Je, uwepo wa Dini ni sababu ya Afrika kutokuendelea?

Hoja hii inafanana na tabia ya mara kwa mara ya kutafuta mbuzi wa kafara (scapegoat) wa kumtupia lawama zote za udhaifu wetu, badala ya kugusa na kuibua changamoto halisi, zenye uzito, na zinazoweza kutatulika.

Inakuwa rahisi sana kuisukumia dini mzigo wote wa matatizo badala ya kuangalia mifumo ya utawala, ubora wa elimu, sera za kiuchumi, nidhamu ya kazi, na matumizi ya rasilimali zetu. Dini ni chombo—ambacho kinaweza kutumiwa kujenga nidhamu na maadili, au kutumiwa vibaya kufanya watu wawe wavivu—lakini siyo msingi pekee unaoamua hatima ya bara zima.
 
Kwahiyo kikwazo cha maendeleo ya Afrika ni Nini embu tueleze!!!!!
Tatizo kubwa haswa ni kuwa na mifumo inayolinda watu badala ya sheria, tuna viongozi wasio na maono ya mbali, tunafanya sana siasa za kujinufaisha badala ya kufanya siasa za maendeleo. Nchi haiwezi kuendelea kama kila anayeingia madarakani anawaza uchaguzi ujao badala ya kizazi kijacho.

Elimu yetu pia Afrika ni tatizo maana inamuandaa mtu kuwa mfanyakazi badala ya kuwa mbunifu au mjasiriamali, tunakaririshwa historia ya akina Vasco da Gama badala ya kufundishwa coding, technology, na ujuzi unaoweza kuzalisha viwanda. Kifupi tunazalisha wasomi wenye vyeti lakini hawana ujuzi wa kutatua matatizo ya kijamii.
 
Hayo ndio mambo ya msingi ya kuangaliwa sio mtu anakazana tu kuitupia mizigo ya lawama dini Tena kinacho kela wakisema Dini mara nyingi wakiulenga uislamu ni ujinga kabisa!!!!!
 
Kwahiyo mashekh ndio kikwazo cha maendeleo ya Afrika? Au wewe ujasoma hii mada vizuri?
Labda wewe ndo hujaelewa mada,dini zimekuwa kikwazo cha maendeleo hasa dini ya kiislamu imekuwa imekuwa kikwazo kikubwa
 
Italy na saudi arabia kote kuna dini lakini Cha ajabu wamepiga hatua kutuzidi sisi huku nafikiri ni nature ya watu tu
 
Labda wewe ndo hujaelewa mada,dini zimekuwa kikwazo cha maendeleo hasa dini ya kiislamu imekuwa imekuwa kikwazo kikubwa
Ww ndo aina ya watu wapumbavu anao wazungumzia mtoa mada .
Malawi,zambia,uganda,zimbabwe,congo nchi ambazo idadi ya waislam hawafiki hata %5 zina nn kuizidi Tanzania,Senegal,au Tunisia zenye waislamu wengi ?
Au dodoma yenye waksito wengi ina kipi cha ajabu kuizidi Tanga yenye waislamu wengi?
Uislam ni kikwazo cha maendeleo ya kwamba kwenye Quran kuna andiko linalo sema kuwa waumini wasitafute pesa au wasijenge?au kuna andiko linalo sema kuwa viongozi wawe mafisadi washindwe kuwaletea maendeleo wananchi wao?
 
Tatizo limeanzia hapa.
Kuna viongozi wa dini walitengenezwa na serikali kuwajaza hofu "ya Mungu" wananchi wanapokuwa kwenye ibada,ikatengenezwa miujiza fake na ikaaminiwa na waumini,kwa kuwa serikali ilihusika haikukemea matokeo ndiyo haya ya kushinda makanisani kuomba miujiza itende anavyo taka muumini.
Moses Kolola, Emmanuel Lazaro,kisha akina Kakobe na kizazi chake ndiyo wametufikisha hapa kwenye imani ya miujiza kwa msaada wa viongozi serikalini
 
Mwenye fikira za hivyo ni mpumbavu na hizo fikira zake ndo kikwazo cha maendeleo ya Africa.
Utasemaje kuwa uislam ni kikwazo cha maendeleo ya Afrika hali ya kuwa eneo la kusini mwa jangwa la Sahara ambalo ndo kuliko jaa nchi masikini kuliko sehemu yeyote duniani %70 ya watu wake ni wakrsito,aya tukubali kuwa Gambia haina maendeleo kwa sababu ya uislam wake ,je na Malawi haina maendeleo kwa sababu gani hali ya kuwa uislam hakuna?
Waafrica tusipo acha tabia ya kukwepa uwajibikaji kwa kujificha nyuma ya kundi fulani kuwa ndo wabaya wetu basi tusahau kupata maendeleo.
 
Awezi kukuelewa huyo analeta ushabiki
 
islam destroyed nations, hata iran zamani illitwa persia kabla ya islam ilikuwa na advanced civilization mpaka siku ilipokuwa conquered na islam, kuanzia hapo persia na ustaarabu wote ulianza kupotea, iraq Mesopotamia ilikuwa na civilization iliyosimama mpaka walivyokuwa conquered na islam leo hii irak kwisha tribal lords wanapigana kila siku kila mahali ni hivyo siria leo hii ni poorest country in the world, afghstan, north afrika civilizaztion iliyokuwepo egypt leo hii ilipaswa iwe first world country lkn walikuwa conquered na islam na leo egypt ni third world developing country, lebanon before islam well developed country, north afrika yote before islam conquest ilikuwa cvilization ya hali ya juu,.

so, yes if you look at the patterns unaona islam destroys nations, hata tanzagiza tu unaweza kuangalia patterns nepotism, massive corruption scandals kama epa, escrow & co. corruptions kubwa ktk historia ya tanzagiza ni chini ya uraisi wa muslims, bado sijagusia kuuza na kupora maeneo ya wazi, kufukuza wananchi kwenye ardhi yao kugawa kwa wageni, kubomoa national parks zetu, only muslims do this ...
 
Sahihi
 
Usisahau dini ipo Irani , Israel na nchi zingine nyingi
 
Kwahiyo Iran yenye techinologia unaifananisha na nchi za Afrika?
 
Kwahiyo Iran yenye techinologia unaifananisha na nchi za Afrika?

hauelewi irani au persia haikupswa kuwa hapo ilipo leo hii inaomba omba, persia ilipaswa iwe mbali sana na dunia nzima ilitakiwa iwe inakwenda kujifunza persia, ilipaswa iwe kama USA au EU, ila tangia walivyokuwa conquered na islam walianza kushuka na mpaka leo hii wanategemea msaada ya russia au china ili wa-survive, wakati persia was big with advanced civilization before islam ...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…