Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Afya ya akili...Salaam, Shalom.
Tanzania kuibeba Dunia, Hilo tu tayari ni HOJA fikirishi.
Kabla sijaenda ninakotaka kuelezea, ZIFUATAZO, ni sifa za Nchi hii ambazo, huwezi kuzipata Mahali pengine popote duniani katika macho ya kibinadamu katika Ulimwengu wa mwili.
1. AMANI
Pamoja na Nchi hii kuwa na makabila mengi kuliko Nchi nyingine yoyote duniani, Bado watu wa Nchi hii wameendelea kuishi kwa Amani.
2. UPENDO
Pamoja na tofauti za kiimani ,kitamaduni, nk nk,Bado Nchi hii unaweza kwenda popote na kupokelewa na yeyote popote na kukarimiwa.
3. UTAJIRI
Amini usiamini, Kuna watu wanasema kuwa congo ndiyo inayoongiza Kwa utajiri chini ya ardhi, Si Kweli, vilivyomo chini ya ardhi ya nchi hii, ambavyo havijavumbuliwa Bado, hakuna kama Tanzania.
4. UTULIVU
Mtanzania unaweza kumfananisha na Kondoo, Kwa nje ni kama dharau, lakini Kwa ndani ni silaha kubwa sana ya kulifanya Taifa kuwa hapa lilipo. Hata anapofanyiwa ubaya, hutulia, hata ukimdhulumu atanyamaza, na hata akiamua kufuatilia katika vyombo vya HAKI, ni Rahisi kusamehe na kumwachia Mungu.
5,6,7.......
Pamoja na sifa nyingi zinazoonekana Kwa macho, msingi wa Tanzania uko katika Ulimwengu usioonekana, na ndiko nitakapojikita zaidi.
Taifa hili, kama Kuna Nchi ambayo Mungu anaangalia Kwa ukaribu duniani baada ya Israel ni Tanzania.
Baada ya Messiah kuja duniani katika mwili wa mwanadamu, Alianza kuhubiri INJILI katika Israel, na akateua mitume, wanafunzi kuhubiri INJILI duniani kote,
INJILI hiyo imehubiriwa katika mataifa mbalimbali Kwa njia ngumu sana, wengi wa wanafunzi wa Yesu na wapeleka INJILI waliuawa na kukataliwa, na Kwakuwa, INJILI wanayoihubiri asili yake ni mbinguni, Dunia haikuipokea Wala kuwapokea wahubiri INJILI Kwa kiasi kikubwa.
KIVIPI TANZANIA IMEIBEBA DUNIA?
Kuibeba Dunia ni kufanyika LANGO. VIASHIRIA vyote nilivyoyaja pale juu, ni matokeo ya nchi hii kuwa center ya Amani na mazuri yote ambayo hupita na kubariki Dunia nzima.
1. KANISA LA MWISHO LITAKUSANYWA KUTOKEA TANZANIA.
Hapa katika Nchi hii, lile Kanisa la kwanza lililotawanyika Kutoka Israeli kwenda mataifa mbalimbali kuhubiri INJILI, litajikusanyia tena Kutokea hapa kwenda kuhubiri INJILI ya ufalme Kwa mataifa yote.
Kama ni mtu wa Roho, tayari harakati hizo zimeanza kuonekana.
Nitaendelea.........
We mzee acha kututisha basiINAENDELEA......
1. KANISA LA MWISHO LITAKUSANYWA KUTOKEA TANZANIA.
KANISA la kwanza lile lilikoachwa na mitume, lilianzia Yerusalem na kuenea duniani kote limepitia changamoto na vita kubwa sana, utawala wa kidunia haukuikubali INJILI iliyohubiriwa na mitume na wanafunzi katika Kanisa la kwanza, mitume wengi waliuawa wengine Kwa kukatwa Vichwa, lakini INJILI Ile ikiendelea kuhubiriwa,
Ilipoonekana kuwa INJILI hii haizuiliki, ndipo utawala wa Rumi, wakishirikiana na Wayahudi waliomkataa mwanzilishi wa INJILI hii ya ufalme, wakaamua kubadili mbinu ya Kupambana na kuenea Kwa Kasi Kwa INJILI Ile ya Kanisa la kwanza,
Kilichofanyika, wakaanzisha kitu kinachoitwa Dini na mfumo wa kuabudu ulioshikamanishwa na mfumo. Katika aina hii ya dini, Ili uabudu, ulihiyaji kusajili na kupata KIBALI Kwa Watawala, ndani ya mfumo huo Ile INJILI ya Kweli iliendelea kuminya , watu hawakubughudhiwa tena Wala kufungwa.
Zilianzishwa dini na madhehebu ambayo hayakuzuia watu kujitenga na Mila zao, utaona wengine waliruhusu NDOA za mitala, wengine walipinga, wengine walinyamazia wizi Kwa waumini wao, kwamba, wakiiba huko makazini, wakileta sehemu ya pesa hizo Kwa watumishi, hawakuulizwa wamezipata vipi, Bali walipewa seat za mbele, na kupewa uongozi, nk nk, Polepole, ladha na uhalisia wa Kanisa la kwanza ukaanza kupotea Polepole.
Kila walipoinuka wale waamini wa Kweli waliohubiri INJILI Ile iliyoghoshiwa, walitimuliwa na KUTENGWA.
Tumefikia sasa, Israeli katika Taifa la AHADI, imepitishwa SHERIA ya kuzuia Jina la YESU kutajwa hadharani, na kwamba, kulitaja Jina Hilo hadharani, ungekabiliwa na kifungo nk nk.
Hali hiyo Kutokea katika Taifa la AGANO, ikupe kujua kuwa Yesu aliposema kuwaambia Wayahudi kuwa, Kwakuwa mmeukataa ufalme wa Mungu, ufalme huo wamepewa mataifa.
Tayari tupo katika kipindi na msimu mpya.
2023-2030 ni msimu mpya wa kuonekana Kwa uhalisia mgawanyiko wa kimfumo na kiutawala Kwa Dunia nzima.
Ni katika kipindi hiki, Dunia itapitia DHIKI ambayo haijawahi Kutokea kabla.
Ni katika wakati na kipindi hiki, Nchi zote duniani zitajaribu kutafuta kuungana Ili kupata nguvu ya pamoja kiuchumi nk nk nk, Nia nyuma yake ni kuwakusanya mataifa yote katika kitu kitakachoitwa DINI MOJA, SERIKALI MOJA, SARAFU MOJA,KIONGOZI MMOJA WA DUNIA NZIMA.NK NK.
Kwa jinsi ambavyo mifumo imeundwa kujitegemeza chini ya utawala mmoja uliojificha, Nchi nyingi hazitaweza kupingana na Nia hiyo.
Lakini, Cha kushangaza, Taifa hili, Tanzania, litaibuka na kuleta upinzani juu ya mfumo huu tofauti utakaokwenda kuanzisha Duniani.
Na jambo Hilo ndilo lotakalokuwa ni tiketi ya kuwakusanya wote yaani KANISA lile la kwanza halisi litajikusanyia tena kupingana na mifumo kandamizi itakayokuwa imeanzishwa.
KANISA la kwanza, litajikusanya tena baada ya INJILI ya ufalme kuwa imehubiriwa na wote ambao watakuwa wanapingana na mfumo mmoja ulioanzishwa Ulio tofauti na Mungu, watakuja hapa.
Ni wakati huo ambao, wote watakaokuwa wakipinga USHOGA, utoaji mimba, na Naibu mbalimbali watakuwa wakikatwa Vichwa.
KANISA katika kitabu Cha ufunuo, linatabiriwa na kupata picha Cha mwanamke, Nchi yetu kutawaliwa na kiongozi mwanamke Kwa kipindi hiki, Ina maana kubwa Kwa Kanisa.
ITAENDELEA......,
Noma asee kuna sehemu nimeenda nimekuta paka mmoja anaitwa hilo jina Genta sijui Gunta nikashtuka mnamuitaje nikaambiwa nikasema emu muiteni nione akaitwa kweli paka anakuja, noma JF kuna majina hadi ya mapakaAmani - kuna GENTAMYCINE vs LIKUD wanataka kuzichapa mda si mrefu
Upendo - nimeachwa solemba na juzi nimetimuliwa ujombani
Utajiri - nina alfu nne tu hapa
😂😂😂 HatariNoma asee kuna sehemu nimeenda nimekuta paka mmoja anaitwa hilo jina Genta sijui Gunta nikashtuka mnamuitaje nikaambiwa nikasema emu muiteni nione akaitwa kweli paka anakuja, noma JF kuna majina hadi ya mapaka
We endelea tu....2023-2030.
Hii ni miaka Saba.(7). Namba saba, Ina maana yake kiroho.
Wakati Ule Yusuph anatabiri miaka Saba ya CHAKULA tele na miaka 7 ya njaa Kali, namba hazikuja kimakosa.
Pia katika Nchi yetu, kiongozi wa Nchi anaondoka March 2021, miaka hii Hadi kufikia mwaka 2023, ilikuwa ni maandalizi ya kuingia msimu mpya 2023.
2023-2030 ni miaka Saba, utaniuliza, kipindi chote tutaendelea kuwa na kiongozi mwanamke? Hilo Kwa sasa Sina majibu yake.
Miaka Saba hii ni mingi sana Kwa yatakayojiri duniani, ni wakati tunaweza Sema ni kipindi Cha ADHABU juu ya Dunia.
Ni katika kipindi hiki kilipoanza tu, Dunia nzima ilipata upungufu wa Dollar, Uchumi wa Dunia ulianza kutikisika, ni katika mwaka huu, tayari vita ya Israeli na Palestina ikaanza,
Miaka hii Saba isipopunguzwa, wengi sana watapotea, miaka hii 7, kupunguza kwake ni kugawanyika Kwa 2, yaani miaka 3na nusu au 3.5. Kumbuka kuwa ikiwa tutapata unafuu huo, miaka 3.5 yaweza Anza hesabiwa baada ya 2021 maandalizi hayo yalipoanza.
ITAENDELEA....
Mwendelezo nitasoma keshoBANDARI SALAMA.
Ukiiniuliza kwanini kiongozi aliyepita, aliyeondoka March 2021 alosikiliza ushauri wa watumishi wa Mungu na Kutoka hadharani kuikataa CORONA wakati Dunia nzima ikiwa uvunguni kuongopa gonjwa Hilo la mafua hatari, jibu ni Hilo Hilo, kuwa Tanzania. ndio lango la Dunia katika Ulimwengu wa Roho.
Ukiiniuliza, kwanini mara tu baada ya kupokea uongozi wake, haraka sana alianzisha mpango uliokwama wa kuhamishia makao makuu ya nchi kwenda Dodoma, Jibu ni lile lile, Tanzania ni lango na imeibeba Dunia nzima katika Ulimwengu wa Roho.
Mpango huo aliupeleka Kwa Kasi na Hadi anaondoka alibakiza kidogo sana kukamilisha, na Kila alipoulizwa kwanini anayapeleka mambo hayo haraka, alisema kuwa muda ni mchache. Ukikaa katika KITI kikuu Cha Nchi, lazima utapata maelekezo ya KITI Kutoka Kila pande katika Ulimwengu wa Giza na Nuru.
Miungu ya nchi hii imejipanga na kusimika tangu zamani katika mji huu wa Bandari salama, na Kwakuwa aliyeichagua Nchi hii ana matumizi na Nchi hii Kwa yajayo tangu zamani, miungu iliyojimilikisha Nchi lazima ifurushwe. Kwakuwa miungu ni ya kiroho, hauonekani na madhabahu imewekwa juu ya nchi katika mji huo,
Mpambano huu wa kiroho ni LAZIMA utokee na mshindi kupatikana, Kwa kuwa vita ni ya kiroho, lakini madhabahu ni ya kimwili, na lazima matokeo ya kipigo Kwa miungu yatokee katika Ulimwengu wa Damu na nyama, mji lazima upigwe.
Utasoma mwenyewe, enzi za Nuhu, gharika ilipiga, Enzi za lutu Dodoma na gomora, moto ulishuka, vita ilikuwa ni kati ya miungu, WANADAMU walipopelekewa taarifa kuondoka katika miji Ile, walikaidi, kilichotokea wakaangamia pia.
Likewise, vita ya Bandari salama, ni ya miungu, Mungu wa Kweli, dhidi ya miungu ya nchi, wananchi wametangaziwa kuhama Ili kupisha vita hiyo katika eneo Hilo, ila Bado wanapuuza, vipeperushi wanapewa hawasikii, wanatangaziwa lakini wanapuuza, na Kwakuwa muda haujafika w deadline, ni matumaini yangu wananchi wayapisha uwanja wa vita Kwa kuhama, ni kama tu vile GAZA, wananchi walitangaziwa kuhamia kaskazini. Hata sasa ni hivyo, hameni.
Baada ya vita hiyo Kutokea na miungu ya nchi kuteketezwa, ndipo maandalizi ya kutengeneza mahala salama pankukimbilia mataifa baada ya kuanza kwanza kuhubiriwa Ile INJILI ya ufalme sawasawa na Mathayo 24 utakapoanza.
ITAENDELEA.....