Je, Utaratibu huu wa 'Waswahili' una 'Baraka' za Mungu au labda kwa sasa Shetani 'anaupiga mwingi' Mioyoni mwetu?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Katika ngazi za Familia nyingi za Kiswahili utakuta Mtoto mwenye Mafanikio ya Kipesa kuliko Wenzake hata kama ni wa mwisho Kuzaliwa ndiyo anasikilizwa na Wazazi hata kama wale Wasiokuwa na Pesa ni Werevu na Wamesoma kuliko Yeye.

Katika Kamati mbalimbali za Jumuiya za Makanisa ( hasa langu la Katoliki ) Viongozi Wakuu wa Kamati hizo ni Watu wenye Hadhi za Kiuweledi Maofisini Kwao ila wale wasiokuwa nacho na ni Wafanyakazi wa Kawaida tu huwa hawapewi au hata hawachaguliwi katika nafasi za Kinyadhifa.

Katika Kamati mbalimbali za Sherehe ( hasa Harusi ) wale Wajumbe wa Kamati hizo huwa ni Watu wenye Pesa au Umaarufu fulani pia ila wale wasiokuwa nacho ( akina GENTAMYCINE ) tutapangiwa tu Kunawisha Mikono Wageni, Kuzoa Makombo yao ya Chakula, Kuosha Vyombo na Kuzurula tu kuangalia pale Ukumbini nani hajala au hajapata Kinywaji au ameshavimbiwa na Chakula kwa Uroho ( Umelo ) wake anataka kwenda Kunya ( Kuukweka ) Chooni na tunatakiwa Kuwaelekeza vilipo.

Je, yote haya yanampendeza Maulana?
 
Lazima iwe hivo ili na wew upate uchungu wa kupambana kutafuta pesa
Duniani wote tukiwa na Pesa, Utajiri na Mafanikio Mambo yataenda baina ya Wanadamu?

Wewe uliingia Akilini kwa Mwenyezi Mungu na akakuambia kuwa hawa ( hao ) wasiokuwa nacho sasa watakuwa hivyo daima na Wewe Utajiri wako utadumu nao?

Umeshajiuliza ni kwanini Matajiri wengi wenye Kujitambua hupenda sana Kujishusha na Kutowadharau wasiokuwa nacho na tena huwashirikisha katika Mipango yao na hujikuta si tu wanaishia Kuendelea kuwa Matajiri ila pia hupendwa na huombewa Baraka zaidi na wale wasio na Kipato cha Utajiri kama wao?

Sasa mbona mkifa hamzikwi na Pesa zenu?
 
Pambana mtoto wa kiume acha kulalamika.. utu uzima bila pesa utamwamkia mpaka mtoto. Umasikini ni laana, sali omba mungu fanya kazi kwa bidii utafanikiwa. ..
 
Nimeanzisha Uzi Kuwasilisha Ujumbe muhimu sana ambao kwa Mpumbavu kama Wewe ni ngumu kujua.

Kwani hakuna Watu wanaofanya Kazi lakini bado tu ni Masikini? Unajua dhana pana ya neno Masikini / Umasikini?

Mnakimbilia humu Mitandaoni kujitapa ( Kujimwambafai ) mna Pesa huku huko Vijijini Kwenu Wazazi wenu wanataabika tu na hata Kushindia Mizizi na Uji.

Mshamba mkubwa Wewe. Kwahiyo unaposema kuwa Umasikini ni laana unataka kusema 65% ya Masikini waliopo Ulimwenguni wamelaanika?
 
Kumbuka, aliyebarikiwa duniani kabarikiwa na mbunguni. Lkn pia hakuna kinyonge kitakacho urithi ufalme wa mbingu. Umaskini ni unyonge
 
Kwahiyo Wanyonge wote tu ni Masikini?
 
HAMNA, HAPANA, HAKUNA, HAIPENDEZI
We antibiotic mm ni wa kwanza na nina mkwanja kuliko wote pale home nimewajengea na nyumba wazee na nikawaleta shamba mkata wanaishi kwangu nawahudumuia kwa mengi including nimewakatia bima ya afya lakini wanamsikiliza dogo wa pili toka mwisho kuna wazee makauzu
 
Katika ngazi za Familia nyingi za Kiswahili utakuta Mtoto mwenye Mafanikio ya Kipesa kuliko Wenzake hata kama ni wa mwisho Kuzaliwa ndiyo anasikilizwa na Wazazi hata kama wale Wasiokuwa na Pesa ni Werevu na Wamesoma kuliko Yeye.

Katika Kamati mbalimbali za Jumuiya za Makanisa ( hasa langu la Katoliki ) Viongozi Wakuu wa Kamati hizo ni Watu wenye Hadhi za Kiuweledi Maofisini Kwao ila wale wasiokuwa nacho na ni Wafanyakazi wa Kawaida tu huwa hawapewi au hata hawachaguliwi katika nafasi za Kinyadhifa.

Katika Kamati mbalimbali za Sherehe ( hasa Harusi ) wale Wajumbe wa Kamati hizo huwa ni Watu wenye Pesa au Umaarufu fulani pia ila wale wasiokuwa nacho ( akina GENTAMYCINE ) tutapangiwa tu Kunawisha Mikono Wageni, Kuzoa Makombo yao ya Chakula, Kuosha Vyombo na Kuzurula tu kuangalia pale Ukumbini nani hajala au hajapata Kinywaji au ameshavimbiwa na Chakula kwa Uroho ( Umelo ) wake anataka kwenda Kunya ( Kuukweka ) Chooni na tunatakiwa Kuwaelekeza vilipo.

Je, yote haya yanampendeza Maulana?
Kwenye misiba hata inayowahusu wao hawachimbi kaburi wala kubeba jeneza. Wao wanachaguliwa taji zuri la kiweka juu ya kaburi huku wakiweka kwa pozi la picha.
 
Back
Top Bottom