Je, wajua kuwa Simba ndio ilisababisha Tanzania kuitwa kichwa cha Mwendawazimu?

Hayo ni mawazo Yako, Mimi nimekupa habari kama ilivyokuwa wakati huo.
 
Hili bandiko alione Kalpana ili awashauri mbu3 wenzake waache kuwa vichwa vya wendawazimu [emoji1][emoji1][emoji1][emoji23][emoji23]
WWala sijisumbui kulisoma maana ni chuki binafsi tuu hizo..nimeishia kichwa cha habari hapo juu..ila nimekuja nimeheshimu wito wako...
 
WWala sijisumbui kulisoma maana ni chuki binafsi tuu hizo..nimeishia kichwa cha habari hapo juu..ila nimekuja nimeheshimu wito wako...
Sasa mkuu kama ingekuwa chuki au ni habari isiyo na ukweli Wana Simba si wangekuwa wamemshukia tayari?
 
KIA ndio ulikua usafiri maarufu Kwa hapa DSM kama daladala nikama Sasa zinavyotesa Nissan Civilian. Mnajazana Nyuma uko ata Dereva haoni. KIA zilikuja baada ya Serikali kuruhusu biashara huria kwenye usafirishaji maana Kampuni za usafirishaji za Serikali UDA zilizidiwa na wingi wa Watu.

Watu mnapanga foleni kupanda UDA kwenda kazini ambayo ni mabasi ya shirika linalo milikiwa na Serikali, Mkirudi mkapange foleni kununua sukari kwenye maduka ya ugawaji Sasa kupunguza adha hizo watu binafsi wakapewa Fursa.
View attachment 2544954
 

ABIOLA hakuwa dikteta.
 
Mashabiki wa rainbow fc wanapenda kuisema simba sana mambo hayo yalishapita
 
Nadhani mleta mada ametereza kidogo, sio toyota KIA bali ilikuwa ni KIA. Kama sikosei ilikuwa gari za kutoka Korea, kwa kipindi hicho ilikuwa ni gari popular Tz/Dar.
 
Kiukweli huwa nikiangalia mpira wa sasa wa Simba na Yanga na Tanzania kwa ujumla, najaribu kufananisha na miaka ya tisini then naangalia na maslahi wanayopata wachezaji zama hizi daah ni mbingu na ardhi.

Siku hizi vijana uwezo mdogo kelele nyingi na maslahi yako juu kweli huku kipindi cha nyuma watu walikuwa 'mafundi' haswa halafu hakuna maslahi.

Mtu aliye shuhudia mpira Tz wa miaka ya 90 kurudi nyuma hawa vijana wengi wa leo ataona wanaruka ruka tuu.
 
Sasa hivi fedha Ipo ila mpira hamna, chakushangaza kwasasa soka linaendeshwa kitaalamu sana ila wachezaji wazuri ni wachache. Mfano mdogo Kwa Simba au Yanga ya 1993 kama Kwa awa mapro wanatoka nje ni wachache sana wangeweza kupata namba kwenye kikosi Cha kwanza Cha hizo timu.
 
Sasa hivi fedha Ipo ila mpira hamna, chakushangaza kwasasa soka linaendeshwa kitaalamu sana ila wachezaji wazuri ni wachache.
Kwa maoni yangu, nadhani ubabaishaji wa mfumo mzima wa michezo hapa nchini umefanya hii tasnia kupuuzwa sana. Jinsi set up ya wizara husika pamoja na vyombo vyenye dhamana km TFF nk vinavyo endesha mambo yao.

Michezo na sanaa hapa Tz kwa kiasi kikubwa bado inachukuliwa kama 'uhuni' usio na future. Hili limefanya wazazi/walezi wengi kutoruhusu watoto wao (wenye vipaji halisi) kushiriki michezo/sanaa, matokeo yake wengi wanao elekea huko imekuwa ni wale wasio na mbadala kwenye maeneo mengine ya fursa.

Miaka kadhaa nyuma kwa mfano mashindano ya urembo ('mamiss') washiriki wengi walikuwa wanavyuo, walivyo ingiza 'ukanjanja' watu wameyapuuza pia. Bongo movie na music pia zinachukuliwa hivyo.

Pamoja na uwekezaji mkubwa ikiwemo endorsement za makampuni kibao na uboreshwaji wa facilities bado uwiano kati ya uwekezaji unaofanyika na tija inayo patikana ni kama una mahusiano hasi vile.
 
Walio bahatika kumuona Yusufu Macho au Hamis Tobias Gaga kwenye ishu ku Comand mpira au kupiga mashuti basi Feisal hafiki ata nusu.
Kuna mechi ya Yanga na Sigara pale shamba la bibi, Hamisi Gaga akiwa Yanga alipiga shuti na kuchana nyavu Sasa uwa najiuliza mpaka Leo Ile ilikua nguvu ya kupiga au Nyavu zilikua zimeoza!![emoji1][emoji1].
 
[emoji2][emoji2][emoji2]
Hamis Thobias 'Gagarino' na Yusuf Macho 'Muso', viungo hatari kabisa hawa miaka hiyo daah!!
 
Hivi Dua alikuwepo!?..aliyeiponza ni mfadhili,alihonga baadhi ya wachezaji, fullback ya kulia ilikua uchochoro kusudi tu,mwameja akimlaumu 'mbona unamuacha huyo anapita tu'!?..hapo Azim dewji alijifanya anaumwa,kalazwa hospitali muda wote wa maandalizi
 
Hao uliowataja walikua wakipiga haswa mashuti,macho alipiga shuti faulo makundi 2003,kipa mwarabu alielemewa kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…