Je utakubali???

Je utakubali???

Hivi mapenzi yanafundishwa wapi au kwa lugha gani ili na mimi nikajifunze ?
Nadhani hakuna certificate, diploma au degree ya mapenzi, hivyo basi ni mapenzi ya wawili (wakipendana) wewe mzazi, rafiki au jamii si vema kuingilia
 
elimu yako kutwa unalalamika na ccm elimu nini bwana watu wana pesa nakutajia matajili darasa la tatu.. nenda sinza au kkoo mbeya njombe songea ukikuta hotel zote za kisasa zimeandikwa wanyama hotel mwenyewe std 3 rombo grean view darasa la pili engeen mbezi beach za seif mwalabu kasoma chuo tu madrasa hela ndio mpango nyie niaje[/QUOTE

MZEE HEBU RUDIA KUWAPASHA TENA. SIYO HAO TU MATAJIRI WAKUBWA/WALIOFANIKIWA DUNIANI ELIMU YAO YA KAWAIDA SANA. WENGINE HATA HIYO SIJUI BACHELOR DEGREE YENYEWE HAWANA. WENGINE WALIFUKUZWA SHULE KWA UKILAZA LAKINI NDIYO HAO WALIOFANIKIWA KWA SANA.
 
swali gumu. Kwangu itategemea;
form4 or less - no. I may date the person but not marry...
Form6 - not sure
bachelor/masters - ideal
phd - lol, how many are even there?

I prefer small gaps between couple attributes and i wouldn't feel comfortable having such large gaps with my lover. Some discussions zinakuwa ngumu kidogo because of the gap.
I guess it's my background and environment inanifanya niseme hivi. Most of my friends frequently challenge me intellectually and that's something i'd want in a future partner.
for the record, i'm not a chick but i would do this if faced with a such a situation
hongera mzee, uko juu kielimu.
 
Most of my friends frequently challenge me intellectually and that's something i'd want in a future partner.
for the record, i'm not a chick but I would do this if faced with a such a situation
Mkuu the color of fonts you are using its hard to see (please be considerate) unless you want to read what you write yourself.

You want to be challenged intellectually you have your friends am sure a partner can challenge you in many other ways.., and being wise, you don't have to be a rocket science, am sure she can challenge you in current affairs.
 
fazaa kwani mtu kutokwenda shule ni mjinga?...wajinga kibao tunao maofisini...
Ujinga unapishana ujuwe, kuna catogories nyingi tu....Hio ya kuto kusoma imepitiliza, yani kama hana elimu siwezi kumuozesha hata siku moja binti yangu.

Hao ujinga unao ongelea kwa wale wako ma ofisini...sidhani ni wajinga.

Wasinge fanya kazi ma ofisini, wewe unaongela tabia zake sio nzuri labda, na kama ni mjinga basio lazima awe katika wale hawajasoma tu, yani kaingizwa kazi kimipango mipango tu, sio ki elimu yake.

Usisahau kuna watu wako ma ofisini kwa mipango mipango flani tu ndo wamepew3a kazi :A S shade:
 
unaongea utumbo gani wewe?...we elimu unaitafsiri vipi...wangapi wamesoma hahwajaelimika..katik amaisha yako yote hapa duniani cha kuombe a ni uwe na elimu ya maish basi!!!

omba umpate uyo mwanaume anaejua maana halisi ya maisha na kutafuta..elimu is just secondary kwangu...wangap wamejiendeleza ukubwani na sasa wako mbali;wangap ni wafanyabiashara wakubwa uku wana elimu ya lasaba/....jipange upya
 
Wazungu walituweza kwenye hili. Ni bora waarabu walitufanya watumwa.
Hii western Education imetuharibu sana kifikra. M
 
@ Mkona wa kwapa, Hizo ni kelele zenu tu ,huwezi kumfananisha mtu aliye soma na mtu asiye soma hata siku moja.

Eti elimu gani unayo ongelea, wewe ndo ungetueleza elimu una itafsri vipi? Ajabu eti elimu ni maisha, maisha anayo panga ni mungu, na elimu ni kitu kingine kabisa.

Mimi navyo jua maisha ni mungu anaye panga, uwe na elimu au huna...akitaka kukupa atakupa tu...sisi tunaongelea elimu.

Afu hebu someni mtoa mada anasema nini kabla ya kurukia kujibu ana ongelea elimu gani.


Yani utani pembeni mimi binti yangu siozeshi wajinga, na wajinga ni wale baba zao walikuwa na uwezo wakuwasomesha na hawakusoma...Siwezi muita mjinga kijana ambaye baba yake alikuwa hana uwezo hakusoma, huyo tamchukulia kama hakubahatika tu kupata elimu sio mjinga, na watu kama hao wako wachache sana duniani ambao wazazi wao hawana uwezo hata ya kuwanunulia nguo :A S shade:
 
kwani elimu inatengeneza mapenz? Wangap wamesoma na ndoa zao ni sifuri? Wangap hawajasoma na hawana kitu ila wamekubaliana na hali zao na wanaish kwa furaha na aman? Maprofesa wangap ndoa znawashnda? Na wakulima wangap wanakufa wamegandana kama luba? Elimu haina maana mbele ya mapenz,
 
jAMANI NINYI ACHENI: Kuna mfano mmoja halisi wa dada ambaye alikuwa na elimu ya kidato cha sita na akaolewa na kaka mwendesha pikipiki ambaye alikuwa hana shule na hajaelimika kwa lolote. ye kwake alijua kusoma tu na kuandika tena kwa kubabaisha. Baada ya dada kuolewa kilichofuata ni kulea mtoto mmoja baada ya mwingine hadi ndoto zake za kuwa lawyer zikafutika. Pia huyu mwanaume illiterate huwa hana shukurani kwa namna yule dada anavyojitahidi kuhakikisha anaanya kila analoweza familia iwe na mkate wa kila siku na kusomesha watoto. lakini yule kaka akaona haifai akamwachisha kijikazi alichokuwa nacho et akae nyumbani..... Ndo n=maisha gani hayo et kisa pesa ipo... LAZIMA MTU AWE NA UPEO WA MAISHA WALAU KUSOMA KUNASAIDIA MTU KWUA NA EXPOSURE!!!!!! SHULE MUHIMU JAMANI
 
jAMANI NINYI ACHENI: Kuna mfano mmoja halisi wa dada ambaye alikuwa na elimu ya kidato cha sita na akaolewa na kaka mwendesha pikipiki ambaye alikuwa hana shule na hajaelimika kwa lolote. ye kwake alijua kusoma tu na kuandika tena kwa kubabaisha. Baada ya dada kuolewa kilichofuata ni kulea mtoto mmoja baada ya mwingine hadi ndoto zake za kuwa lawyer zikafutika. Pia huyu mwanaume illiterate huwa hana shukurani kwa namna yule dada anavyojitahidi kuhakikisha anaanya kila analoweza familia iwe na mkate wa kila siku na kusomesha watoto. lakini yule kaka akaona haifai akamwachisha kijikazi alichokuwa nacho et akae nyumbani..... Ndo n=maisha gani hayo et kisa pesa ipo... LAZIMA MTU AWE NA UPEO WA MAISHA WALAU KUSOMA KUNASAIDIA MTU KWUA NA EXPOSURE!!!!!! SHULE MUHIMU JAMANI
A wonderful point of view, ubarikiwe sana 😛oa
 
elimu yako kutwa
unalalamika na ccm elimu nini bwana watu wana pesa nakutajia matajili
darasa la tatu.. nenda sinza au kkoo mbeya njombe songea ukikuta hotel
zote za kisasa zimeandikwa wanyama hotel mwenyewe std 3 rombo grean view
darasa la pili engeen mbezi beach za seif mwalabu kasoma chuo tu
madrasa hela ndio mpango nyie niaje

Nina dada yangu binamu alimaliza form 6 tu akaolewa na jamaa ambae ni std 7 leaver,jamaa ni mfanyabiashara amemsomesha mkewe kwa gharama zake(sasa yuko chuo anasoma masters) na amemwambia atamsomesha mpaka dada mwenyewe aamue hataki kusoma tena! Watoto wao wawili tu wanasoma academy homeworks,reports,diary anawaambia hiyo kazi ya mama. Ila maisha yao safi tu.
 
jAMANI NINYI ACHENI: Kuna mfano mmoja halisi wa dada ambaye alikuwa na elimu ya kidato cha sita na akaolewa na kaka mwendesha pikipiki ambaye alikuwa hana shule na hajaelimika kwa lolote. ye kwake alijua kusoma tu na kuandika tena kwa kubabaisha.
Charminggirl
Kuna mifano kama thelasini halisi (ya watu ambao hawakusoma) ila wana busara (Henry Ford.., Richard Bransom, Mzee Faraja.., Baba Athumani n.k n.k n.k.) wameoa na wamezaa na wanajukuu na maisha yao yanakwenda bila tabu yoyote

Baada ya dada kuolewa kilichofuata ni kulea mtoto mmoja baada ya mwingine hadi ndoto zake za kuwa lawyer zikafutika.
Uzazi wa mpango sidhani kama unafundishwa shule.., hii ni tabia ya mtu.., Kuja jamaa yangu Proffessor mmoja anawatoto kumi kwa mama mmoja na wengine kama 8 kwa kina mama tofauti, yeye ni toka nitoke yaani mimba baada ya mimba nadhani mke wake angekuwa na uwezo wa kuzaa watoto kila baada ya miezi mitatu jamaa angefanya hivyo.., na controlling ni tabia ya mtu na haifundishwi shule

Pia huyu mwanaume illiterate huwa hana shukurani kwa namna yule dada anavyojitahidi kuhakikisha anaanya kila analoweza familia iwe na mkate wa kila siku na kusomesha watoto. lakini yule kaka akaona haifai akamwachisha kijikazi alichokuwa nacho et akae nyumbani.....
Again hii ni tabia ya mtu, na upeo mfupi wa mtu, Babu yangu hakusoma wala alikuwa hajui kuandika ila alihakikisha watoto wake wote wanakwenda shule (yupo radhi kuuza shamba) na alimwandikisha mke wake kisomo cha watu wazima ili waweze kusoma barua za wajukuu (hivyo hii ni tabia ya mtu na has nothing to do na kwenda shule)

Ndo n=maisha gani hayo et kisa pesa ipo... LAZIMA MTU AWE NA UPEO WA MAISHA WALAU KUSOMA KUNASAIDIA MTU KWUA NA EXPOSURE!!!!!! SHULE MUHIMU JAMANI
No Doubt kusoma ni muhimu sana tena sana, exposure even more.., lakini lack of kusoma na exposure does not mean kwamba mtu atafanya hayo uliyosema, vile vile unaweza ukasoma lakini ukawa na tabia za kizamani (huenda hataki mke wake afanye kazi sababu ya wivu, sasa niambie shule gani inatibu wivu)
 
Last edited by a moderator:
Kuna mifano kama thelasini halisi (ya watu ambao hawakusoma) ila wana busara (Henry Ford.., Richard Bransom, Mzee Faraja.., Baba Athumani n.k n.k n.k.) wameoa na wamezaa na wanajukuu na maisha yao yanakwenda bila tabu yoyote

Yani wewe unashangaza sana, hivi ukiona kipofu anatembea na hapotei njia ndo na wewe unaweza kuwa kama yeye....Tumeisha sema maisha na elimu ni vitu tofouti kabisa...Maisha ni bahati na bahati ya mwezio sio yako, hebu nipe watu wanagapi dunaini walio soma wanamaisha mabaya na wangapi wasio soma wanamaisha mabaya....Afu nipe percentage of educated people na uneducated people wangapi wana masiha mazuri sana.


Uzazi wa mpango sidhani kama unafundishwa shule.., hii ni tabia ya mtu.., Kuja jamaa yangu Proffessor mmoja anawatoto kumi kwa mama mmoja na wengine kama 8 kwa kina mama tofauti, yeye ni toka nitoke yaani mimba baada ya mimba nadhani mke wake angekuwa na uwezo wa kuzaa watoto kila baada ya miezi mitatu jamaa angefanya hivyo.., na controlling ni tabia ya mtu na haifundishwi shule

Na nani anasema uzazi wa mpango haufundishwi shule, sa hao wanao fundisha walijifunzishia wapi? Matatizo yako wengi unachukulia mfano wa watu wachache wako vile...Kama huyo professor ambayo ni jamaa yako, lakini ukienda muliza yeye mwenyewe ma professor wangapi wanao zaa watoto wachache, atasema ni wengi kuliko wale wako kama jamaa huyo...We nenda kamulize kama hakujibu kama mimi.





Again hii ni tabia ya mtu, na upeo mfupi wa mtu, Babu yangu hakusoma wala alikuwa hajui kuandika ila alihakikisha watoto wake wote wanakwenda shule (yupo radhi kuuza shamba) na alimwandikisha mke wake kisomo cha watu wazima ili waweze kusoma barua za wajukuu (hivyo hii ni tabia ya mtu na has nothing to do na kwenda shule)



Hata babu zetu na baba zetu hawajasoma na wako ambao walikuwa hawajasoma wakawa viongozi wa nchi, na mmoja wao kiongozi wa UAE aliye fariki hajaenda kabisa shule, lakini wangapi wale hawajasoma wanao ongoza nchi sasa hivi?

Babu zetu walikuwa hawajasoma kutokana na wakati wao, wakati tulio nao kama huna elimu wewe huna kitu, na utaitwa mjinga labda uwe umerithi mali za baba/babu zako ndo utaozeshwa...Tena watakao kuozesha ni wale wazazi wajinga ambao hawana elimu ya kutosha :A S shade:

No Doubt kusoma ni muhimu sana tena sana, exposure even more.., lakini lack of kusoma na exposure does not mean kwamba mtu atafanya hayo uliyosema, vile vile unaweza ukasoma lakini ukawa na tabia za kizamani (huenda hataki mke wake afanye kazi sababu ya wivu, sasa niambie shule gani inatibu wivu])

Wewe kama unaona kusoma sio muhimu ni wewe tu sio sisi....Tabia na elimu ni vitu tofouti kabisa, ni sawa sawa na maisha na elimu ni vitu tofouti kabisa, elimu mana yake kuondoa ujinga :A S shade:
 
Wewe kama unaona kusoma sio muhimu ni wewe tu sio sisi....Tabia na elimu ni vitu tofouti kabisa, ni sawa sawa na maisha na elimu ni vitu tofouti kabisa, elimu mana yake kuondoa ujinga :A S shade:
Mkuu yaani umeongea mengi..., ila sijui unataka kusema nini (ebu nionyeshe ni wapi nimesema kusoma sio muhimu)

Point yangu ni kwamba kusoma sio guarantee kwamba mtoto wako au wewe utakuwa na maisha mazuri na partner wako (hivyo basi ni bora mwanao/wewe upate illiterate unayempenda au msomi usiyempenda)., uvumilivu, busara na kuendesha maisha hakuitaji degree., of course kusoma ni added advantage kwenye maisha, ila kutokusoma sio guarantee kwamba utashindwa maisha.., na tukianza kutoa mifano ya watu ni kupotoka (sababu every case should be judged according to its own facts).

Kwahio mkuu tukiangalia definition ya illiteracy hapo chini hususan kwenye bold:-


  1. The condition of being unable to read and write.


  1. An error, as in writing or speech, made by or thought to be characteristic of one who is illiterate. See Usage Note at literate.
  2. The condition or quality of being ignorant or unknowledgeable in a particular subject or field: cultural illiteracy; scientific illiteracy.

Utaona kwamba most of us tupo illiterate kwenye one subject or the other na mtu anaweza asiwe college/school smart ila akawa street smart, mwenye busara na anayejua kuishi na watu vizuri na kuendesha maisha.., hivi kumpenda mke/mume, kumuenzi, na kumuheshimu kunafundiswa shule gani ?, grade gani ?, na kwenye syllabus ipi ?.
 
Mkuu yaani umeongea mengi..., ila sijui unataka kusema nini (ebu nionyeshe ni wapi nimesema kusoma sio muhimu)

Kutokana na mazungumzo yako...Sijasema umesema kuna sehemu umeandika, nilipo highlighted kule ulikuwa umesema elimu ni mhumu sana, afu pale pale maneno yako yanasema vingine....Sa kama elimu ni muhimu kama unavyo sema, yanini tunabishana hapa...Au unataka tujaze maneno mengi tu :A S shade:
 
Hapa mimi naona kwa hali siku hizi kinachomata ni mshiko tu hata kama hujui kusoma wala kuandika lakini unamshiko wa kutosha utaonekana una masters na watakung'ang'ania kuanzia wazazi wao mpaka binti mwenyewe. Njooni huku mererani mwone
 
Back
Top Bottom