Je wafahamu kuwa baada ya kufa ni hukumu na je wampenda nduguyo?

Je wafahamu kuwa baada ya kufa ni hukumu na je wampenda nduguyo?

Swali hapa ni, kama ungejua kwa hakika kwamba hamna hukumu baada ya kufa, bado ungempenda nduguyo na kujitoa kwa wote?
 
Mu hali gani wanajf,

Awali ya yote nimeonelea niandike kitu hichi ili kuwaweka katika utayari wa maisha yenu/ yetu, sijamkusudia mtu yeyote kumwandika hapa bali kutokana na hali yangu ninayopitia sasa yani najiona DOUBLEDOUBLE (Naumwa mgongo). sio kwamba nimependa kujiandika ila kuwatadharisha na hali ya dunia inavyokwenda na kukujenga na kukushauri katika mstakabali wa maisha yako. hususani kiroho zaidi kwa yule atakayefahamu nilichoandika hapa.

Hivi unajua kwa Duniani sisi ni wasafiri na hapa si makao yetu kabisa, na je watambua kuwa unapompenda nduguyo au jirani yako unajitengenezea mahali pazuri mbinguni. Huna budi kujichunguza na kujihoji moyoni mwako umejiandaaje kukabaliana na swala hili, ndo tumeanza mwaka ni bora ungeanza mwaka vyema kwa kujichunguza na kujipima. Angalia mwaka 2012 uliamalizaje je ulimaliza kwa mapenzi ya Mungu au kwa mapenzi yako mwenyewe. Je wafahamu kuwa baada ya kufa ni hukumu? na umejua kuwa umewekewa kufa mara moja tu na baada ya kufa ni uzima wa milele. UMEJIANDAAJE? Je yule msanii aliyekufa tarehe 1 hakupenda kuishi alipenda sana ila ndo hivyo tena ilifika siku yake na je Wewe upo mpaka leo mmempa nini Mungu mpaka amekuweka leo. JICHUNGUZE KISHA CHUKUA HATUA YA ZIADA. Hebu soma hapa "Na kama vile watuwalivyowekewa kufa mara moja moja baada ya kufa ni hukumu" Waebrania 9:27
Je wewe Unawapenda ndugu zako au unawachukia na kuwasengenya ama kutokuwajali pindi Mungu anapokufanikisha kimaisha unawajali wale waitaji na masikini au unawapita tu njiani bila hata ya kuwasaidia, je unajitoa kwenda kwa watoto yatima na wasiojiweaza kuwasaidia kutokana na hicho kidogo ulichopata au unawakandia na kuwaona hawafai kitu. JICHUNGUZE MPENDWA NA ANZA SASA KUTENDA MEMA. BADO HUJACHELEWA. Hivi unajua unapowasaidia wasiojiweza unamkopesha Mungu na utapata BARAKA toka kwa Mungu. hebu soma hapa: "Upendano wa ndugu na hudumu msisahau kuwafadhlili wageni maana kwa njia hii wengi wamewakaribisha malaika pasipo kujua Waebrania 13:1-2. Je wewe umekuwa mmojawapo wa kuwapenda na kuwafadhiili wahitaji ANZA SASA NA UTABARIKIWA
Be blessed
 
Back
Top Bottom