kipara kipya
JF-Expert Member
- May 2, 2016
- 18,833
- 23,276
ndio vizuri!Mawazo mgando!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
ndio vizuri!Mawazo mgando!
Badilika kipara jipya,upambe Huwa sio mzuri,ulimponza Yuda!ndio vizuri!
Endelea kuja tu kata kushoto!Badilika kipara jipya,upambe Huwa sio mzuri,ulimponza Yuda!
HUO NI MKAKATI WA RAIA FEKI WALIO JIMILIKISHA TANGANYIKA CHINI YA KIBARAKA WAO BUSHIRI SAMIAKwa mujibu wa Katiba ya nchi hii, uwepo wa vyama vya kisiasa hapa nchini ni halali na vinapaswa kuendelea kulelewa Ili vikue, Kwa lengo la kutaka kuendelea kuleta maendeleo nchini.
Uwepo Kwa vyama vya upinzani nchini ni muhimu sana Kwa kuwa serikali inabidi ipokee mawazo mbadala Kwa lengo la kujisahihisha Kwa lengo la kutaka kuleta maendekeo ya nchi yetu.
Kwa namna ya mambo yanavyoendelea hapa nchini, inaelekea kuwa uwepo wa vyama vya upinzani nchini, inaonekana kama maadui na wanafanyiwa kila aina ya hila, Ili vifutike kabisa katika ardhi ya nchi yetu!
Hivi vitendo la watu kutekwa na baadhi ya hao wahanga kukutwa wameuawa, nadhani ni Moja ya mikakati ya serikali hii ya CCM, Kwa lengo la kutaka kuwaogopesha raia wa nchi hii, Ili waone kuwa kujiunga na vyama vya upinzani hapa nchini ni kuhatarisha maisha yao
Hivi tujiulize ni kwanini wanaotekwa wote, hakuna wa kutoka Kwenye CCM Wala kutoka Kwenye vyama vidogo vya upinzani, bali ni kutoka Kwenye chama kikuu Cha upinzani nchini Cha CHADEMA pekee??😳
Ipo mifano hai ya karibuni inayoweza kuthibitisha haya madai yangu.
Kitendo Cha kutekwa mchana kweupe Kwa kiongozi wa CHADEMA, Ali Kibao na baadaye mwili wake kukutwa ameuawa huko Ununio na baada ya hapo kujitokeza Rais wa nchi kusema kuwa hicho kitendro ni kibaya mno na anataka uchunguzi wa haraka sana kutoka Jeshi la Polisi na wamletee taarifa ya kina Ili wajulikane ni kina nani waliofanya unyama huo.
Viongozi wa CHADEMA, akina Soka na wenzake wametekwa zaidi ya mwezi mmoja hivi sasa, wananchi hatuelezwi upelelezi unavyoendekea
Hivi sasa ni mwezi mmoja kamili, wananchi wa nchi hii hawajaelezwa maendeleo ya uchunguzi wa kifo Cha Ali Kibao na kutekwa Kwa akina Soka unavyoendelea na umefikia wapi.
Inaelekea kuwa chama Cha CCM na serikali yake wanatumia mkakati wa kuwaogopesha wananchi Ili wasiweze kujiunga na vyama vya upinzani hapa nchini, hususani wasijiunge na CHADEMA
Kumetolewa wito na Chama Cha siasa Cha CHADEMA, balozi mbalimbali za nje ya nchi za nje na wanaharakati mbalimbali, kuwa iundwe Tume huru ya uchunguzi, Kwa kuwa hao wanaotaka Tume huru iundwe, hawana Imani na Tume ya kuchunguza kutoka vyombo vya usalama vya hapa nchini, Kwa kuwa wao vyombo vya usalama hapa nchini ni miongoni ya watuhumiwa wakuu wa uovu unaotokea hapa nchini hivi sasa
Lakini inaelekea wito huo wa kuunda Tume huru ya uchunguzi, unaelekea kuwa umepuuzwa na serikali hii ya CCM.
Kutokana na hali inavyoendelea hapa nchini, inaelekea kuwa chama Cha CCM na serikali yake, vinafanya Kila juhudi kutaka kuuwa mfumo wa vyama vingi nchini, ambao upo kihalali Kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu na badala yake wanataka urejee mfumo wa chama kimoja uliokuwepo hapo awali
Mbeleezi tembea!Endelea kuja tu kata kushoto!
Mimi namtetea mbowe tu dhidi ya wasaliti wengi wanaojifanya wana uchungu na chadema ila sitetei mtu mwingine au kikundi!Wewe kipara kipya, hao unaowatetea wao wanakula Kwa urefu wa kamba zao, wewe wanakuachia manyoya tuu😳