Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
- Thread starter
- #41
Nawatakia mapumziko mema ya leo siku ya Muungano.Wanabodi,
Wakati tukijiandaa rasmi kuingia kwenye serikali 3, tutake tusitake, lazima tutarudi nyuma kuungazia muungano wetu, na kabla hatujaingia katika serikali tatu, lazima kwanza tuwe na Mkataba rasmi wa Muungano, ndipo zifuate hizo serikali 3. Hiki kilichopo, kinaichwa Mkataba wa Muungano, "Articles of Union", kiukweli, nasema bila kumung'unya maneno, sio Mkataba wa Muungano (contract), bali ni Makubaliano ya Muungano (Agreement) tuu.
Kuna tofauti kubwa kati ya Mkataba na Makubaliano, kila mkataba ni makubaliano, ila sio kila makubaliano ni mkataba!. Yaani "Every contract is agreement, but not every agreement is a contract!".
Ili makubaliano yaitwe mkataba, ni lazima makubaliano hayo yawe na sifa kuu nne za mkataba. Kwa bahati mbaya sana, Makubaliano ya Muungano wetu, yamekosa baadhi ya sifa hizo muhimu.
Ambatana nami katika kuyachambua haya makubaliano ya muungano kwa nini ni makubaliano tuu na sio mkataba, na niu kwa nini lazima kwanza tuwe na mkataba wa muungano ndipo tuweze kwenda kwenye serikali tatu.
Kwa wale wenye nafasi, mnaweza kuanza kuyapitia haya makubaliano ya muungano, kisha tutapelekana kidogo kidogo kwa lugha rahisi kwa kila mtu kulielewa hili.
NB. Mambo mengine, yako kisheria zaidi, ila bado I stand to be corrected na "the learned brothers and sisters"
Kwa wale ambao sio wanasheria, unaweza pia kuwa mwanasheria bila kusomea chuo chochote
kwa kuanzia jisemee mwenyewe
NB. Japo makubaliano haya ya muungano sio mkataba, na japo hayakuridhiwa rasmi Zanzibar (ratification), bado ni makubaliano halali, hivyo muungano wetu ni halali na nchi yetu Tanzania ni nchi halali (de facto) ila sio halali kisheria (de jure).
- What is a contract?
- What is an agreement?
- What are the differences between Contacts and Agreements?
- Why every contract is an agreement but not all agreements are contracts
- Baada ya kusoma hayo hapo juu, tunaweza kwenda pamoja kujua kwa nini makubaliano ya muungano sio mkataba!
Karibu uandamane nami.
Pasco.
Pasco