Miaka ya tisini mwishoni tulikua na tabia ya kutembea kikundi, tukafika kwenye shamba la wajeda lina miembe kibao.... tukaanza kudeal nayo bhana..... kumbe hairuhusiwi..... jamaa wakatuzunguka wakatuteka na kutuuliza kwa nini tunatungua maembe mabichi... mmija wetu akajibu njaa.... tumetembea sana...
Kulikua na sherehe siku hiyo... wakatupeleka upande wa jikoni kwe masufuria ya pilau ambayo tayar wameshapakua mzigo..
Bwana weeee..... tulikulaa.... kila ukisema umeshiba... unakula mbata la mgongo......
Tulikula adi mtu unaanza kulia "nimeshibaaa" huku unaomba msamaha.... "afande naomba nisamehe nimeshibaaa"
Sitamsahau jamaa yangu mmoja kashiba akaomba msamaha.... kusimama tu ivi akacheulia kwe sufuria lake.... akaambiwa hakunankuondoka adi amalize...
Wanajeshi noma.