Pre GE2025 Je, wabunge watakaoshinda kupitia CHADEMA 2025 watagomea mshahara wa Milioni 18 kwa mwezi?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Acha kuwa-judge na kuwapa labels watu kutokana na background zao.

Personal Priscus ashinde au ashindwe uchaguzi wa 2025 sikosi usingizi.

Lakini usiwaondelee watu credibility zao kwa sababu żako.
Mimi nipo kwangu Mtwara, siasa za Mikoa yote nafuatilia na nilicho kwambia ndio amin na kweli.
Endeleeni kupigwa tu hapo, Priscus aliahidi kumalizia ujenzi stendi ya Nganga-mfumini iliyoanza kujengwa na CHADEMA , amefikia wapi? Mabilioni ya fedha yamefia chini na ile ujenzi itabidi kila kitu kivunjwe waanze upya!

Naskia hapo stendi kama unaenda njor ile open space amempa jamaa ake ajenge kituo cha mafuta.

Okay kile ki sambusa[kipande cha ardhi] kama unatoka uhuru hostel kwenda mjini na kwenda KCMC naskia wamempa mmiliki mmoja wa kamuni ya utalii , mwenye asili ya kiasrabu, sijui inaitwa MALI TOURS?ni kweli?

Naskia Pale karibu na FIVE STARS HARDWARE kuna open space zamani kuna kanisa lilianzishwa likavunjwa, kuna mayor aliyefukuzwa amejimilikisha, ni kweli?
 
Majungu at best

Maamuzi ya mkoa, wilaya, baraza la madiwani; unataka kutuamisha mmbunge anaweza yatengua peke yake.

Kwa utaratibu huo wamtoe tu 2025, Iła kipindi alichobakiza anastahili walau unaibu waziri.
 
Majungu at best

Maamuzi ya mkoa, wilaya, baraza la madiwani; mmbunge anaweza amua peke yake.

Kwa utaratibu huo wamtoe, Iła kipindi alichobakiza anastahili walau unaibu waziri.
Pri awe naibu waziri? Mara 500 apewe Kasheku Msukuma!

Unajua kwa miaka yote 4 Bungeni ameuliza swali moja la msingi tena ambalo jibu analo the rest ni kusifia tu?
huyu hata wizara wa wanawake ambayo hainaga kazi hafai kuwa naibu waziri, Level yake hata kwenye kamati za bunge sijui ana mchango gani alafu ni kakijana kamesoma Umbwe na ilboru.
 
nchi wanaichezea kila dansi kwa mwendo huo lazima tukope ili kuendesha serikali ambapo kuja kulipa tutashindwa mwishoe tutauza hadi mlima kilimanjaro kwaajili ya madeni ya kijinga tu
 
nchi wanaichezea kila dansi kwa mwendo huo lazima tukope ili kuendesha serikali ambapo kuja kulipa tutashindwa mwishoe tutauza hadi mlima kilimanjaro kwaajili ya madeni ya kijinga tu
Ina maana unataka mwaka huu tusinunue magoli ya Simba, Azam , JKU na Yanga kwenye mashindano ya CAF?

Kununa magoli ni kuchezea hela?
 
Kwasababu unamwita ‘Pri’ jina ambalo watu wake karibu wanalitumia kwa miaka mingi, as opposed na kutumia jina lake kamili ‘Priscus’ sina sababu ya kuingilia siasa zenu.

Mnajuana nyie kwenye mambo yenu ya siasa wacha niwaachie wenyewe.
 
Ina maana unataka mwaka huu tusinunue magoli ya Simba, Azam , JKU na Yanga kwenye mashindano ya CAF?

Kununa magoli ni kuchezea hela?
kununua magoli
safari zisizo na tija kupeleka watu wasionielewa
ununuaji wa magari mapya ya viongozi
vikao visivyo na maana a posho zisizoeleweka
mishahara mikubwa kwa watu wenye utendaji hafifu
ufujaji wa fesha na rushwa kuzidi
mawaziri kuanzisha mipango au miradi isio weza saidia taifa wanabaki kula hela za kodi au mikopo iliyotoka nje tena yenye masharti ya kijinga ya kutuumiza

haya mambo yanalididimiza sana taifa alafu tunakazana kujitetea tumekopa mikopo nafuu

hebu jiulize tunamlipa mbunge 18m kwa kazi ipi anayofanya..... tunamnunulia mkuu wa wilaya gari jipya lenye thamani ya 300m+ wakati wilaya yake haichangii chochote serikalini zaidi ya kusubiri kupewa pesa za uendeshaji hao watu kwann wanathaminiwa hivyo wakati huduma wanayotoa ni hafifu..

leo unampa mbunge 18m mwalimu unampa 400k Alafu utarajie taifa lenye maendeleo ni kujidanganya mtu mwenye manufaa ya moja kwa moja kwenye jamii hakumbukwi ila wajinga tunaowachagua na wakageuke chawa wa raisi tunawalipa 18m ni ushenzi
 
Chadema ilivyojaa majizi hivyo,yanawaza kupata mishahara ya mamilioni wakat huku yanadanganya watu kuwa hawapendi ufisadi
 
Great job
 
Hoja yako inakosa kabisa mashiko kwa kuhusisha malipo ya juu ya mishahara ya wabunge watarajiwa wa CDM. Kumbuka viwango vya malipo haya yamependekezwa na kupitishwa na wabunge wa sasa wa CCM. Ufinyu wa hoja yako upo katika taswira mbili kubwa. Kwanza, stahiki za mtumishi wa umma ikiwamo mshahara zipo kisheria, hivyo kupokea ama kugomea ni utashi binafsi wa mtumishi mwenyewe, na wala hilo halina mgogoro wowote ule wa kisheria

Pili, ni upofu na ukibogoyo wa hoja yako umejielekeza kwa kuegemea upande wa wabunge watarajiwa wa CDM kana kwamba wa vyama vingine vya upinzani hawahusiki, na pia kwa hata upande wa wabunge wa CCM, unataka kutuaminisha kuwa ni kama vile hii ni stahili isiyostahili kuhojiwa kwa wao kupata mishahara hiyo ya juu. Badala ya kujielekeza na kuuzungumzia kwa uwazi mzigo wa malipo waliojiwekea wabunge wa CCM, wewe unajaribu kukwepa kinafiki kuihusisha CDM katika hili.

Natambua unautambua ukweli wote, na pia unatambua CCM haiwezi kulishughulikia suala hili. Bali unatambua kuwa uwepo wa wabunge wengi na halali wa CDM ndani ya bunge ndiyo pekee wanaweza kulishughulikia jambo hili.
 
Natambua hili ndio maana nataka watoe msimamo wao mapema kabisa.
 
Tusitafute ajira ,tutafute KAZI ambazo zipo Kila Mahali.

Ukifanya KAZI, tengeneza ajira.
 

Honestly, mimi sijakuelewa

Unaposema "watagomea", what exactly do you mean?

Ugomee kupokea mshahara? Wapi duniani umeona hiyo? Watu hugoma ili walipwe mishahara bora zaidi na si kugomea kilichopo..

Sioni kosa la Mh. Freeman Mbowe ku raise hii ishu kwa jamii kwa lengo la ku - build awareness juu ya unequal of pay miongoni mwa makundi ya umma tofauti yanayolipwa mishahara toka ktk mfuko wa serikali.

Kwa kilichopo, uwe unaridhika na kiwango hicho au la, kitalipwa moja kwa moja kwenye Bank Account yako

Ukishalipwa zinakuwa pesa zako.

Baada ya hapo wewe ndiye uamue kuurudisha kwa aliyekupa ale yeye (kwa kuwa ni mkubwa sana) au uutumie kwa namna uonayo wewe. Unaweza kutoa kama sadaka kwa wasiokuwa nacho.

Nadhani ni muhimu waendeleze mapambano haya ya usawa ktk malipo wakiwa bungeni ili wanacholipwa wao kiwe na uwiano sawa na wafanyanyakazi wengine!

Therefore, kwa maoni yangu, hoja yako ina upogo uliotukuka.!

Hoja ya Mh. Freeman Mbowe inalenga kuleta usawazisho (equality) katika malipo ya mishahara kwa makundi yote ktk nchi yanayolipwa mishahara yao kutoka ktk pesa za umma..

Kama ni ukubwa, basi wote tulipane kwa ukubwa huo na kama ni kidogo, wote tulipane kwa udogo huo!

Kwa hiyo sio kosa kwa Mh. Freeman Mbowe kupiga kelele kuonesha utofauti wa malipo kwa kiwango hicho lengo likiwa ni ku - build awareness juu ya ishu hiyo kwa wananchi ili waamue hatua za kuchukua.
 
Msimamo wa wananchi ni kuwa,

Hatukubaliani na Wabunge kujilipa mshahara zaidi ya milioni Tano,

Tunataka tuweke makubaliano na msimamo.

Tunataka mkataba kati yetu na wabunge, mshahara ishuke iwe Chini ya milioni Tano,

Tupate pesa ya kuwapa chakula Cha mchana Bure watoto wa shule zote nchini Kwa hiyo ziada ya mishahara ya wabunge.
 
Msimamo wa wananchi ni kuwa,

Hatukubaliani na Wabunge kujilipa mshahara zaidi ya milioni Tano,

Tunataka tuweke makubaliano na msimamo.

Mh. Freeman Mbowe na wabunge wengine tayari wameshaibua mjadala kwa uelekeo huu.

Kosa lake lipi hapo hata umtake agomee anacholipwa kisheria?

Wewe uliyeanzisha mjadala huu huku benchmark ikiwa ni hoja ya Mh. Freeman Mbowe, umekosea kuingiza swali la "watagomea mshahara huo?" na kwa maana hiyo ukauelekeza mjadala kusiko! Hii ndiyo hoja yangu

Mimi nadhani, wakifika bungeni ili kuonesha kuwa wako committed kuleta mabadiliko kwenye eneo hili, waendelee kuisukuma hoja hii kwa nguvu lengo ni ili kuweza kuleta usawazisho au uwiano wa mishahara ulio sawa miongoni mwa watumishi wa umma kulingana na aina na nature ya kazi/majukumu anayoyafanya mtumishi.
 
Wewe unakubali Utaratibu wa wabunge kupewa mamlaka kikatiba ya kujipangia mishahara?

Kwamba wanaweza kujiongezea bila ushauri wa yeyote yule?

Ruhusa hiyo wanadai tumewapa sisi,

Sasa Nia ya thread hii ni kuwaamsha wananchi tukae na wabunge watarajiwa tuwekeane mkataba kabisa.

Na Kwa kuwa CDM inaaminiwa na wananchi,

Tuanzie na wao, watoe msimamo.

Mbona Rais wa Bukinafaso, Malawi amekataa mishahara mikubwa na marupurupu?

Kusema kwamba huwezi Gomez mshahara uliopo kisheria ni Ujinga mkuu,

Walimu wanagoma kudai waongezewe mshahara ni kiduchu, sasa kwanini wabunge wazalendo wasigome kuwa pesa hiyo ni nyingi sana?

Na kama hawawezi sisi waajiri wao tuchukue hatua.
 
Nimekulewa

Naheshimu mtazamo na maoni yako, anyway.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…