Je, wafahamu suluhusho la tatizo la kukosa choo?

Je, wafahamu suluhusho la tatizo la kukosa choo?

manushiboy

Member
Joined
Aug 3, 2011
Posts
34
Reaction score
9
Jamani naombeni msaa wenu kuhusu nini cha kufanya maana nina tatizo la kukosa choo kwa muda mrefu inakia kipindi nakaa hadi siku tano sita.

Naombeni utatuzi wa tatizo hili.

Asanteni.
 
jamani naombeni msaa wenu kuhusu nini cha kufanya maana nina tatizo la kukosa choo kwa muda mrefu inakia kipindi nakaa hadi siku tano sita. Naombeni utatuzi wa tatizo hili asanteni

Tatizo la kukosa choo kwa muda mrefu (Constipation)...

UKOSEFU wa choo ni tatizo sugu miongoni mwa watu wengi. Bila kujua kuwa ni tatizo ambalo linahitaji tiba ya haraka, watu wengi hupuuzia na kuona siyo tatizo kubwa na ni hali ya kawaida.

Ukosefu wa choo wa muda mrefu, huwa ndiyo chanzo cha magonjwa mengine hatari.

Mtu anapokosa choo kikubwa kwa siku kadhaa, uchafu hujikusanya tumboni na unapokosa sehemu ya kutokea hukimbilia kwenye damu na kuingia kwenye mfumo mzima wa damu.

Uchafu huo unapoingia kwenye mfumo wa damu huwa sumu na chanzo cha maradhi mengine ambayo hujitokeza baadae na kuanza kumuathiri mtu, bila kujua chanzo chake.

Kwa kawaida mtu unapaswa kupata choo cha uhakika japo mara moja kwa siku, kutegemeana na mlo wake wa kila siku, unapokosa choo kwa siku nzima ili hali una kula milo yote kwa siku, elewa una tatizo katika mfumo wako wa kusaga chakula hivyo unapaswa kuchukua hatua haraka.

MTU MWENYE TATIZO HILI ANA DALILI GANI?

Mtu mwenye tatizo la ukosefu wa choo huwa na dalili kadhaa, ikiwemo kutumia nguvu na muda mwingi wakati wa kujisadia haja kubwa.

Pili ulimi wake huwa na utandu mweupe na hutoa harufu mbaya mdomoni. Mtu huyu pia hukosa hamu ya chakula na wakati wote tumbo huwa limejaa.

NINI HUSABABISHA TATIZO?

Tatizo la ukosefu wa choo husababishwa zaidi na ulaji mbaya wa vyakula, kuacha kula matunda na mboga na staili mbaya ya maisha ikiwa ni pamoja na kutokunywa maji ya kutosha kwa siku.

NINI KIFANYIKE?

Ili kuondoa tatizo kabla halijawa sugu, fanya moja miongoni mwa haya yafuatayo:

Kunywa maji ya uvuguvugu asubuhi mapema, kisha tembea tembea, baada ya muda utasikia haja ya kwenda Choo. Ili usifanye haraka na upate muda wa kutosha kujiandaa kwenda kazini, amka mapema zaidi.

Kula kiasi cha kutosha cha salad ya mboga mboga na juisi ya matunda halisi asubuhi kabla ya kula chochote.

Kila siku kabla ya kwenda kulala, kunywa maji ya uvuguvugu yaliyochanganywa na kijiko kimoja cha asali. Kunywa maji ya uvugu

yaliyochanganywa na limau asubuhi na mapema kabla hujala kitu chochote. Kunywa ‘castor Oil’ muda mfupi kabla ya kwenda kulala.

Ili kujiepusha kabisa na tatizo la ukosefu wa choo, jenga mazoea ya kunywa maji mengi ya uvuguvugu kula mboga na matunda kwa wingi kila siku na

kuacha kabisa ulaji wa vyakula vilivyoondolewa virutubisho kama vile mikate

myeupe, ugali wa unga mweupe, keki vyakula vyenye sukari nyingi na vyakula vingine vitamu.
 
jamani naombeni msaa wenu kuhusu nini cha kufanya maana nina tatizo la kukosa choo kwa muda mrefu inakia kipindi nakaa hadi siku tano sita. Naombeni utatuzi wa tatizo hili asanteni

Usile ugali wa sembe, gonga dona, kunywa juice ya ubuyu kwa sana, maji, kula mapapai pamoja na maembe bila kumenya maganda yake. Usisahau mboga za majani hasa mchicha! Ukiweza hii, umepona!
 
Habar wadau mim mkaz wa dar ninatatizo la kukosa choo limedumu kwa muda mrefu sana na nikipata basi huwa kigum sana nina vidonda vya tumbo pia nisaidien ushaur
 
Hospital si watakuwa wamekushauri?ama unaenda hospital za vichochoroni?
 
Jitahidi kuondoa hizo " konstipisheni " kwa kula mapapai kila mlo katika siku moja lazima utakwenda choo safi kabisaa
 
Hii ndo.siri kubwa na ushauri wa bure.Huta pata ushauri huu hospitali but ndo muarobaini wa tatizo lako.
1:Anza kula ugali wa dona yaani unga wa mahindi yasiyo kobolewa
2:kama utakuwa na uwezo wasi jitahidi angalau mara moja kwa wiki kula mchanganyiko wa mchemsho wa mboga za majani zifuatazo(coliflower,brocoli,kabichi,biringanya isiyomenywa maganda,nyanya chungu,green beans,karoti isiyomenywa maganda,bamia ).Chemsha kwa moto wa wastani kwa dakika zisizo zidi kumi.lazima kibakie na ubichi ubichi.Tatizo lako ni kwamba unakosa fibre katika milo yako ambapo husababishwa na kukoboa nafaka na ukosefu wa matunda na mboga za majani.
Ukishindwa point namba mbili kwa sababu ya kipatobasi point ya kwanza ni muhimu zaidi itamaliza tatizo lako
Fuata ushauri huo upone na kuishi kwa furaha
 
Chukua ukwaju kl1 uloweke kwenye maji kiasi na ukishalowana ukamue na uuchuje! hakikisha juisi yake iwe nzito!
dozi: kunywa glac1 kutwa mara3 kwa cku1 then utaleta feedback!
 
Mwoongezee na matunda mfano Papai japo kipande kwa siku mara moja au kila baada ya siku 1.
 
Kunywa mafuta ya ubuyu, asubuhi sana kabla ya kufungua kinywa na usiku kabla ya kulala ni dawa tosha..
 
Habar wadau mim mkaz wa dar ninatatizo la kukosa choo limedumu kwa muda mrefu sana na nikipata basi huwa kigum sana nina vidonda vya tumbo pia nisaidien ushaur

Maji kwa wingi+Mapapai+Ndizi mbivu=Choo laini cha kutosha
 
ni pm nikuelekeze dawa ila uwe mvumilivu tu na usiwe na ratiba ya kutoka kwa angalau masaa matano na uandae sh 2000 tu
 
Mkuu kunajuis inaitwa splina liqiud niki boko inatibu hadi vidonda vyatumbo
 
Chukua ukwaju kl1 uloweke kwenye maji kiasi na ukishalowana ukamue na uuchuje! hakikisha juisi yake iwe nzito!
dozi: kunywa glac1 kutwa mara3 kwa cku1 then utaleta feedback!

chukua huu ushauri na ufanyie kazi haraka kwa matokeo ya haraka zaidi
 
Back
Top Bottom