Je, Wabunge Wasaliti 19 watang'olewa Bungeni?

Je, Wabunge Wasaliti 19 watang'olewa Bungeni?

Je wakiondolewa!?wengine watateuliwa upya!?

Yaani Rais atateua wengine!?
Sifahamu kitakachojiri lakini Rais si mteuzi wa wabunge wa viti maalum , kwa vile sheria za Tanzania haziruhusu jambo hilo , viti maalum huteuliwa na vyama husika , huu ndio msingi wa mgogoro wa Halima Mdee na wenzake , Hawa waliteuliwa na Mahera na kuapishwa na Ndugai
 
How wapeleke wakati chadema hawatambui uchaguzi? Kwanza watambue uchaguzi ulikuwa huru na haki then ndio wafanye hayo mambo
Mtego huo, watatumia hoja gani kuukubali huo uchaguzi au ndio sehemu ya maridhiano?
 
Mzaha mkubwa sana! Bad joke, so to speak! Sidhani kama unaamini kwa dhati kwamba, kwa hali iliyokuwepo na iliyopo hata sasa, Chadema ilistahili kuhangaika na kosa la jinai la kughushi nyaraka za mchakato wa viti maalum vya ubunge. Chadema hii ambayo mwenyekiti wake alitengenezewa kesi ya ugaidi na mahakama ikatumika kubariki ushahidi wa kutengenezwa mbele ya macho ya raia na dunia nzima? Hivi jukumu la kufungua mashtaka kwenye kosa la jinai linalopelekea uvunjaji wa katiba ya nchi ni la chama cha siasa? Siyo DPP? Binafsi nimekuwa nikiamini kuwa bila mitandao ya kijamii kuaninika mwenendo wa shauri hilo in real time, na bila mabebaru kufuatilia kwa karibu, watuhumiwa wale wangepatikana na hatia! Mungu atujalie siku moja tukapata muda wa kuyarejea mambo haya kwa utulivu, ukweli na uwazi.
Mkuu nakushukuru sana kwa ufafanuzi wako kwa P. Mayala.
 
Ukiwatoa hao na Siri zote za uchaguzi zitatoka sio kazi rahisi like the way unafikiria
Mara zote Shetani akishamtumikisha mtu humbwaga , halafu ni siri zipi walizonazo hawa ambazo hatuzijui ? mbona kila kitu kiko wazi !
 
Iv km wakifukuzwa ela zawalipa kodi watalipa nazo au ndo itakuwa imeisha iyo???
 
Nihivi huwezi kuruhusu shughuli za kisiasa zianze na msamiati wake pendwa wa maridhiano wakati bado kuna wanasiasa haramu ndani ya bunge letu

Ikiwa msingi wa maridhiano ni kutengeneza uhuru haki na usawa basi hata wabunge haramu hawapaswi kuendelea kura kodi zetu kanakwamba nikodi zisizo kuwa na mwenyewe
 
Mbona ruzuku mnachukua? Kama hao wabunge hamuwatambui mbona ruzuku zinazotokana na wao mnachukua

Chadema mnajikutaga kama watu ambao mnaweza kusimamisha inchi hivi

Makelele mengi kwenye keyboard, ground hakuna kitu

Si mnaanza mikutano ngoja uone kama watu watakuja kuwasikiliza
 
Kwamba CDM rasmi inamtambua sa100 baada ya maridhiano!!

Hapo sasa COVID wataondoka automatically. Bt b4 that zilikuwa kelele tu, wasingeondoka Hadi 2025.
Kwa vyovyote vile, tumeona mambo ya ajabu ajabu sana miaka hii ya karibuni. Hopefully huko mbele hayatajirudia!
 
Kuna Dokezo kwamba Wabunge wale 19 Wasaliti, waliojiuza na kuapishwa na Job Ndugai kwenye eneo la Gereji ya Bunge, huenda Wakaondolewa Bungeni kwa vile waliingizwa kinyume cha Sheria, inadaiwa kwamba hawana tofauti na lile zuio la mikutano ya hadhara lililoondolewa hivi karibuni .

Taarifa zaidi zinasema kwamba Jambo hili la kuondolewa bungeni kwa Halima Mdee , Sophia Mwakagenda na wenzao NI SEHEMU YA MARIDHIANO baina ya CCM na CHADEMA, na kwamba utekelezaji wake waweza kuwa ndani ya siku chache zijazo.

Uwezekano wa Wasaliti hawa kufukuzwa Bungeni ni zaidi ya 100% , Hii ni kwa sababu waliingia kwa kufoji , hata ile KESI YAO WALIYOFUNGUA MAHAKAMANI inapinga kuvuliwa Uanachama wao tu , HAIHUSIANI NA UBUNGE , hivyo basi wakivuliwa ubunge bado wanayo nafasi ya kuendelea na kesi yao , na ikiwa watashinda basi watarejeshewa uanachama wao (japo uwezekano wa kushinda ni kama hakuna).

Usaliti ni laana, Kwa Mujibu wa Maandiko Matakatifu, Laana ya Usaliti yaweza kukikumba hadi kizazi cha nne cha Mhusika .

INASIKITISHA SANA!
Hao ni kibora ya CCM
 
Mkuu si utafute jambo jingine kwa maana hili kwanza liko mahakamani; pili hamna namna ya kuwatoa zaidi ya kulilia huruma za watu wengine ndiyo wawatoe; hawa 19 mpaka 2025 take my word
Tatizo sio tu Covid-19 waliokiuka taratibu za kuwateua/kubariki teuzi za wabunge hao,bali kuna vigogo wa Chadema wapo waliosaidia kuwapeleka bungeni,lakini mambo yalipobainika wakaingia mitini.
 
Tatizo sio tu Covid-19 waliokiuka taratibu za kuwateua/kubariki teuzi za wabunge hao,bali kuna vigogo wa Chadema wapo waliosaidia kuwapeleka bungeni,lakini mambo yalipobainika wakaingia mitini.
Kama kuna covid yeyote alikubali kupelekwa na kigogo wa chadema bungeni basi atakuwa fala sana ! Katiba ya Chadema hairuhusu jambo hilo na Halima Mdee akiwa kiongozi wa juu wa Chadema , alijua utaratibu .

Muapishe Mfungwa aliyetolewa Jela msingizie vigogo wa Chadema ! hata kama Watanzania ni mbumbumbu mzungu wa reli , ndio muwadanganye kibwege namna hii kweli !

Hivi Job Ndugai na Mahera ndio vigogo wa Chadema ?
 
Itabidi uvumilie tu hadi 2025
 
Back
Top Bottom