavyo:- 1.kushindwa kwa serikali kuzitatua kero za muungano kwa mika takriban 41; tokea muungano huu ulipoanza pamekuwa na kasoro mbali mbali ambazo hadi sasa hapana iliyopatiwa ufumbuzi, hii inaonyesha kwamba tukikurupuka kuziingiza tena nchi katika muungano wa aina yeyote hatutofanikiwa na badala yake mmoja atanamiwa na mmoja atafaidi,kero hizi ni kero za kihistoria kwani zilianza muda mfupi baada ya muungano pale mzee karume alipokwenda kwa nyerere kumtaka waondoshe baadhi ya mambo ndani ya muungano na nyerere akajibu "muda bado"na hadi sasa umekuwa mchezo wa mtoto lalalala tu ,hadaa na dhulma ndio matokeo ya muungano. 2.kushindwa kwa wasimamizi wa muungano kuzieleza bayana faida za muungano kwa zanzibar:mikutano mingi ambayo nimekuwa nikihudhuria bado kabisa viongozi wasimamizi wa muungano hawajaeleza hasa ipi ni faida kwa zanzibar katika muungano kwa kipiondui chote cha muungano,ni juzi tu nilihudhuria katika mkutano wa kuwaaga wahitimu wa vyuo vikuu mkoani morogoro wa chama changu ccm, ambapo alialikwa mgeni rasmi mh. Abrahmani kinana pamoja na viongozi wengine kama mh.samia(waziri husika wa muungano),mh. Samia alipewa fursa ya kuzungumza na wananchi kuhusu faida za muungano,faida kubwa aliyoiogelea nikuwa watanganyika sasa wanajua kupika urojo! Ivi hii ni faida ya kuitaja mbele ya wasomi?, faida nyengine akasema kuwa yeye alisoma katika chuo kikuu cha mzumbe na lau si muungano ingebidi kusoma kwaoo zanzibar,huyu haifahamu historia ya zanzibar hasa katika nyanja ya elimu,zanzibar kabla ya muungano ilkuwa nchi ya tatu kwa wasomi katika nyanja zote,wakati huo tanganyika hata kuzaliwa bado. Na faida ya tatu akasema watu tayari wameshachanganya damu, pia hoja hii haina msingi, kuvunjika kwa muungabno kuna tofauti kubwa na kuvunjika kwa ndoa , bado watanganyika ni ndugu zetu lakini kinachodaiwa ni hii sababu ya udhalili kule zanzibar ife. 3.kukosekana kwa hati halali ya muungano hadi sasa: Nchi zozote zinapoungana lazima mkataba wa muungano uwekwe wazi kwa nhi zote na hata kwa raia ili papatikane uhalalai wa muungano huo, zanziba imishi ndani ya muungano kwa miaka isiyopungua 40,lakini dai unavo dai basi hupati maelezo yanayojitosheleza, mwisho wako ni kifungo na kuandaliwa kesi ya uhaini . 4.dhulma za makusudi zilizofanywa dhidi ya zanzibar.,ikiwa nipamoja na kuporwa haki ya kuwa dola kwa maelezo zaidi soma kitabu cha kanisa katoliki na siasa za tanzania bara cha dr. Sivalon, pia soma kwaheri ukoloni kwa heri uhuru cha dr. Mohammed saidi na hata maisha na nyakati za abdulwahid sykes.