Je, uwepo wa Dini ni sababu ya Afrika kutokuendelea?

Kikwazo cha Africa siyo dini, wala elimu, hivyo ni vichaka tu vya kufichia upumbavu wetu, tatizo kubwa ni ubinafsi na kutokujitambua, Mungu alivyomuumba mwanadamu alimpa akili, akili inazaa maarifa, sisi Africa hayo maarifa hatuyataki, kwa maana hatuzifikilishi akili zetu, na akitokea kiongozi au mtu ambaye ana nia ya dhati kusaidia watu, basi anaanza kuchukiwa na viongozi wenzie na watu wachache wanaonufaika na mfumo ,viongozi wa Africa ni tafsili ya uchawi, hadi shetani mwenyewe anaogopa roho za viongozi wa Africa ni mbaya sanaa
 
Lengo la kuanzishwa kwa dini haikuwa kuwafanya watu wawe wajinga.

Dini ni muanga mmoja kati ya waanga wengine. Ila siku zote "Mjinga ni mtaji kwa mwerevu hasiye na hekima"

Wajanja wametumia mgongo wa dini kwa matakwa yao wenyewe. Lakini dini haikuanzishwa kwa lengo la utapeli.

Kisu kilitumika kwa matumizi ya asili kukatia matunda, nyanya, vitunguu nk~ lakini jambazi hutumia kisu hichohicho kuwadunga watu na kuwaua.

Hosea 4:6
"Watu wangu wanaagamia kwa kukosa maarifa" NA SIO VINGINEVYO
 
Ukiwa na imani ya dini, imani ya kweli kabisa, unamuachia mambo Mungu na kuomba sana badala ya kufanya kazi. Kimsingi unatakiwa kuishi kwa methali ya "Jitihada haizidi kudura".

Hata suala la uwajibikaji unalolisema kimsingi linatoweka, kwa sababu utasema tunaishi kwa neema za Mungu si kwa ujuzi na uwajibikaji wetu.

Dini is inherently unscientific. Na inatumika kudumaza demokrasia, kudumaza maendeleo. Badala ya watu kudai haki zao hapa duniani, wanaambiwa hapa wanapita tu, waangalie zaidi uzima wa milele na kuitafuta pepo na kuepuka moto.

Ctitique yako ina contradictions.
 
Ni kweli wengi ni religious badala ya kuwa spiritual. Wapo busy na Dini badala ya kuwa busy na Mungu!
 
Sahihi, na nddio nilicho kieleza kwenye comment yangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…