JE UTAJUAJE WEWE Ni MHENGA?

JE UTAJUAJE WEWE Ni MHENGA?

Joined
Jun 14, 2016
Posts
40
Reaction score
38
UTAJUAJE KAMA WEWE NI MUHENGA.
zifuatazo ni factors za kujijuaa kama wwe ni mhenga[emoji1541][emoji1541][emoji1541][emoji223][emoji223][emoji87]

1. Kama ulikata daftari mara mbili. Kipande kimoja ukaacha nyumbani na kingine ukaenda nacho shule. We ni muhenga.
2. Kama ulitumia kipande cha kandambili kama ufutio.
3. Kama ulikanyagia kisigino ulipotoka kuoga ili usichafuke kwa kuwa hauna kandambili....We ni muhenga.
4. Kama kwenu mlianika betri za national ili ziongezeke chaji kwenu We ni muhenga.
5.Kama ulilala na sare za shule ili asubuhi usichelewe halafu asubuhi ukajikuta umejikojolea We ni muhenga.
6. Kama ulienda choo porini na ukajipangusa kwa nyasi hongera aisee.....We ni muhenga
7. Kama uliweka chumvi kwenye uji mweupe ndio ukanywa....We ni muhenga
8. Kama ulilamba sukari ukapangusa mikono na ukasahau mdomo....sema kichapo heheeee..We ni muhenga
9.Kama uliogea karai la chuma We ni muhenga
10.Kama uliambiwa ushike sikio la kulia kwa kupitisha mkono wa kushoto juu ya kichwa ndio uende darasa la kwanza.....We ni muhenga
11.Kama ulipaka mafuta yanaitwa RAYS ya bluu au YOLANDA....We ni muhenga
12.Kama sare yako ya shule ilikuwa na viraka vingi hadi watu wasitambue rangi ya sare ya shule yenu.....We ni muhenga
13.Kama ulivalishwa nepi na sio papmpers.....We ni muhenga
14.Kama ulikunywa maji kwa kata na ukaogea sabuni ya REXONA wewe We ni muhenga
15.Kama wewe ni mwanamke na Uliwahi kuvaa viatu vya LOSO We ni muhenga.
16. Kama ulipenya njaa ya mwaka 1984 na bado unaijua facebook We ni muhenga.
17.Kama ulipakwa Gv au mafuta ya breki ya AGIP kwenye kidonda.....We ni muhenga
18.Kama ulienda shule peku huku umebeba kuni na maji ya kuwapikia walimu..We ni muhenga
19.Kama ulivaa kandambili mikononi wakati mnacheza mpira wa makaratasi "one touch".....We ni muhenga
20.Kama uliweka kioo chini ya dawati ili uwachungulie wasichana...We ni muhenga
21.Kama mpiga picha alishakuambia picha yako imeungua basi wewe pia ni muhenga
22.Kama wewe ni msichana na uliwahi kuvaa NYANYAPUZO We ni muhenga
23.Kama uliwahi kutengeneza magari ya waya,mabox na makopo yalioisha KIMBO We ni muhenga
24.Kama uliwahi kucheza ule mchezo wa kifimbo cheza We ni muhenga
25.Kama ulitumia GUNZI kuchambia au kujisugua makalio chini We ni muhenga
26.Kama ulienda shule na sukari kwenye kipande cha gazeti kwa ajiri ya kuweka kwenye bulga We ni muhenga
27.Kama uliwahi kuvaa ndala za SKY WAY ,NODIN,UMOJA na viatu vya bora We ni muhenga
28.Kama uliwahi kukojoa dirishani kisa unaogopa kutka nje We ni muhenga
29.Kama uliwahi kuogea sabuni ya komoa,komesha,mshindi,ilula We ni muhenga
30.Kama uliwahi kutumia mafuta yanaitwa. TANBOND,KIMBO,,,,We ni muhenga
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Hebu wakumbushe wahenga wenzio uliocheza nao
 
Ila losso ikirudi tena lazima itaheat tu,wallah ningekuwa mfanyabiashara ningeshauri campuni moja china itengeneze losso lazima atauza sana tena sana.
 
Back
Top Bottom