3. Japo Spika Mhe. JYN tayari ameisha jiuzulu uspika, kujiuzulu huko, japo ni kujiuzulu batilifu, lakini kujiuzulu ni kujiuzulu na Spika amejiuzulu, lakini kwa kuheshimu katiba, lazima ubatili katika barua hizo uondolewe kwa kuandikwa barua rasmi kwa mujibu wa katiba.
4. Bunge lipokee kimya kimya barua mpya ya kujiuzulu kwa Spika iliyoandikwa kwa mujibu wa katiba, kisha Bunge ndio litoe copy kwa CCM.
Hitimisho.
Namalizia kwa lile swali la msingi la uzi huu
Je wajua, haramu Isipoharimishwa Inageuka halali?, na batili Isipobatilishwa inageuka halali!. Je, Tanzania, tuhalalishe ubatili huu wa kujiuzulu kinyume cha katiba kwa mkuu wa mhimili wetu wa Bunge? Kama katiba imeelekeza jinsi ya kufanyika kwa jambo fulani, kuna sababu gani ya msingi ya kutofuata katiba na badala yake tukumbatie ubatili?
Jumatatu Njema.
Pascal