Je, utaratibu wa Serikali kuwapangia wahitimu sekondari vyuo binafsi umerudi?

Je, utaratibu wa Serikali kuwapangia wahitimu sekondari vyuo binafsi umerudi?

kmbwembwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
10,892
Reaction score
7,780
Kwenye awamu ya nne elimu ilivurundwa sana hadi wahitimu wa form four kupangiwa chuo kikuu tena na kupewa mkopo kwa kisingizio cha kuandaa waalimu huku vigogo wakiwapangia jamaa zao ambao hata sifa hawana. Tulifikia mahali ambapo wahitimu form six walikua wanapangiwa vyuo vikuu binafsi kwanza hadi vijae wanafunzi wakati vyuo vikuu vya serikali vinakosa wanafunzi.

Chuo Kikuu cha Dodoma kwa mfano kilikua kinapata wanafunzi kama theluthi tu ya uwezo wake, wakati chuo kikuu cha Dar es Salaam nacho kilikua hakijai idadi ya wanafunzi. Yote hayo yalikua yanawezekana kutokana na viongozi vyuo binafsi kutoa rushwa kwa mamlaka za kupanga ambapo wanafunzi wakawa wanapangiwa vyuo binafsi japo maombi yao ni vvuo vya Serikali.

Katika awamu hii ya 6 yenye kushutumiwa kukubali kurejesha mafisadi serikalini na kukumbatia wafanyabiashara binafsi nimepata mshituko kuona binti wa ndugu yangu aliyefaulu vizuri masomo ya sayansi div 3 akiwa amepangiwa kwenda chuo cha uganga binafsi wakati hakuchagua chuo hicho. Ada kwa mwaka inastaajabisha kwa ukubwa kulinganisha na kama angepangiwa chuo cha serikali. Wazazi wa huyo jamaa yangu ni watu wenye uwezo mdogo kifedha na wanaona hawata mudu gharama hizo.

Kutokana na hiki nilichokijua inaelekea kile kilichodhibitiwa na awamu ya tano kimerejea tena.

Hapo nyuma kabla ya ufisadi kokomaa kwenye awamu ya nne vyuo binafsi vilikua na utaratibu wao binafsi wa kupata wanafunzi na sio kupangiwa na serikali.

Kwa maoni yangu naomba uongozi wa samia kujihadhari na vigogo kwenye serikali yake wanaojidai kuleta taratibu mpya kila nyanja kama ndio njia bora. Ukweli ni mafisadi tu wala rushwa wabaya na wataifarakanisha serikali ya CCM na wananchi.
 
aliyefaulu vizuri masomo ya sayansi div 3 akiwa amepangiwa kwenda chuo cha uganga binafsi wakati hakuchagua chuo hicho
Chuo cha serikali, CLINICAL MEDICINE IF IT IS WHAT YOU MEANT, hupati kwa pass hizo, never on earth! Sana sana huwa ni Div 1 ; na 2 ya mwanzo ingawa nayo ni very rare!

Hoja yako iwe kupangiwa vyuo binafsi, hilo si sawa. Akikosa chuo cha serikali alichoomba, huwa hapangiwi chuo cha binafsi. Hapo kweli kuna rushwa. RAIS SAMIA Fukuza takataka zote NACTE
 
Chuo cha serikali, CLINICAL MEDICINE IF IT IS WHAT YOU MEANT, hupati kwa pass hizo, never on earth! Sana sana huwa ni Div 1 ; na 2 ya mwanzo ingawa nayo ni very rare!

Hoja yako iwe kupangiwa vyuo binafsi, hilo si sawa. Akikosa chuo cha serikali alichoomba, huwa hapangiwi chuo cha binafsi. Hapo kweli kuna rushwa. RAIS SAMIA Fukuza takataka zote NACTE
Kwani hoja yangu ni nini kama sio hiyo kupangiwa chuo binafsi wala hajaomba. Chuo chenyewe kipo Dodoma.
 
Nyie MATANGA tulieni bhana acheni chochoko, maana hata vyuo binafsi vinatoa ajira kwa watanzania wenzetu
 
Back
Top Bottom