Je wafahamu kuwa baada ya kufa ni hukumu na je wampenda nduguyo?

ladyfurahia

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Posts
14,753
Reaction score
9,575
Mu hali gani wanajf,

Awali ya yote nimeonelea niandike kitu hichi ili kuwaweka katika utayari wa maisha yenu/ yetu, sijamkusudia mtu yeyote kumwandika hapa bali kutokana na hali yangu ninayopitia sasa yani najiona DOUBLEDOUBLE (Naumwa mgongo). sio kwamba nimependa kujiandika ila kuwatadharisha na hali ya dunia inavyokwenda na kukujenga na kukushauri katika mstakabali wa maisha yako. hususani kiroho zaidi kwa yule atakayefahamu nilichoandika hapa.

Hivi unajua kwa Duniani sisi ni wasafiri na hapa si makao yetu kabisa, na je watambua kuwa unapompenda nduguyo au jirani yako unajitengenezea mahali pazuri mbinguni. Huna budi kujichunguza na kujihoji moyoni mwako umejiandaaje kukabaliana na swala hili, ndo tumeanza mwaka ni bora ungeanza mwaka vyema kwa kujichunguza na kujipima. Angalia mwaka 2012 uliamalizaje je ulimaliza kwa mapenzi ya Mungu au kwa mapenzi yako mwenyewe. Je wafahamu kuwa baada ya kufa ni hukumu? na umejua kuwa umewekewa kufa mara moja tu na baada ya kufa ni uzima wa milele. UMEJIANDAAJE? Je yule msanii aliyekufa tarehe 1 hakupenda kuishi alipenda sana ila ndo hivyo tena ilifika siku yake na je Wewe upo mpaka leo mmempa nini Mungu mpaka amekuweka leo. JICHUNGUZE KISHA CHUKUA HATUA YA ZIADA. Hebu soma hapa "Na kama vile watuwalivyowekewa kufa mara moja moja baada ya kufa ni hukumu" Waebrania 9:27
Je wewe Unawapenda ndugu zako au unawachukia na kuwasengenya ama kutokuwajali pindi Mungu anapokufanikisha kimaisha unawajali wale waitaji na masikini au unawapita tu njiani bila hata ya kuwasaidia, je unajitoa kwenda kwa watoto yatima na wasiojiweaza kuwasaidia kutokana na hicho kidogo ulichopata au unawakandia na kuwaona hawafai kitu. JICHUNGUZE MPENDWA NA ANZA SASA KUTENDA MEMA. BADO HUJACHELEWA. Hivi unajua unapowasaidia wasiojiweza unamkopesha Mungu na utapata BARAKA toka kwa Mungu. hebu soma hapa: "Upendano wa ndugu na hudumu msisahau kuwafadhlili wageni maana kwa njia hii wengi wamewakaribisha malaika pasipo kujua Waebrania 13:1-2. Je wewe umekuwa mmojawapo wa kuwapenda na kuwafadhiili wahitaji ANZA SASA NA UTABARIKIWA
 
Ujumbe mzuri,.. Mimi nawapenda wote, sijui ntauonja ufalme wa mbingu!.!
 
Nawapenda wote hata shetani pia nampenda,siachi mtu mie
 
Ninamshukuru mungu nimelishwa neno la mungu nilikua na kiu nalo sana ,ubarikiwe sana
 
ASANTE akenajo nitaendelea kurusha NENO la MUNGU kadri niwezavyo kwani kuna watu wana kiu na njaa ya kujua ufalme wa Mungu, ila endelea na moyo huo utafika mbali kiroho
Niombee mwenzio ninaumwa na niko serious mwili wote umeshambuliwa naitaji maombi yako akenajo
 
Last edited by a moderator:
kama umezamilia kuishi maisha yanayompendeza Mungu Husninyo mbinguni utafika tu kwa imani na utakuwa mrithi pamoja na Yesu katika makao ya milele, wewe endelea na msimamo wa maisha yaliyo matakatifu usimwache Mungu
ladyfurahia ahasante sana kwa kumweleza Husninyo manake ni majuzi tu alitaka kupindua ndoa yangu....sasa atafata uliyomshauri mungu atamjalia mume mwema na watoto wazuri waizunguke na kuipamba nyumba yake... Wakiishi katika kumjua, kumpenda, kumtumikia mungu na hatimaye furaha ya milele mbinguni
 
Last edited by a moderator:
kama umezamilia kuishi maisha yanayompendeza Mungu Husninyo mbinguni utafika tu kwa imani na utakuwa mrithi pamoja na Yesu katika makao ya milele, wewe endelea na msimamo wa maisha yaliyo matakatifu usimwache Mungu

emeeeeeennnn!!! jina la bwana lipewe sifa.
 
Last edited by a moderator:

nimepokea neno la ladyfurahia.. hapa najiona kama nimezaliwa upya. lol! sikupindui tena mdogo wangu ila mwambie watu8 aache uchokozi maana yeye ndio anasababisha. lol
 
Last edited by a moderator:
Afu nakupenda sana Husninyo.
Swali la kwanza lilikuwa nini tena?
 
Last edited by a moderator:
Nimepita magumu na mazito nimezushiwa nimesengenywa na hata wakati mwingine kutaka kuuwawa. Ila nimemwambia Mungu nipe kusamehe nakusahau. Amen
 
Afu nakupenda sana Husninyo.
Swali la kwanza lilikuwa nini tena?

mkwe nnavyokupenda hadi natamani nikulipie dar white party! Lol, swali la kwanza achana nalo halikokotoleki.
 
Last edited by a moderator:
nimepokea neno la ladyfurahia.. hapa najiona kama nimezaliwa upya. lol! sikupindui tena mdogo wangu ila mwambie watu8 aache uchokozi maana yeye ndio anasababisha. lol

Mchokozi kwani mie njiwa dume???
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…