Usafiri wa Train ni wa lazima sana China nafikiri kuliko usafiri wa ndege, hii inatokana na mabadiliko ya hali ya hewa zinazotofsutiana sana kutoka mji moja kwenda nyingine...kutofautiana kwa hali ya hewa inasababisha usafiri wa anga isiwe tegemeo sana kwani kuna wakati wanapoteza muda kwa safari za anga kusimama kwa muda kutokana na mabadiliko hayo.
Mfano Jiji la Shanghai hali ya hewa inabadilika kila wakati, unaweza kushangaa kutoka Guangzhou hadi Shanghai ukatumia masaa zaidi ya 10 kwa ndege au safari kuhairishwa kabisa. Hapo ndipo umuhimu wa train inaonekana.