Je, Wajua Kuwa Tanzania Hatuna Mkataba wa Muungano? Kilichopo ni Makubaliano Tuu ya Muungano?

Pascal Mayalla kwa uzoefu wako uliotukuka huoni kuwa huu Muungano ulinzi wake unazidi kupukutika kila uchwao??

Kwa kifupi ni kwamba kizazi hiki cha sasa na kijacho Muungano kwao utakuwa ni Historia tu. Naweza kulinganisha na nyumba ya miti. Hivi sasa imeshashambuliwa na mchwa wakati wowote inaanguka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maalim Seif hajawahi pinga muumgano anachopinga siku zote ni muundo wa muungano.
 
Mkuu ulisema hakuna mkataba wa muungano. Vipi hakuna henga au hata kamfuko ka rambo ka kuhifadhia koti letu pindi likitubana na kulazimika kulivua?
 
Mkuu chagu wa malunde , hii ndio naiona leo. Vikao vya BLM ni kama Bunge, vina hansard. There is no any Documentary evidence ya ratification ilifanyika Zanzibar.
Happy New Year.
P
 
Kwa vile leo ni mwisho wa mwaka, nafanya tuu marejeo, niliwa kushauri nini, nini kilifanyika, na matokeo ni nini.
Kwaheri 2020, karibu 2021.
Mimi na familia yangu tawatakia Heri ya Mwaka Mpya.
Paskali
 
Mkuu chagu wa malunde , hii ndio naiona leo. Vikao vya BLM ni kama Bunge, vina hansard. There is no any Documentary evidence ya ratification ilifanyika Zanzibar.
Happy New Year.
P
Tafsiri sahihi ya neno ratify ni kutambua au kurdhia. Ni kweli kuwa BLM halikuridhia? Mimi binafsi haingii akilini maana kwa Wazanzibar Muungano ulikuwa ni wa lazima.
 
Nawatakia maadhimisho mema ya sikukuu ya muungano.
Paskali
 
Wanabodi,
Leo sikukuu ya Muungano, nafanya mapitio ya baadhi ya mabandiko ya muungano.

Japo waasisi wa muungano wetu huu adhimu ni Nyerere na Karume, muungano ni kama ndoa, kuna mtu ana proposes, mwingine anakubali, ndoa inafungwa. Kwenye muungano wetu huu adhimu, aliye proposes ni Nyerere, Karume akakubali. Nia ya Nyerere ni kwenda kwenye serikali moja. Wito kwa viongozi wetu, kama nia ya kweli ni kudumisha muungano, twende kwenye serikali moja. Tumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kuyaishi maono yake!. Nawatakia Muungano Mwema.

Paskali
 
eo ni Sikukuu ya Muungano, nachukua fursa hii kuutafakari Muungano wetu adhimu, kupitia hoja mbalimbali za kimuungano.

Nawatakia maadhimisho mema ya muungano na mapumziko mema.
P
 
Nipe tofauti Kati ya "makubaliano" na "mkataba"
Karibu
P
 
Huyu naye ni kilaza tuu wa sheria kama wale vilaza wa IGA, kisheria hati za muungano sio mkataba, ni makubaliano tuu!. Je, Wajua Kuwa Tanzania Hatuna Mkataba wa Muungano?. Kilichopo ni Makubaliano Tuu ya Muungano?!. tumeyasema humu 10 years back!, wakati huo yeye akimtumikia kafiri!.

Tena nilimpendekeza huyu ndiye ampokee Mwinyi kule Zanzibar ili Mwinyi aje huku kumpokea Mama ile 2025, Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke
Lakini kwa kauli hizi, huyu jamaa ni hatufai, hatufai, hatufai kabisa!.
P
 
Hawafai kina nani?

Sent from my ATU-L31 using JamiiForums mobile app
 
Kweli nimekumbuka nilipitia sheria kidogo Kuna contract and agreement kunacontract or agreement ,
Sawa sasa tueleze
nini madhara yake kisheria agreement dhidi ya contract.
 
Leo tunapo adhimisha miaka 60 ya huu muungano wetu adhimu, nafanya tafakuri, niliwahi kuandika nini humu kuhusu muungano wetu.
Nawatakia maadhimisho mema ya miaka 60 ya muungano wetu adhimu.
Ujumbe wangu ni muungano wetu adhimu udumu milele, na sasa ni muda muafaka tuachane na huu muungano wa kimaghumashi, wa union na federation, sasa twende kwenye muungano wa kweli wa union wa nchi moja, serikali moja, na rais mmoja!.
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Tusaidie
P
 
Cha maana ni willingness or lack of....

Kama watu hawataki Muungano hata kama mna mkataba uliosainiwa na kusimamiwa na Malaika utakuwa hauna maana..., na kama watu wapo willing hata kama hakuna mkataba wala makubaliano wataendelea kuungana...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…