Je, wajua kuwa hatma ya CHADEMA ipo mikononi kwa Lwakatare? Baada ya CHADEMA kumwaga ugali, Lwaka akiamua kumwaga mboga, CHADEMA kwishney!

Duh....kwa hivyo unataka chama cha siasa kiache kuzingatia kanuni na katiba yake katika kuleta nidhamu, kianze kungalia sura za watu? Ikiwa hivyo, basi hicho chama si ni bora kife tu!?

Nafikiri kama tunaweza kukubaliana kuwa hao wabunge wamefanya makosa kwa mujibu wa taratibu za chama chao, then hatua ambazo chama imechukua ni a kupongezwa! Lazima watu wawe na nidhamu. Nje ha hapo itakuwa holela.

Hili la kuanza kutizamana usoni au kutizama nani "kabeba mboga" sio kitu cha kukikaribisha kwenye chama au taasisi yoyote ile.

Kwa hivyo wabunge wengine ni haki wafukuzwe kwa kuwa tu hawajabeba mboga? Kwa kosa linalofanana na kosa la Lwakatare?

Mimi nafikiri kama tunataka kuishauri CDM, basi iwe ni kufuata katiba na kanuni zake bila kukomoa yoyote. Kama wabunge hawana makosa, tuseme hivyo na kuonesha ni kwa vipi ....either hawana makosa, au makosa waliyofanya hayastahiki adhabu waliyopewa.
 
KAka
 
Unajiona bingwa wa kupiga ramli....Usijione unawaza sn kuliko waliomfukuza kwan wao ndo wanamjua kuliko wew.Achana na ramli za kisukuma...baada ya kuoteaotea unajiona proffesional wa ramli hvi lwakatare ni zaidi ya akina zitto na Slaa?.Acha ulevi wa ramli
 
Mjinga Huyu jamaa anamaanisha vyama vinafanya ughaidi ambao ni kosa la jinai, muda wote huo inteligensia imara isiwagundue na kuwakata na kuwashitaki.
Mpaka rwakatare afukuzwe uanachama alafu ndo eti afungue mdomo,
Chadema kinavyowindwa hakiwezi fanya huo ugaid msajiili akawa anakiangalia tu angekifutilia mbali, sababu Kila siku msajili anakiwinda kwa Kila namna
 
Kama Chadema inakufa kweli, kama tuna uhakika na hili basi turuhusu yafuatayo
Tuwe na Tume huru, Tuwe na Wasomamizi huru, tuwe na Free and Fair campaigns, Jeshi la Polisi lisijihuishe na siasa kama ilivyo sasa, kuwe na Katiba huru (wenye akili wameelewa), turuhusu mikutano ya siasa. hayo machache tu. Then baada ya hapo turudi tukae mezani tuone kama inakufa au inaishi
 

Nadhani umeandika hii ukiwa ‘bwii’.
CDM haijafa alipo ondoka Dr Kaburu
CDM haijafa alipo ondoka Dr Slaa
CDM haijafa alipo ondoka Lowassa

Ndiyo ife kwa huyu aliye kufa kisiasa ambaye hata 2020 hawezi mshinda tena Balozi Kagesheki?
Doesn’t make any sense mkuu


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Sio Lwakatare tu, huwa nawashangaa sana CHADEMA kumdhihaki Jaji Feleshi, kila siku huwa nawaeleza humu, ushahidi tena ule unaitwa "a water tight evidence" juu ya ugaidi wa CHADEMA Mwanza na ule wa Tabora uko mezani, walireconcile na JK akamuomba DPP by then akiwa Jaji Feleshi awaondolee mashitaka. Huyo wanaemdhihaki sasa ndo Jaji Kiongozi na anawafahamu vizuri.

Lwakatare ambaye alijitoa mbuzi wa kafara sasa wamemgeuka na hana cha kupoteza, alichobakiza ni kushirikiana tu na ofisi ya mashitaka mambo yaibuliwe..siombei hilo wawaache tu October sio mbali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahahahhaa mimi uelewa wangu mdogo, mimi huyo? Et NCCR ilikuaje? Pathetic
Mtu anakuambia chadema kinakufa au kinauliwa kwa nguvu kupitia wakurugenzi, time ya uchaguzi, polisi n.k, lazima tufahamu waafrika ni watu wajinga na wapumbavu ndo maana wazungu wanatuzarau sana, kwa sababu huwez kuwa mtu mwenye akili ukadharauliwa, mbaya Zaid wasomi ndo wanaongoza huu ujinga
 
Nyie ndio mmeijulia Chadema kupigia jf!
Kiufupi huna ujualo

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani wewe ambaye hata JF umeijua 2014 ndio unamwambia aliyejiunga JF 2008 kuwa kaijua Chadema kupitia JF na kwa hivyo hakuna ajualo!!
Ndio maana sisi wengine tumeamua kuwa waangaliaji tuu humu maana tuna wajukuu humu ambao hata harufu ya maziwa haijawatoka bado,vijana ambao bado mpo kwenye balehe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…