- Source #1
- View Source #1
kumekuwa na video kadha wa kadha zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii zikionyesha watu wakiishi na kufanya shughuli zao chini ya daraja.
- Tunachokijua
- Kupitia mitandao ya kijamii kumekuwa na kipande cha video kinachowaonesha baadhi ya watu wakiishi juu ya daraja na kuhusishwa na maeneo tofauti barani Afrika.
JamiiCheck iliwashirikisha wadau kupata maoni yao kuhusu uhalisia wa video hiyo ambapo wengi walibainisha kuwa video hiyo haikuwa halisia kutokana na doasri walizozibainisha.
Mathalani mdau mmoja kupitia JamiiCheck.com aliandika
"Kwa kutumia njia za ufuatiliaji wa kidijitali, imebainika kuwa video inayoonesha baadhi ya watu wakionekana kuweka makazi yao katika eneo la reli ya Standard Gauge Railway (SGR) imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya akili unde
Uchunguzi umeonesha kuwa video hiyo si tukio halisi, kwani katika mazingira ya kawaida si jambo linalowezekana kwa watu kuweka makazi na kuishi moja kwa moja kwenye njia ya reli ya SGR, ambayo imeundwa kwa ajili ya kupitisha treni kwa usalama."
Hata hivyo jamiiCheck kupitia nyenzo za kidigitali ya kubaini maudhui yaliyotengenezwa na AI, sambamba na dosari nyingine imebainika kuwa video hiyo si halisi na imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya akili unde.