Hakika kinachoendelea Syria kinatisha, Waarabu wameendelea kutokujua adui yao namba moja ni nani! Ili washughulike nae bado hawajajiuliza vyema na kujibu swali hili ipaswavyo. Je ni Iran, je ni Urusi! Je ni misimamo Yao ya kidini au ni Marekani na washirika wao ikiwemo Israel?
Ni ajabu Waarabu wamekuwa wakipigania kitu ambacho hakijawahi kuwa ni jambo safi kwao! Kinawaangamiza na kuwatafuna. swala la demokrasia ya Kimagharibi ! Demokrasia inayowataka wao kuwa wapiga kelele bila kushughulikiwa na watawala, demokrasia inayowafanya wavae kama wamagharibi, waoane wa kiume na kiume na wa kike aolewe na wa kike mwenzake. Haya yote si jadi yao, wao ni wafuasi wa Uislam na ajabu zaidi Uislam hautaki na hautoi uhuru huo wa kidemokrasia ya kimagharibi wautakao.
Kama ni uongo nitajie nchi moja tu ya kiarabu inayofuata mrengo wa demokrasia ya kweli ya kimagharibi na Haina makelele.
Ajabu ni kwamba katika upiganiaji huu wa uhuru mpya wa kidemokrasia wanashindwa kupigana wakiwa neutral. Imekua ni lazima wajifungamanishe vilivyo, na dini hiyo ya Kiislam. Hapa utaona makundi mbalimbali yenye silaha kama FSA wakipigana dhidi jeshi la Syria, utaona pia ISIS, Al Qaeda, nk.
Wengi wa makundi haya hufadhiliwa na US, Israel, Ufaransa, Uingereza , Turkey ,Qatar, Saudia nk. Makundi yote haya wana silaha nzito lengo lao ni kuziondoa serikali zao za kiimla utaona Kule Libya na Egypt lakini wanapoingia madarakani hakuna wanachobadilisha. Hali za kiuchumi huwa ni mbaya zaidi, hali za kibinadamu mbaya zaidi, watu huchinjwa kama kuku.
Waarabu hawana malengo ya pamoja ya kuunganisha jamii zao zenye dini tofauti na misimamo tofauti kujenga nchi zao ziwe bora zaidi kijeshi, kiuchumi, na kijamii. Wanajisahau hata Wamarekani kuna jamii mamia zenye dini, mirengo, na itikadi tofauti lakini linapokuja swala la utaifa na utambulisho wao si dini wala U -democratic au U- Republic huyumbisha Imani ya kuijenga Marekani iliyo na nguvu zaidi kijeshi, kisasa na kiuchumi kuliko yeyote duniani.
Je ni kweli Waarabu hawajui adui yao namba moja, Waarabu wa Leo ni walaini laini. Hawana nguvu ! Wao Kila kitu kisemwacho na US ni ndio. Hebu ona hili. Kwani unafikiri Kuwait, SaudiArabia, na Qatar ni nchi ambazo Marekani inazipenda sana kwasababu wanafuata demokrasia ya Kimagharibi? Jibu ni Hapana yenye Herufi kubwa. Yes Hapana.
Wamarekani wameshawafunga Kwa kuhakikisha hawataenda kinyume na maslahi yao. Ndio maana hapo Saudia watu huchinjwa vibaya Kwa makosa ya uzinifu na pengine hisia za upinzani dhidi ya ufame huo!
Lakini je uliwahi kusikia Wamagharibi wakipiga kelele kubwa na nzito juu ya uvunjifu mkubwa wa amani ufanywao na taifa hili?
Syria juzi Kwa msaada mkubwa wa Silaha na Intelijensia kutoka Marekani ,wamemuondoa kiongozi wao aliyeongoza kwa muda mrefu kabisa miaka ishirini na nne,wanasahau kwamba Marekani anaupinga utawala wa Syria wa miaka 53 lakini Mmarekani huyohuyo anaushabikia kuukumbatia na kuuenzi utawala wa kimabavu wa Qatar, Kuwait, Oman na UAE wa miaka nenda rudi.
Je halitoshi kuwa fundisho Kwa Waarabu wengine wote kwamba kuwa against US ni sumu kuu ? Kwamba ukiamua hivyo kuwa tayari Kwa uasi, vita na vikwazo?
Je halitoshi hili kuwa ni fundisho waungane zaidi kujenga zaidi mataifa yao?
Baada ya serikali ya Syria kuanguka Israel iliamua kuingia Syria kama sehemu ya uwanja wa bibi. Syria imesambaratika , Syria Haina jeshi tena, silaha zote maelfu za former Syrian Army zinashambuliwa kuangamizwa ziishe kabisa. Kwa wenye akili taifa kama Syria kuongozwa na Wanamgambo ni fedheha. Fedheha kuu isiyomithilika.
Je hili halitoshi kuwa fundisho kwao kwamba adui yao hakuwa Assad?
Ni huzuni kubwa Leo Syria taifa kubwa la kihistoria dahari Kwa dahari haina jeshi la ulinzi. Ajabu ni kwamba Kwa kujua au kutokujua Waarabu wanashangilia.
Poleni sana Waarabu!
Karibuni sana.
Mwisho.