Je, utaratibu upoje kuhusu mirathi?

Je, utaratibu upoje kuhusu mirathi?

mdathiru

New Member
Joined
Jan 25, 2022
Posts
1
Reaction score
1
Rafiki angu mmoja wazazi wake wawili wamefaliki yeye ndo mtoto wa kwanza wa kiume lakini pia ni mtoto wa kambo yani mama ake aliolewa na mwanaume mwingine baada ya kuachana na baba ake mzazi mama ake alikua mtumishi na alibahatika kuwa na nyumba na viwanja kwa majina yake na aliandika urithi na idadi ya watoto wake.

Aliepewa usimamizi wa mirathi baada ya wazazi kufariki ni dada wa rafiki yangu na mahakama ilimtaka kufikia mwezi wa kwanza mwaka huu arudishe majibu ya namna alivozigawa mali au walivokubaliana kama familia lakini mpaka sasa Msimamizi wa mirathi ambae ni dada mtu yupo kimya na ndugu wengine wapo kimya je kaka mtu anaweza chukua hatua gani kisheria ili apate haki yake?
 
Rafiki angu mmoja wazazi wake wawili wamefaliki yeye ndo mtoto wa kwanza wa kiume lakini pia ni mtoto wa kambo yani mama ake aliolewa na mwanaume mwingine baada ya kuachana...
Aende mahakama iliyomthibitisha huyo dadayake kuwa msimamizi wa mirathi aombe order ya kumwita huyo dada ili aieleze mahakama na wanufaika kwaujumla kwanini mpaka sasa hajagawa mirathi kama wosia ulivyoelekeza.

NB: ikiwa ni mahakama ya mwanzo anaweza kwenda moja kwa moja kuomba order yamahaka, lakini mahakama zingine order inaombwa kwa documents za kisheria (court forms).

AWASILIANE NA MWANASHERIA WAKE ILI AWEZE KUMUONGOZA.
 
Naomba msaada: file la mirathi kutoka pspf kwenda mahakama kuu inachukua muda wa miezi mingapi kwa makadilio mbaka kutoa hela za mirathi?? naomba msaada
 
Back
Top Bottom