Je, UTI ni ugonjwa wa ngono?

Je, UTI ni ugonjwa wa ngono?

Daata

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2012
Posts
4,673
Reaction score
1,875
Wasalaam Sana wajumbe.

Kumekuwa na dhana iliyojengeka miongoni mwa wanajamii kuhusu ugonjwa wa Urinary Track Infection UTI ambao unawakumba watu wengi nyakati hizi bila kujali umri wala mazingira anayo kaa mtu.

Je UTI ni ugonjwa unaoambukizwa kwa kujamiiana.? Nauliza hivi kwa Sababu Kuna msemo umezoeleka wa kusema ukitaka UTI sugu tembea na binti mwenye tabia hizi na hizi, hasa tabia za kuwa na Wanaume wengi.

Ukirejea kwenye uhalisia bado hiyo hoja inakosa mashiko kwa Sababu Kuna watoto wadogo ambao nao wanaugua UTI na bado hawajuani na mambo mahusiano.

Je, usugu wa UTI unasababishwa na zinaa na watu mbali mbali au Kuna mazingira mengine changishi.

Nawasilisha.
 
Wengine hatufanyi chochote, tena hatutumii toilet za public tena under wear tunapiga pasi, ukienda medical check ups unasikie oops una UTI eeh japo siyo nyingi,....
sheet...
Na hiki ndio kinanifanya niamini kuwa UTI sio ugonjwa wa ngono
 
Wasalaam Sana wajumbe.

Umekuwa na dhana iliyojengeka miongoni mwa wanajamii kuhusu ugonjwa wa Urinary Track Infection UTI ambao unawakumba watu wengi nyakati hizi bila kujali umri wala mazingira anayo kaa mtu...
Kuchangia Vyoo hasa Vyoo vyetu hivi vya kisasa!
 
Wasalaam Sana wajumbe.

Umekuwa na dhana iliyojengeka miongoni mwa wanajamii kuhusu ugonjwa wa Urinary Track Infection UTI ambao unawakumba watu wengi nyakati hizi bila kujali umri wala mazingira anayo kaa mtu...
Hapana,
Ni dhana iliyojengeka tu kwa watu! Kama ulivyosema kwamba dhana au hoja yenyewe huhusishwa na mtu kuwa mahusiano (kufanya ngono) na watu wa aina mbalimbali! Kinachoambukizwa kwa ngono ni magonjwa ya zinaa.

Kwa hiyo ni jina tu limebadilishwa kutoka magonjwa ya zinaa na kuwa UTI sugu! Hakuna UTI sugu!
 
Wasalaam Sana wajumbe.

Umekuwa na dhana iliyojengeka miongoni mwa wanajamii kuhusu ugonjwa wa Urinary Track Infection UTI ambao unawakumba watu wengi nyakati hizi bila kujali umri wala mazingira anayo kaa mtu...
Sio wa ngono lakini ngono inatengeza urahisi pia na unaye ngonokabnaye
 
Mnaposema U.T.I huwa mnaongelea maambukizi au htilafu katika eneo gani hasa ?
DR Mambo Jambo spidernyoka
Tunaposema U.T.I tunamaanisha ni Urinary tract infections ambayo ni maambukizi katika mfumo wa mkojo
UTI kitaalamu zimegawanyika makundi mawili Upper &Lower

Maambukizi yanasababishwa zaidi na bacteria mlinzi wa mfumo wa chakula E coli huyu ni normal flora akiwa kwenye tumbo na anakua muharibifu akiingia kwenye mfumo wa mkojo

Mfumo wa mkojo unahusisha kutokea chini
Ureta & urethra
Kibofu
Mirija
Figo
 
Back
Top Bottom