GE2025 Je, Vijana wanahudhuria kampeni kwa sera kweli, au ni kwa zawadi na burudani?

GE2025 Je, Vijana wanahudhuria kampeni kwa sera kweli, au ni kwa zawadi na burudani?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Nimefuatilia mikutano kadhaa ya kampeni na nimeona kundi kubwa la vijana wakishiriki kikamilifu kuwasikiliza wagombea. Uwepo wao unaibua mjadala mkubwa kuhusu nafasi ya vijana katika siasa na mchango wao katika mustakabali wa taifa.

Vijana ndio nguvu kazi ya taifa, hivyo kushiriki kwao katika siasa ni jambo la msingi.

Hata hivyo, swali linaloulizwa ni hili: Je, vijana wanahudhuria mikutano ya kampeni kwa sababu ya sera zinazotolewa na wagombea, au kwa sababu ya zawadi na burudani zinazotolewa? Mara nyingi tumeshuhudia muziki, burudani, na ahadi za muda mfupi zikitumika kuwavutia vijana, jambo ambalo linaweza kuathiri umakini wao katika kuchambua sera zinazogusa maisha yao ya kila siku.
 
Write your reply...yanga bingwa tanzania haina ugumu wa maisha ukiamua hata kuuza maji kuni vibarua udalali unapata hela
 
Kuhudhuria sio tatizo mana ht chadema wanafuatilia kinachofanywa na ccm, tatizo ni kupiga kura kwa watu wasio sahihi
 
Back
Top Bottom