Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 1,831
- 5,489
Tunapofikiria jangwa, kwa kawaida huwa tunapiga picha maeneo yenye joto na mchanga kama Sahara. Na ni mara nyingi watu huhusisha jangwa na mazingira ya joto, yenye mchanga na Jua kali lakini kiuhalisia jangwa hufafanuliwa na viwango vyao vya chini vya mvua. Kwa hivyo, jangwa ni sehemu ambayo haipati mvua nyingi.
Jangwa kubwa zaidi ulimwenguni sio Sahara lenye mchanga, lakini ni bara la barafu la Antaktika. Antaktika ni jangwa kwa sababu kuna baridi kali na linapata mvua kidogo sana, hasa katika umbo la theluji kwa mwaka. Ni kama jangwa lililoganda!
Ingawa tunaweza kufikiria jangwa kuwa lenye joto na mchanga, la hasha Antaktika ndilo jangwa kubwa zaidi ulimwenguni kwa sababu ni kavu sana, na kwa namna nyingine ni la baridi sana. Na pia Antaktika ndilo bara kame na lenye upepo mkali zaidi Duniani.