BigBaba
JF-Expert Member
- Feb 7, 2017
- 1,908
- 9,040
1. Hao kuku wanaitwa Ayam Cameni , Ni Weusi kwa kila kitu mpaka nyama na kiini cha Yai,
2. Waligunduliwa nchini Indonesia Karne ya 17 na bado hawapatikani nchi nyingi Hadi sasa
3. Nchini Marekani waliingia mwaka 1998 na Yai moja la kuku Hawa nchini marekani linauzwa dola $130 Karibia Shilingi laki 3 za kitanzania
4. Kuku mzima nchini marekani anauzwa dola $2500 Takribani shilingi millioni 5.5 za kitanzania
5. Nyama yake inadaiwa Kuwa tofauti kidogo lakini inadaiwa Kuwa tamu zaidi kuliko kuku wa kawaida waliozoeleka
6. Wengine nchini Indonesia wanaamini kula nyama ya kuku hao inaongeza kinga ya mwili
7. Kula kiini kibichi cha Yai la kuku Hawa inadaiwa inasaidia Wanawake wajawazito wanaopata uchungu wa kuzaa muda mrefu kujifungua vizuri
Lakini mpaka sasa habari zinasema bado hakuna tafiti nyingi za kutosha wala kuridhisha ukweli wa mambo mbali mbali kuhusu kuku Hawa sababu bado hawajaenea nchi nyingi mpaka sasa