Powell Gonzalez
JF-Expert Member
- Jun 28, 2023
- 843
- 1,630
Habari za Kazi Wana JF, niende Moja Kwa Moja kwenye mada.
Vijana wengi hatufahamu kabisa umuhimu WA kuinvest katika umri mdogo, miaka 20+/- ndio wakati sahihi wa Kuanza kufanya uwekezaji.
Hii ni Kwa kwa sababu zifuatazo;
1. Ni vizuri kupata uzoefu WA kutosha katika uwekezaji, hivyo ni vyema uanze kuwekeza katika umri mdogo ili kupata ujuzi na uzoefu WA kutosha.
2. Kupata nafasi nzuri ya kukuza mtaji.
3. Katika kipindi hiki ndio kipindi cha kutake risk as much as you can.
4. Inakupa MDA WA kutosha wa kijana kukuza mtaji wake na kufikia malengo ya kifedha.
Mimi nawashauri vijana wenzangu kujifunza zaidi kuhusu maswala ya uwekezaji katika huu umri mdogo Kwa faida za hapo baadae.
Siku Moja nilimsikia Jeff Bezos anasema Moja Kati ya vitu anavyovijutia ni kutokuwekeza mapema hasa katika kipindi cha miaka ishirini.Sifa ya Mtu mwekezaji ni kuwa anaithamini kesho yake, ndio maana anakubali kurisk milioni kadhaa Kwa kuwa anaamini baada ya Mda fulani thamani yake itaongezeka kuliko kama akiitumia au kuweka akiba.
Unaweza kusoma vitabu vya uwekezaji ili kukuza uelewa wako wa haya maswala au ukawasiliana watu wenye utaalam huu (hata Mimi bado ni beginner).
Kwa Kuanza unaweza kuwekeza katika;
1. Stock market(masoko ya hisa)
2. Bonds
3. Fixed deposits(Amanda za kudumu)
4. Real estate investment ( kuwekeza katika Mali zisizohamishika)
5. Exchange traded fund
Cha msingi NI kupata uelewa juu ya Aina ya uwekezaji,risk zake na kiwango chako cha kifedha.
Nimeanzisha hii, naamini wataalamu watakuja kutema madin, karibuni Sana wakuu Mimi bado Sana ndio Kwanza first year bachelor of business, hahah Ila najua humu kuna watu wanaojua karibuni Sana mshushe madini!
Raphael kalolo
student at CBE, bachelor degree in business administration
email; raphaelmathewkalolo@gmail.com
watsapp:0756401790
Instagram;View attachment 2680554raphaelkalolo23