Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
JE WAJUA KUNA ALAMA ZENYE MAAGANO NA VIAPO? JITAHIDI SANA KUZILINDA MAADUI ZAKO WASIZIPATE.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Alama!
Watu wengi hawana ufahamu Mkubwa kuhusu Elimu ya ALAMA.
Alama zipo nyingi Sana na zina matumizi Mengi Sana.
Alama ni kitu au Jambo linalobeba au kurejelea maana Fulani.
Kuna Alama za Mahesabu, alama za Barabarani, Alama za kitaifa, alama za hali ya hewa na mazingira n.k.
Alama zinmatumizi mbalimbali kama vile;
a) Kutoa ishara au tafsiri, au taarifa au maana Fulani(mawasiliano).
Ingawaje sio kila alama inamaana kwa watu wote.
b) Kuweka Kumbukumbu
c) Kuweka utambulisho
d) Kuficha Jambo na kulifanya kuwa la Siri
e) Kuweka Ulinzi na usalama.
Kwa vile sitaki kuwachosha, Leo Mtibeli ataeleza Alama zenye Maagano na Viapo;
Sio kila alama imewekewa Maagano na Viapo. Zipo Alama ambazo zimewekewa Maagano na Viapo. Nitafafanua.
1. Kuna Maagano ya Kimwili na Maagano ya Kiroho.
2. Maagano ya Kimwili haya utayakuta hata Jeshini au mambo ya kipelelezi.
3. Maagano iwe ya Kimwili au ya Kiroho huwa ni Siri kwa sababu Maagano yamebeba nguvu ya makubaliano ya watu wawili au Makundi ya watu wawili.
4. Kwenye Mambo ya Kijasusi Alama, Code au ishara ni muhimu Sana.
5. Watu wawili hufanya agano(makubaliano) kwamba tutashirikiana kwa Jambo Fulani, kisha tuweka Alama hii ambayo hii itakuwa kama utambulisho ili tusidhuriane au ili watu wangu wasikudhuru na wako wasinidhuru, au ili watu kutoa taarifa Fulani za kiulinzi na kiusalama.
6. Mfano wa ALAMA YENYE MAAGANO ya Kimwili, Kisa cha Majasusi 12 wa Israel Kule Yericko na RAHABU KAHABA.
Kisa hiki ALAMA waliyoiweka ilikuwa KITAMBAA CHEKUNDU lakini Chenye agano lao yaani Majasusi 12 na RAHABU KAHABA.
Kitambaa chekundu ilikuwa Alama yenye agano baina ya Rahabu na wapelelezi ambapo Wapelelezi walimwambia Rahabu akiweke hicho kitambaa chekundu dirishani, kwa Nje juu ya ghorofa ili jeshi la wayahudi likija kuupiga mji wa Yeriko nyumba watakayoona kwenye dirisha kuna kitambaa chekundu hawataishambulia Wala Kuua watu wake.
Hilo lilifanikiwa.
Hii inamaanisha kwa wengine ambao wangekuwa wanakiona kile kitambaa chekundu kikining'inia wangeona ni Jambo la kawaida lisilo na maana lakini kumbe ilikuwa ni alama ya Siri yenye agano kubwa lililobeba ulinzi na wokovu wa kutokuangamizwa.
Kama ingetokea mtu akakitoa kile kitambaa iwe Kwa bahati mbaya basi Rahabu Kahaba angejikuta kwenye tabu. Lakini uhakika ni kuwa, Rahabu kwa vile anajua Alama Ile unaumuhimu gani lazima kila mara alikuwa akichungulia kama kitambaa kile chekundu kipo au hakipo.
Pia, endapo angetokea mtu mwingine kwa Siri kubwa akasikia hayo mazungumzo kisha naye akaweka kitambaa chekundu kwenye Dirisha la nyumba yake huenda naye angesalimika pindi jeshi la waisrael likija kuuangamiza mji wa Yericko.
Alama zingine ni kama rangi au nguo aina Fulani.
Mfano, Kwenye Vita Wanajeshi hupeana Alama ambazo zitawatambulisha wao ni kitu kimoja.
Hapa watavaa nguo za kijeshi zenye Alama zinazowatambulisha kama jeshi Fulani.
Mfano, Jeshi la wananchi la Tanzania, JWTZ wao wanasare Zao zenye Alama Zao, wanapoenda kupambana na Jeshi jingine mfano M23 hujitofautisha na wao kwa Sare za Nguo.
Hata hivyo kuna ALAMA za Siri ambazo wanapoenda Vitani hupewa, hizi sio Alama za kuonekana. Huweza kuwa NENO Fulani, au ishara Fulani ya mwili. Hii ni kuepusha endapo adui akavaa Sare za nguo za kijeshi zinazofanana na sare za JWTZ.
Alama zingine za Kimwili ni kama Pete za ndoa n.k.
7. ALAMA ZA KIROHO.
Zipo Alama za kiroho zenye Maagano.
Mfano, ukienda kwa mganga, Mganga anaweza kukupa Pete au bangili ambayo ni alama inayokutambulisha popote uendapo.
Mtu anaweza kukuona umevaa Pete au Bangili ya Kawaida lakini kumbe wewe Pete hiyo ni Jambo kubwa Sana katika maisha yako.
Alama hiyo unaweza ukiambiwa usiivue, au ivue wakati au katika mazingira Fulani.
Wengine hupewa Hirizi au hupewa kitambaa au huambiwa wavae nguo Fulani ambayo hufanyiwa Dua maalumu kisha kifaa hicho huwa kama Alama katika ulimwengu wa Kiroho.
Mfano, ni Kisa cha Kaini kuwekwa ya Kiroho na Mungu.
Mfano mwingine ni Wana waisrael walipokuwa Misri wanaambia ili watoto wao WA Kwanza wasife itawapasa Wachinje mnyama kisha Ile Damu waweke kwenye miimo ya milango Yao ili Yule Malaika muuaji atakapopita usiku akikuta Damu kwenye huo mlango atambue nyumba hiyo ni yawanaisrael
Ikiwa mwana wa Israel atakaidi na hataweka hiyo Alama hiyo itamaanisha atapata madhara na mtoto wake wa Kwanza atakufa.
Hii itaenda sambamba na Ikiwa kuna wamisri Wachache waliipata Siri hiyo wakaweka Alama hiyo ya Damu kwenye miimo ya milango Yao, hawatadhurika.
Alama zenye Maagano huwa ni Siri ili kuepuka kuibiwa na maadui.
Samsoni yeye agano lake lilikuwa ni kutokunyoa nywele zake. Nywele kwake ndio ilikuwa Alama yenye agano kubwa.
Hivyo Samson anapomuomba Mungu wake ili amsikilize lazima azingatie uwepo wa ALAMA ya Nywele ambapo ndio agano lao.
Kitendo cha kutoa ALAMA au Nywele, ni kukata mawasiliano baina yake na Mungu. Hivyo zile nguvu zake zinakuwa zimeyeyuka.
Katika ulimwengu huu kila mafanikio yanasiri ndani yake. Na katika Siri hizo kuna Maagano yaliyowekwa kwenye ALAMA Fulani katika maisha ya Mtu.
Mimi nimechoka, Acha nipumzike sasa.
Nawatakia maandalizi Mema ya Sabato
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam