Wasalaam Sana wajumbe.
Kumekuwa na dhana iliyojengeka miongoni mwa wanajamii kuhusu ugonjwa wa Urinary Track Infection UTI ambao unawakumba watu wengi nyakati hizi bila kujali umri wala mazingira anayo kaa mtu.
Je UTI ni ugonjwa unaoambukizwa kwa kujamiiana.? Nauliza hivi kwa Sababu Kuna msemo umezoeleka wa kusema ukitaka UTI sugu tembea na binti mwenye tabia hizi na hizi, hasa tabia za kuwa na Wanaume wengi.
Ukirejea kwenye uhalisia bado hiyo hoja inakosa mashiko kwa Sababu Kuna watoto wadogo ambao nao wanaugua UTI na bado hawajuani na mambo mahusiano.
Je, usugu wa UTI unasababishwa na zinaa na watu mbali mbali au Kuna mazingira mengine changishi.
Nawasilisha.
Ugonjwa waUTI(Urinary Tract Infection) siyo ugonjwa wa ngono. Hii inatokana na kwamba wadudu/bakteria/virusi wanaosababisha UTI hawana uwezo(adapted) kuhamishwa toka mtu mmoja kwenda mwingine kwa njia tajwa.
UTI nyingi ni za kujiambukiza hasa kwa wanawake kutokana na changamoto ya kimaumbile. Changamoto hii pia inaweza kuchochea suala hili kutokea wakati wa ngono, laki si njia rasmi ya maambukizi.
Wadudu/bakteria/virusi wanaoweza kuhamishwa toka mtu mmoja kwenda mwinginekwa njia yango huwekwa kwenye kundi la ugonjwa wa STI(Sexual Transimitted Infection).
TIBA KWA UTI
1: Unapopatikana na UTI ni vyema kutumia dawa uliyopewa kwa kadri ya maelekezona kumaliza dozi. Unapomaliza dozi ni vyema kupima naafa ya siku mbili au tatu kuona kama umepona au la. Kama haujapona ni vyema KUOTESHA mkojo husika na kutibu kadri ya majibu husika.
2: Kwa watoto, hasa wa kike: Kuhakikisha usafi wa nguo zao za ndani, kutokuwaacha na mkojo au choo kikubwa kwa muda mrefu na kuwafanyia usafi mara tu wanapokuwa wamejisaidia.
3: Kutokutumia wipes zenye pombe/alcohol sehemu za siri. Huvuruga balansi ya aina ya bakteriakwenye njia ya uzazi.
KUHUSU UTI KUONGEZEKA KWENYE JAMII
Ni suala mtambuka, sababu ni nyingi kati ya hizo:
1: Ongezeko la vituo vya afya.
2: Uwepo wa teknolojia ya ugunduzi.
3: Mabadiliko kwenyemfumo wa maisha ie. Pampers
4: Ulaghai wa majibu/faida.
5: Uelewa wa utafsiri wa majibu/kutokuwa na elimu ya kutosha
6: Ongezeko la idadi ya watu.
7: Nk.