Je, vitendo vya kutekana na baadhi ya Wahanga kuuawa ni mkakati wa CCM kutaka kuua upinzani nchini ili usiwepo kabisa?

Je, vitendo vya kutekana na baadhi ya Wahanga kuuawa ni mkakati wa CCM kutaka kuua upinzani nchini ili usiwepo kabisa?

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,843
Reaction score
31,057
Kwa mujibu wa Katiba ya nchi hii, uwepo wa vyama vya kisiasa hapa nchini ni halali na vinapaswa kuendelea kulelewa Ili vikue, Kwa lengo la kutaka kuendelea kuleta maendeleo nchini.

Uwepo wa vyama vya upinzani nchini ni muhimu sana Kwa kuwa serikali inabidi ipokee mawazo mbadala Kwa lengo la kujisahihisha Kwa lengo la kutaka kuleta maendekeo ya nchi yetu. Hiyo ndiyo tafsiri ya neno Demokrasia.

Kwa namna ya mambo yanavyoendelea hapa nchini, inaelekea kuwa uwepo wa vyama vya upinzani nchini na wale wote wanaojiunga navyo inaonekana kama maadui na wanafanyiwa kila aina ya hila, Ili vifutike kabisa katika ardhi ya nchi yetu!

Hivi vitendo la watu kutekwa na baadhi ya hao wahanga kukutwa wameuawa, nadhani ni Moja ya mikakati ya serikali hii ya CCM, Kwa lengo la kutaka kuwaogopesha raia wa nchi hii, Ili waone kuwa kujiunga na vyama vya upinzani hapa nchini ni kuhatarisha maisha yao

Hivi tujiulize ni kwanini wanaotekwa wote, hakuna wa kutoka Kwenye CCM Wala kutoka Kwenye vyama vidogo vya upinzani, bali ni kutoka Kwenye chama kikuu Cha upinzani nchini Cha CHADEMA pekee??😳

Ipo mifano hai ya karibuni inayoweza kuthibitisha haya madai yangu.

Kitendo Cha kutekwa mchana kweupe Kwa kiongozi wa CHADEMA, Ali Kibao na baadaye mwili wake kukutwa ameuawa huko Ununio na baada ya hapo kujitokeza Rais wa nchi kusema kuwa hicho kitendro ni kibaya mno na anataka uchunguzi wa haraka sana kutoka Jeshi la Polisi na wamletee taarifa ya kina Ili wajulikane ni kina nani waliofanya unyama huo.

Viongozi wa CHADEMA, akina Soka na wenzake wametekwa zaidi ya mwezi mmoja hivi sasa, wananchi hatuelezwi upelelezi unavyoendekea

Hivi sasa ni mwezi mmoja kamili, wananchi wa nchi hii hawajaelezwa maendeleo ya uchunguzi wa kifo Cha Ali Kibao na kutekwa Kwa akina Soka unavyoendelea na umefikia wapi.

Inaelekea kuwa chama Cha CCM na serikali yake wanatumia mkakati wa kuwaogopesha wananchi Ili wasiweze kujiunga na vyama vya upinzani hapa nchini, hususani wasijiunge na CHADEMA

Kumetolewa wito na Chama Cha siasa Cha CHADEMA, balozi mbalimbali za nje ya nchi za nje na wanaharakati mbalimbali, kuwa iundwe Tume huru ya uchunguzi, Kwa kuwa hao wanaotaka Tume huru iundwe, hawana Imani na Tume ya kuchunguza kutoka vyombo vya usalama vya hapa nchini, Kwa kuwa wao vyombo vya usalama hapa nchini ni miongoni ya watuhumiwa wakuu wa uovu unaotokea hapa nchini hivi sasa

Lakini inaelekea wito huo wa kuunda Tume huru ya uchunguzi, unaelekea kuwa umepuuzwa na serikali hii ya CCM.

Kutokana na hali inavyoendelea hapa nchini, inaelekea kuwa chama Cha CCM na serikali yake, vinafanya Kila juhudi kutaka kuuwa mfumo wa vyama vingi nchini, ambao upo kihalali Kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu na badala yake wanataka urejee mfumo wa chama kimoja uliokuwepo hapo awali
 
Nimekuwa nikijiuliza, hivi vitendo vya kutekana na hao baadhi ya watu kutoonekana tena, je ni mkakati wa serikali hii kutaka kuwaogopesha raia Ili wasiweze kujiunga na vyama vya upinzani nchini??
Wenyewe kwa wenyewe pia hawaaminiani.
Hata mpina wanamtafuta usiku na mchana
Hata hivyo, upande WA pili mkikutana nao ni kuwamalizi.. mbali.
 
Wenyewe wanakuja na majibu mapesi kua watu wanajiteka mbona hatuoni watu wao au watoto wao wakitekwa au watekaji wanawachagua CDM mana ndio targeted kwa upinzani inasikitisha haiwezekani tukajenga Taifa kwa wote kusifia tu muda wote
 
Wenyewe kwa wenyewe pia hawaaminiani.
Hata mpina wanamtafuta usiku na mchana
Hata hivyo, upande WA pili mkikutana nao ni kuwamalizi.. mbali.
Ndo ccmu azuie maandamano ya kukosoa utekaj na mauaji?
 
Kwa mujibu wa Katiba ya nchi hii, uwepo wa vyama vya kisiasa hapa nchini ni halali na vinapaswa kuendelea kulelewa Ili vikue, Kwa lengo la kutaka kuendelea kuleta maendeleo nchini.

Kutokana na hali inavyoendelea hapa nchini, inaelekea kuwa chama Cha CCM na serikali yake, vinafanya Kila juhudi kutaka kuuwa mfumo wa vyama vingi nchini, ambao upo kihalali Kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu na badala yake wanataka urejee mfumo wa chama kimoja uliokuwepo hapo awali
CCM, ACT Wazalendo, cuf na vyama vingine uchwara, wao hawatekwi, hawauawi, hawateswi, wala hawapotezwi na kuokotwa kwenye maporini ya Mabwepande, AMA Ununio
 
Wenyewe wanakuja na majibu mapesi kua watu wanajiteka mbona hatuoni watu wao au watoto wao wakitekwa au watekaji wanawachagua CDM mana ndio targeted kwa upinzani inasikitisha haiwezekani tukajenga Taifa kwa wote kusifia tu muda wote
Hizo hoja wanazotoa hao maccm, naweza kuziita kuwa ni walioishiwa na hoja

Hivi kama kweli sisi wapinzani ndiyo tunaofanya huo utekaji, ni kwanini basi hata huo wito tunaotoa wapinzani wa uundwaji wa Tume huru ya kijaji unaotolewa na vyama vya upinzani, nao unapingwa kutekelezwa na serikali hii ya CCM??

Si tungejulikana kuwa sisi wapinzani ndiyo tunaotekana baada ya kukamilishwa Kwa uchunguzi huo huru wa Tume ya kijaji??
 
Hizo hoja wanazotoa hao maccm, naweza kuziita kuwa ni walioishiwa na hoja

Hivi kama kweli sisi wapinzani ndiyo tunaofanya huo utekaji, ni kwanini basi hata huo wito tunaotoa wapinzani wa uundwaji wa Tume huru ya kijaji unaotolewa na vyama vya upinzani, nao unapingwa kutekelezwa na serikali hii ya CCM??

Si tungejulikana kuwa sisi wapinzani ndiyo tunaotekana baada ya kukamilishwa Kwa uchunguzi huo??
Ni muendelezo wa roho mbaya tu hivi kijana kama Soka anakuaje threat kama sio kumkomoa tu? Watu wanaamua kujichafua kwa makusudi kwa kudhani wanamsaidia boss kumbe wanamuwekea wakati mgumu allow people to speak umma ndio utachagua
 
Hata Mimi nimekuwa nikijiuliza hivi Kwa mfano huyo Soka, amekuwa tishio Kwa kiasi Gani, Hadi ifikie System, iamue kumteka na asijulikane alipo Hadi hivi sasa??
 
Tunakaribia kufikia siasa za Venezuela kwa Maduro

kumi na tano tena kwa ccm
 
Kwa mujibu wa Katiba ya nchi hii, uwepo wa vyama vya kisiasa hapa nchini ni halali na vinapaswa kuendelea kulelewa Ili vikue, Kwa lengo la kutaka kuendelea kuleta maendeleo nchini.
Haya hutokea popote duniani penye himaya inayoelekea mwisho... Hali ni mbaya zaidi huko tuendako
 
Haya hutokea popote duniani penye himaya inayoelekea mwisho... Hali ni mbaya zaidi huko tuendako
Bila kuendelea kuweka "pressure" kubwa kwa watawala, ambao wanaamini wanalindwa na vyombo vya Dola, hakika watatumaliza😳
 
Back
Top Bottom