Je, wajua Bei ya Arabica ni kubwa kuliko Robusta?

Je, wajua Bei ya Arabica ni kubwa kuliko Robusta?

OLS

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2019
Posts
426
Reaction score
685
Kwa bei za kahawa zilizoanishwa na Benki ya Tanzania, kuanzia mwaka 2002 hadi mwaka 2020 bei ya kahawa aina ya Arabica imekuwa kubwa kuliko bei ya robusta kwa mauzo ya kilogram moja kwa Dola za kimarekani

1643026328320.png


Wastani wa bei ya kahawa aina ya Robusta ni Dola 1.7 kwa kg wakati Arabika ikiwa ni 3.2 USD. Aidha kwa kipindi cha kuanzia 2002 hadi 2020 bei kubwa iliyowahi kurekodiwa kwa kahawa ya robusta ni dola3.7 ambayo ilitokea mwezi februari na marchi mwaka 2020 wakati bei kubwa ya arabika ilikuwa ni Dola 6.6 ambayo ilikuwa miezi ya mwanzo ya mwaka 2011

Kabla haujaamua kulima angalia trend ya bei za zao husika na kuproject miezi kadhaa ijayo ili uwe salama kibiashara

1643026549683.png

Data Source: BoT
Signed: OEDIPUS
 
Naomba kufahamu. Sisi walaji wa ndani... kama Tanzania, Tunakula Arabica au Robusta??
 
N wapi wana mbegu za kahawa..
Nazihitaji nipate ungaunga wake usio wa kiwandani
Muhimu
 
Huku kijijini kwetu gahawa ni anasa, asubuhi tuna kulumangia ugali na chai, mchana ugali dagaa na usiku wali na mboga ya serikali...
 
Hivi vitu sinaga hata mzuka navyo yaani, bora ninywe chai tu au tangawizi
 
Back
Top Bottom