Je, wageni wanaruhusiwa kutapeliwa huku Zanzibar?

Ninux

Member
Joined
Oct 9, 2016
Posts
34
Reaction score
10
Hamjambo? Miaka mitatu iliyopita nilinunua kiwanja huku Unguja lakini waliniambia nitumie jina la Zanzibari (hata sheha alisema hivi).

Mimi nilikuwa na wasiwasi kwa hiyo nililazimishwa yule mzanzibari ale kiapo mbele ya mwanasheria na kwa mwandiko Rami, Tajani umesajiliwa. Katika kiapo imeandikwa kwamba hiyo mzanzibari ni msimamizi tu wa mali yangu na kwamba Mimi ni mmiliki wa kiwanja kilicholipa taslimu mbele ya sheha. Baadaye Mimi niligombana na huyo mzanzibari kwa Sababu aliniibia yuro 2000.

Nilikwenda ofisi ya ardhi nikawaonyesha hicho kiapo nikahadithia kila kitu. Bodi ya ardhi wananiambia kwamba nilidanganywa na wote kwa Sababu ingawa Mimi ni mgeni ninaruhusiwa kupata "lease". Baada ya siku chance nilipata "lease", lakini yule mzanzibari alifungua kesi ya madai kwa kusema kwa ndiyo yeye aliyenunua kiwanja. Mahakamani alishindwa kutoa ushahidi wowote. Mimi nilitoa kiapo chake, "lease" na mashahidi wengi. Basi jaji alitoa hukumu ya ajabu!

Alikubali kwamba Mimi nilinunua kiwanja kwa hiyo mmiliki ni Mimi lakini alisema kwamba kwa Sababu bodi ya ardhi walifanya kosa moja katika utaratibu wa kunipa "lease" lazima nimpe yule mzanzibari kiwanja changu! Tena ninaweza kukata rufaa lakini huyo jaji wanachelewesha kunipa rekodi zote za kesi! Je, wanasheria, mnaweza kunieleza mantiki hiyo?
 
Mkuu pole sanaa, huyo ni jaji kweli au hakimu? Kesi ilikua mahakama ya ardhi au baraza la ardhi la uko? Lakini uenda kawa ni hakimu tu mwenye uelewa mdogo wa sheria.

Sijawai sikia hukumu ya kijinga kama hio kabisaa, yaani wewe mahakama ikutambue ndio mwenye kiwanja alafu apewe taapeli tena hahahaha, embu kachukue nakala ya hukumu mahakamani hapo haraka sanaa ukakate rufaa, rufaa ukatwa na mahakama ya juu zaidi yake, kama ulikua mahakama kuu nenda mahakama ya rufaa, usiogope juu ya muda wa rufaa kupita, kesi za ardhi rufaa yakd uenda mpaka miaka 12, usiofu haki ni yako kabisaa.... Na endapo ata kama mahakama ingeonelea wewe kutokua na haki ya kumiliki ardhi uko labda sio raia wao bado ingekupa remedy kama kiwanja icho kichukuliwe na wewe upewe fidia ya thamani halisi ya sasa ya kiwanja icho.
 
Mtafute wakili.

Bara ni pazuri sana, amani tele. Mzanzibari ananunua kiwanja na kujenga. Sasa wewe nenda ukanunue kule! utagundua kumbe neno muungano ni jina tu.
 
Mtafute wakili.

Bara ni pazuri sana, amani tele. Mzanzibari ananunua kiwanja na kujenga. Sasa wewe nenda ukanunue kule! utagundua kumbe neno muungano ni jina tu.
Ukitoa ushari nini cha kufanya inatosha

Usitoe kauli za kujenga chuki. Migogoro ya aridhi ipo kila mahala hata baina ya ndugu kwa ndugu inatokezea.
Mtoa post katiririka wala hakushutumu uzanzibar au ubara

Btw
Kuna wa Bara hapa Zanzibar wamejenga na wanaishi na familia zao hata kurudi kwao hawatamani
 
Danali, sijasema wala kuleta chuki. Hiyo ndiyo hali halisi.

Nakubali migogoro ipo kila sehemu, lakini hapa tunazungumzia kununua ardhi.

Hao wabara walionunua ardhi zenji, hakiki makaratasi yao ya umiliki uone kama hamna mtu wa pili ambaye lazima awe mzanzibari.

Tuuseme ukweli bila kupindisha mambo.
 
Kuna mambo mengine ni ya kujitakia tu ivi sheria ya znz juu ya umiliki ardhi inasemaje? Tuseme hukujua au ulifanya makusudi?
 
Kuna mambo mengine ni ya kujitakia tu ivi sheria ya znz juu ya umiliki ardhi inasemaje? Tuseme hukujua au ulifanya makusudi?
Mudhamil nakushukuru sana kwa kujaribu kunisaidia.
Sheria ya Zanzibar inasema kwamba wageni wanaweza kukodi, yaani kupata "lease", hawawezi kupata hakimiliki. Tatizo langu ni kwamba mimi nimepata "lease" lakini Ingawa mashahidi wote, hata yule wa mtapeli, wameshuhudia kwamba ndiyo Mimi aliyenunua kiwanja, ingawa mtapeli aliandika rasmi mbele ya mwanasheria na watu wengine kwamba yeye alikuwa msimamizi tu kwa Sababu Mimi ndiye aliyenunua, ingawa mwanasheria wa ofisi ya ardhi alisema kwamba "lease" ni halali, ingawa wazee wa mahakama walikubali kwamba mimi ni mmiliki jaji aliamua kwamba kweli mimi ni mmiliki lakini alisema kwamba ofisi ya ardhi walifanya kwa hiyo lazima nimpe yule mtapeli mali yangu, yaani kiwanja changu! Unapenda kujua nini tena?
 
Ok, jiaribu kutatua tatizo lako kwa njia nyengine huenda ukafanikiwa
 
Nakushukuru sana.
Sijui Kama ni jaji au hakimu. Wote wanamwita "jaji". Kesi ilisikilizwa mahakama ya ardhi. Mimi si mwanasheria lakini nmeshangaa sana. Nataka kukata rufaa lakini yule jaji anachelewa sana kutoa nakala ya uamuzi na leo ameenda likizoni!
Mwishoni mimi siruhusiwi kuuza kiwanja! Siwezi kusubiri miaka 12, nitakufa. mimi nina miaka 72! Asante.
 
Hamna mtu wa pili.
 
Hata Korea kaskazini walitengana sembuse sisi
 

Nakala ya hukumu nafikiri haitegemei uwepo wa huyo jaji, mpaka anaenda likizo ujue kasha maliza shughuli zote za kiofisi, nenda kwa msajili wa hio mahakama umwambie umuhimu wa hio nakala kua unaenda kukata rufaa na akusaidie kuipata.
 
Nakala ya hukumu nafikiri haitegemei uwepo wa huyo jaji, mpaka anaenda likizo ujue kasha maliza shughuli zote za kiofisi, nenda kwa msajili wa hio mahakama umwambie umuhimu wa hio nakala kua unaenda kukata rufaa na akusaidie kuipata.
Inategemea na uwepo wa jaji kwa sababu hukumu imo katika kompjuta yake!
 
pole mkuu hiyo ndo zanzibar si bara huko.. wazanzibari wakiwa huku ni watanzania wenzetu na tunawachukulia fresh kama watanzania wengine ila sisi tukiwa huko kwao visiwani tunakuwa ni wa bara na wao ni wavisiwani wanabebana vibaya kuna kisa kama hicho kiliwahi kujitokeza kipind nikiwa huko na actually kwa huko zanzibar vipo visa vingi vya namna hiyo kukusaidia tu, kama unataka kukata rufaa mtumie mwanasheria chapchap afuatilie hiyo nakala ya hukumu hapo unachochezewa wewe ni kucheleweshwa kwa makusudi kuipata hiyo ukumu ili muda wa rufaa upite ili ukose haki yako...yani hapo kesi ya nyani umeipeleka kwa tumbili wazanzibari kila mtu kwao huko ni hami yake ukicheza kidogo hapo inakula kwako komaa nao hao nenda mahakama kuu ikishindikana nenda ya rufani huko hadi haki yako ipatikane..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…