Waacheni wananchi waamue nani anawafaa kuwa mwakilishi wao. Nyie na huo usomi wenu mbona hatuoni impact yoyote kwenye maeneo mliyokabidhiwa kulitumikia taifa?
Watu wanaowekea mkazo viwango vikubwa vya usomi kwenye ubunge hawaelewi demokrasia ni nini.
Hawaelewi kabisa demokrasia ni nini, na hili linanipa swali, kama hawaelewi demokrasia ni nini, hata huo usomi wenyewe wanauelewa?
Kuna mifano mingi sana ya jinsi gani kutegemea sana huu usomi ( hususan wa makaratasi) kunavyoweza kutuangusha.
Nitatoa michache hapa.
Kabla ya kuingia kwenye mifano hii, naomba nieleweke kuwa mimi si wale "anti-intellectuals" wanaopingana na usomi. Lakini pia mimi si wale watu wavivu ambao hata definition yao ya usomi ni narrow sana, basically paper qualification ndiyo wanaita usomi. Nakataa extremes zote mbili hizi.
Katika watu wanaopenda usomi, mimi nafikiri nimo. Nasoma sana, at least by our standards. Nafuatilia sayansi na falsafa, napenda critical thinking, immanent critique, logical thinking, mambo ya ethics, natafuta real value as opposed to veneer of intellectuallism as part of status anxiety etc.
Kabla ya mtu yeyote kunilaumu, selewe kuwa napinga usomi, aelewe kuwa hii ni immanent critique, sehemu ya usomi.Si kupinga usomi.
Mfano wangu wa kwanza nautoa katika vitabu vya biography ya Nyerere vya "Development as Rebellion: A Biography of Julius Nyerere". Katika moja ya vile vitabu, nafikiri cha Shivji, kuna habari ya Nyerere alivyohitaji ushauri kuhusu kutaifisha maduka. Nyerere alikuwa hajaamua kama serikali itaifishe maduka makubwa tu, au itaifishe maduka yote mpaka ya waswahili mitaani.
Akawatafuta washauri wake wa uchumi. Wakamwambia taifisha kila kitu mpaka maduka madogo. Nyerere akawa analifikiria lile jambo. Akasema anahitaji kulihakiki kwa watu zaidi. Akamtafuta Mzee mmoja wa CCM. Mzee wa Dar tu alikuwa kiongozi wa Yanga, si msomi wala nini. Ila yupo well connected na watu. Nyerere akamuuliza Mzee Tabu Mangala, akamwambia kashauriwa ataifishe maduka yote, mpaka ya chini kabisa Uswahilini. Je, Mzee Tabu Mangala anaonaje suala hilo?
Mzee Tabu Mangala anajua maisha halisi ya watu mtaani yalivyo. Akamwambia Nyerere Baba chonde chonde usifanye hivyo. Sisi wenyewe Uswahilini tunajua tunavyoishi. Hao wasomi wako hawajui maisha ya Uswahilini. Tuachieni haya maduka yetu ya Uswahilini tuyaendeshe wenyewe, msiyataifishe.
Nyerere katika busara zake, akauchukua ushauri wa Mzee Tabu Mangala. Akaachana na ushauri wa wataalamu wake wa uchumi.
What is the lesson here? Wasomi hawana monopoly ya ujuzi wa mambo. In fact kuna sehemu zinahitaji watu wasio wasomi sana wenye real world knowledge na common sense ku challenge na ku balance maoni ya wasomi. Kuna sehemu usomi unakupa blind spot na arrogance tu ya kujiona unajua vitu usivyovijua. Nyerere alijua hili, ndiyo maana hakutegemea wasomi tu, ali balance na kuchuja mambo mpaka kuomba ushauri kwa wazee wa Dar tu ambao hawakuwa wasomi.
Mfano mwingine, kuna habari nchi moja ya Africa ilikuwa na vijiji vina tatizo la maji. Wakaja watu wa NGOs za nje wasomi wazungu wakaliona tatizo. Wakataka kulimaliza. Wakachimba visima. Tatizo la maji likaisha. Walitegemea furaha sana, wakashangaa watu, hususan wanawake, hawana furaha baada ya kuletewa maji.
Wakaja kugundua kuwa vile vijiji vina tatizo la wanaume kuwa too controling. Wanawake hawana nafasi ya kuhema. Muda pekee wanawake waliokuwa na nafasi ya kuhema na kufanya mambo yao ni muda wa kwenda kuchota maji. Kwa hivyo wale watu wa nje ku solve tatizo la maji, walikuwa wameathiri uhuru wa wanawake.
Mfano mwingine ni balozi wa Marekani Tanzania alivyokwenda visiwa vya pembeni huko Pemba. Balozi alipenda sana mandhari ya visiwa vile. Akawa anataka kufanya jambo la maana sana la msaada. Akawauliza wananchi, hapa likijengwa daraja la kuunganisha kisiwa hiki kidogo na cha Pemba, litasaidia sana maendeleo? Yeye kwa usomi wake na uzoefu wa dunia yake, aliona kuwa daraja ni kitu muhimu sana pale. Wale wananchi wakamwambia chonde chonde baba usijenge daraja hapa. Huku kwetu serikali inaonea watu sana, polisi wanapiga watu sana, na sisi salama yetu ni kuwa tupo kisiwani huku hawafiki. Ukiwajengea daraja tu watakuja kutumaliza.
Ukiangalia mifano hii, kuanzia Nyerere na maduka, mpaka visima na wanawake na hatimaye daraja la visiwa vya huko Pemba, utaona kuna mtazamo fulani wa kisomi ambao uko disconnected na reality ya watu. Mtazamo huu unahitaji kuwa balanced na habari kutoka kwa watu wa kawaida.
Ukiendekeza usomi, hususan huu wetu wa makaratasi, unatengeneza inbreeding problem. System inakuwa haina input tofauti ya mambo waliyokaririshwa watu. Unatengeneza mfumo ambao hauna perspectives nyingi na kwa hiyo mfumo ambao ni rahisi ku fail.