Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
- Thread starter
-
- #21
Mkuu Bramo, hata kupetition kuwa advocate sijapetition na huwezi amini mahakamani sijakanyaga!, kwa sasa nafanya media wind up niachane rasmi na media ndipo nigeukie upande wa pili, bahati mbaya sitajielekeza kwenye litigations, mimi nitajikita kwenye legal opions only hivyo hutakaa unione au unisikie mahakamani!.Mkuu Pasco hivi na wewe unapataga client wa kuwatetea Mahakaman.
Nadhan watakuwa wote wameshindwa kesi na pengine kuswekwa Lupango kabisa
Mkuu nameeless girl, asante, noted, action takenEdit kwanza maelezo ya namba 4 then tutaendelea...
tumeshaungana sasa haijalishi historia yetu ya kuungana ipoje, ni kama ukijua kuwa ulizaliwa baada ya baba ako kumbaka mama yako, tusonge mbele tuweke makubaliano mapya katika katiba mpya tuimarishe muungano wetu unaoendana na kizazi chetu, tusiendelee kuwa watumwa wa historia
Nadhani wakati bunge la
katiba linaanza kesho hapo mjini Dodoma, the hottest issue itakuwa
muungano wa serikali ngapi, natamani pia hili swali la kutokuwepo kwa
mkataba wa muungano kujadiliwe, ili sasa tuwe na mkataba rasmi wa
muungano zaidi ya kile kiini macho cha muungano!.
Nawatakia wajumbe wa bunge la katiba, majadiliano mema!.
Pasco.
Wanabodi,
Wakati tukijiandaa rasmi kuingia kwenye serikali 3, tutake tusitake, lazima tutarudi nyuma kuungazia muungano wetu, na kabla hatujaingia katika serikali tatu, lazima kwanza tuwe na Mkataba rasmi wa Muungano, ndipo zifuate hizo serikali 3. Hiki kilichopo, kinaichwa Mkataba wa Muungano, "Articles of Union", kiukweli, nasema bila kumung'unya maneno, sio Mkataba wa Muungano (contract), bali ni Makubaliano ya Muungano (Agreement) tuu.
Kuna tofauti kubwa kati ya Mkataba na Makubaliano, kila mkataba ni makubaliano, ila sio kila makubaliano ni mkataba!. Yaani "Every contract is agreement, but not every agreement is a contract!".
Ili makubaliano yaitwe mkataba, ni lazima makubaliano hayo yawe na sifa kuu nne za mkataba. Kwa bahati mbaya sana, Makubaliano ya Muungano wetu, yamekosa baadhi ya sifa hizo muhimu.
Ambatana nami katika kuyachambua haya makubaliano ya muungano kwa nini ni makubaliano tuu na sio mkataba, na niu kwa nini lazima kwanza tuwe na mkataba wa muungano ndipo tuweze kwenda kwenye serikali tatu.
Kwa wale wenye nafasi, mnaweza kuanza kuyapitia haya makubaliano ya muungano, kisha tutapelekana kidogo kidogo kwa lugha rahisi kwa kila mtu kulielewa hili.
NB. Mambo mengine, yako kisheria zaidi, ila bado I stand to be corrected na "the learned brothers and sisters"
Kwa wale ambao sio wanasheria, unaweza pia kuwa mwanasheria bila kusomea chuo chochote
kwa kuanzia jisemee mwenyewe
NB. Japo makubaliano haya ya muungano sio mkataba, na japo hayakuridhiwa rasmi Zanzibar (ratification), bado ni makubaliano halali, hivyo muungano wetu ni halali na nchi yetu Tanzania ni nchi halali (de facto) ila sio halali kisheria (de jure).
- What is a contract?
- What is an agreement?
- What are the differences between Contacts and Agreements?
- Why every contract is an agreement but not all agreements are contracts
- Baada ya kusoma hayo hapo juu, tunaweza kwenda pamoja kujua kwa nini makubaliano ya muungano sio mkataba!
Karibu uandamane nami.
Pasco.
Up Date !.
Happy New Year!
Pasco.
Sure brothr u got it. Th suimming is annext to academic field n not into matirial legality of the so called contract herein refered to as a mere agreement.Pasco you are swimming into academic reservoir not reality.
.Leo ndio Sikuu ya Muungano, japo hati halisi za muungano, hatimaye zimetolewa huko zilikofichwa kwa miaka 50, bado kuna maswali bila majibu kuhusu hati hizo,
- Kwa nini zilifichwa miaka yote 50 na kuja kuibuliwa sasa?!.
- Kwa nini hakuna hati Zanzibar, wakati zilisainiwa hati mbili ya Tanganyika na Zanzibar?, kulikopelekea Wanzanzibari kwenda mahakamani kuidai hati yao?!.
- Kwa nini hati hiyo haikuambatanishwa na sheria ya muungano iliyotungwa tarehe 25/04/1964?!.
- Kwa nini hati hiyo haikuambatanishwa na tangazo la kuitambulisha Jamhuri ya Muungano ya Tanganyika na Zanzibar kujiunga UN?!.
- What was so special kuhusu hati hiyo, no a sigle copy was made up to 50 years ndipo imetolewa copy?.
Hayo ni maswali tuu, ila pia mimi Pasco wa jf, ni muumini wa serikali moja!.
Nawatakieni sherehe njema za muungano.
Pasco
tumeshaungana sasa haijalishi historia yetu ya kuungana ipoje, ni kama ukijua kuwa ulizaliwa baada ya baba ako kumbaka mama yako, tusonge mbele tuweke makubaliano mapya katika katiba mpya tuimarishe muungano wetu unaoendana na kizazi chetu, tusiendelee kuwa watumwa wa historia
.
Kesho ni maadhimisho mengine ya sikukuu ya muungano, maswali yangu haya, bado hayajabahatika kupata majibu
Nawatakieni maadhimisho mema ya sherehe za muungano!.
Pasco
Mimi sina ufahamu mkubwa sana wa haya mambo ya muungano ila naomba kujuzwa kidogo.
1. Serikali moja ndo nini, au serekali mbili au tatu, mfumo wake ndo upoje hasa?
2. Tukipoteza huu Muungano watu wa Bara watakosa nini hasa kutoka kwa Zanzibar.
3. Kwanini Zanzibar hataki Muungano?