Je, uwekezaji UTT ni mbadala sahihi wa Real Estate Tanzania?

MR BINGO

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2016
Posts
1,164
Reaction score
2,500
kipi ni bora kwa uwekezaji TANZANIA kati ya kuwekeza katika biashara ya nyumba au kuwekeza katika mfuko wa hifadhi wa UTT??

Let's say una milion 30 ni bora ujengee nyumba in which utapata kodi labda ya 250k au ni bora uwekeze kwenye UTT in which ina return ya labda 1% per month ambayo ni kama 300k

Na kwa upande wa risk management pia naona kuwa it's less risky kuwekeza kwenye UTT kuliko kwenye numba kwa sababu in real estate kuna mambo ya kudeal na wapangaj(kuchelewesha kodi, eviction notices n.k)na kuna muda nyumba inakuwa haina mpangaji in which ni hasara kwa muwekezaji,pia kuna gharama za uendeshaji vitu kama kodi ya jengo na ardhi n.k

kipi ni bora UTT OR REAL ESTATE??
 
Mimi sipendi kuwekeza hela yangu sehemu moja kwakweli, kwenye 30m ningeweka 15m kwenye UTT na 15 kwenye ardhi(Nyumba).

Kwenye biashara zangu zote 50% yake naongezea kwenye hio biashara. Na 30% naweka kwa kufungua uwekezaji mwengine, na 20% hii huwa yangu mimi.
 
hii ni nzuri pia ila nyumba tuseme ya 15milion nadhani itakuwa less marketable na uwezekano wa kuleta faida utakuwa mdogo pia labda kununua ardhi ya 15m then usikilizie miaka kadhaa uuze
 
inawezekana ardhi ina ROI kubwa lakini pia nadhani ina take some time kumature ili uweze kupata faida kubwa
Inategemea na sehemu, Kama umenunua sehemu inayojengeka kwa kasi, itachukua muda mfupi kupata faida nzuri.

Ni kweli, uwekezaji wowote unahitaji muda ili kupata faida nzuri.
 
Mimi nishafanyia maamuzi.. Nina hela UTT zenye thamani ya nyumba 4 last two weeks nimeingia DSE nataka na kwenyewe niweke mzigo nikajifunze zaidi kwa broker na ikiwezekana nipunguze mzigo wa UTT niweke DSE. Sina nyumba physical nimepanga mpaka leo.
hii nzuri DSE nako risk onaongezeka kidogo na faida nsyo inaongezeka kidogo
 
hii ni nzuri pia ila nyumba tuseme ya 15milion nadhani itakuwa less marketable na uwezekano wa kuleta faida utakuwa mdogo pia labda kununua ardhi ya 15m then usikilizie miaka kadhaa uuze
Point yangu ilikuwa ni kutowekeza hela sehemu moja, Nyumba ya 15m labda ujenge mabondeni huko.

Kwenye ardhi inategemea na sehemu mkuu sio kila sehemu ununue tu. Kuna watu wanafanya utafiti wanakwambia miaka 10 hadi 20 ijayo sehemu hii itakuwa ina bei kubwa sana.

Mfano mdogo kuna watu waliwekeza Kigamboni miaka hio kiwanja unapata kwa 3m mpaka 20m lakini sasahivi akitaka kuuza anapata 300m mpaka 1b kama ni nyumba kubwa. Au kule Mbweni miaka 10 nyuma kiwanja cha bei hali ilikuwa 20m mpaka 150m sasahivi bei zake nadhani umezisikia.
 
Kwa mtazamo wangu ni vitu ambavyo vinapaswa kutengeneza balance ya utajiri wako kwa maana ya kuwa havitakiwi kimoja kuwa mbadala wa mwingine ila vinatakiwa vyote kuwa columns zinazolinda your wealth againts inflations

Kwa ufupi kikubwa cha kuzingatia ni kuwa kila kimoja kifanyike kwa wakat sahihi

UTT inaweza kuwa ya kuanzia katika kukuza mtaji kwan inaruhuau uwekezaji wa kudunduliza then real estate ikawa inatumika kulinda thaman ya pesa yako na vikawa vinakupa support ya kifedha mfano kwa UTT kupata gawio na kuweza kuwa cushion au colateral on those rainy days. Kwa real estate pia itakupa support ya kodi na pia kuwa colateral.. changamoto ya Nyumba ni kuwa ubora wa nyumba uendane na ubora wa mazingira yanayozunguka .. maana hivyo ndio vitakavyo determine kufanikiwa kwake kwan mazingira ya eneo na ubora wa nyumba ndio vinaonyesha una target wapangaji wa aina gani

Mfano kuwe na watu wawili wote wakajenga au kununua nyumba maeneo ya kawe au mwenge mmoja akaamua atarget middle
Class kwa bei ya kati ya 300k hadi 700k kwa mwez kutegemea na eneo wa pili akaamua kuifanya AirBNB kwa bei kati ya 80k hadi 120k kwa siku

Utaona mwenye Air BNB katika mwez mmoja wa siku 30 akifanikiwa kupata watu wa AirBNB kwa siku 15 tu anapata pesa zaidi kuliko anaepangisba kwa mwezi ingawa pia atakuwa na maintanance and service cost za kila mwez.. lakini pia wa uoangaji wa mwezi ana advantage ya kuipata pesa ua uoangahiwa wa mda
Mrefu kwa mara moja (6mo au 1yr) bado wote hao wakawa pesa zao za upangishaji wanazipeleka UTT .. so utaona idea zote mbili zinaweza kwenda sambamba kwa kutegemea mazingira ya mtu na hali yake ya kifedha kwa wakat huo hasa mirija yake mingine ya upatikanaji wa fedha

Kama mirija mingine hailet ya kutosha au mtiririko wake sio fixed kama vile salary basi tumia UTT kukuza mtaji zaid ya hito 30m huku hiyo 300k ya kila mwez uki reinvest.. ( infact haifiki 300k)
 
Kusema ukweli uwekezaji mzuri NI ule ambao hauna risk kubwa lakini tatizo utt haujifunzi kitu, ukisema uwekeze kwenye nyumba za kupangisha nibmwanzo mzuri kwasababu unamengi ya kujifunza biashara za majengo NI nzuri Sana lakini Kuna ule uzoefu unaopata kudeal na mafundi wapqngaji huo sio usumbufu hapo unajifunza biashara ni afadhali uwekeze kwenye nyumba ndugu yangu nibrahisi hata kurithisha kizazi chako pesa za utt hazina paper na field work nyingi ambazo ndizo zinazotukutanisha na watu na kupata fursa zaidi.
Au fanya hivi peleka pesa utt halafu faida unayoipata fanyia ujenzi kidogokidogo
Robert Kiyosaki (nguli wa uwekazaji katika majengo sqahiba wake Trump)anasema investing is game unatakiwa uenjoy Mchezo wenyewe kuliko matokeo na zaid NI kupata uzoefu mpya na namna ya kusolve changamoto unazokumbana nqzo kila siku katika uwekezaji huo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…