Waafrica hatujawahi kuwa proud of who we are!! They planted something in our heads! This starts from when they colonized us! Wakaondoka, thanks kwa juhudi za wazee wetu, kwa kutukomboa... Whites walikuwa wajanja kwa kutuachia minds za kutawaliwa, bado tumekubali kuruhusu akili zetu kutofikiri kama sisi.
Kwani ni kitu gani kinachotushinda kuboresha hali ya wananchi wetu!!! Mathalani angalia suala la afya, watawala wetu, waliojaa minds za kikoloni, hawataki kuimarisha hospitali zetu, at the same time wanajiwekea policy ya kujitibu nje wakiugua... Watawala wetu tena kwa makusudi, hawataki kuimarisha elimu katika shule zetu, wao kwa kuwa wana nafasi ya wizi wa mali ya wote, wanawapeleka watoto wao nje, kwa shule za whites, kwa kuwa wanaamini hakuna kilicho bora zaidi ya vya nje, cha kushangaza kabisa, shule na vyuo hivyo vya nje vimejaa walimu wa-afrika!!
Watawala wetu wanatuibia mali ya umma kwa ufisadi, badala ya kuwekeza hapa ndani, wanakimbiza nje, kwenye visiwa..(mnavijua wenyewe...) Whites wanafanyia biashara hela zao walizotuibia, wao wankwenda huko mara mbili kwa mwaka kuchukua faida na kununua ngua wanarudi na nyimbo nzuri nzuri tu!!
Wakati haya yanaendelea, hali ya wananchi wa africa inazidi kuwa mbaya, na kwa kuwa watawala wetu hawajali kamwe hali yetu, ndipo juhudi binafsi zinapokuja, watu wanapanda miboti kuvuka kukimbilia ulaya, akina dada zetu wanakwenda huko njee kujiuza, ndugu zetu wanakimbilia huko nje kufanya misheni town kujipatia angalau za kula!! kwa kuwa mifumo ya wenzetu imenyooka na hakuna ubabaishaji, ndugu zetu hawa wanajikuta katika halia ngumu yamaisha, wengine wanakimbilia kujilipua ili wapate haki za raia wa huko, wengine wanaanza kuwa transporters wa biashara haramu, ali-muradi tu maisha yaende! Pilikapilika zinapokuwa ngumu zaidi, wengine wanajiingiza kwenye utapeli, na wizi mdogo mdogo, mwisho wa siku wenye nchi zao wanagundua majanga kutokana na uwepo wetu!!
Basi jamani, kama kweli hatuyahitaji amnyanyaso haya, turudi nyumbani kuunganisha nguvu zetu na kumuondoa mkoloni mambo leo, tujiwekee utaratibu mzuri wa kuishi na kuboresha maisha yetu hapa hapa nyumbani kuepuka laana za weupe hao!!