Je, wajua kuwa Zanzibar haikuridhia Muungano? Ina Maana Gani?

Je, wajua kuwa Zanzibar haikuridhia Muungano? Ina Maana Gani?

Pasco,

Ahali yangu huo sio Muungano bali ni MVUNGANO.

Kwani ndanimwe kuna malalamiko na manung'uniko lukuki toka kwa wananchi wa nchi hizo mbili. Mvungoano huo utaona unalindwa na kutetewa na viongozi na sio wananchi wa kawaida.

Iko siku haki itasimama na Ulanghai utapotea.

Tuombe kheir

Hapa kuna ndoa ya wawili wapendanao, tatizo sio wanandoa bali ndugu wa mume na jamaa wa mke. Ndugu wa mume wanalalamika na kuwa fedha na rasilimali zao, zinateketezwa kwa mke na jamaa zake, umeme bure!, mishahara bure, na bado wanapewa mgao wa asilimia 4.5 ya fedha zote za misaada!. Jamaa za mke wanalalamika kuwa dada yao amenyimwa uhuru wa kupokea vijizawadi kutoka nje, amenyimwa uhuru wa kuzurura atakavyo, na uhuru wa kujichanyanya na watu atakavyo!.

Maadam wanandoa wenyewe, wanapatana na wanaelewana, then hizi kelele za ndugu na jamaa ni kelele tuu za mlango.

Japo ndoa ilifungwa kwa ghilba na ulangai, maadamu mke kajituliza tuli ndani ya ndoa, then inahesabika ameridhia!.

Pasco
 
Nilitaka kukukosoa kidogo kuhusu hiyo dhana yako ya Muungano wenu na kuinasibisha na Ndoa.

Kumbuka kuwa zilizoungana hapo ni Nchi mbili huru kwa maana Serikali Mbili zilizokuwa zinaongoza nchi hizo mbili huru. Na ukipata Maana ya Serikali utakuja kuona kuwa Serikali ni Watu. Bila watu hakuna Sirikali.

Ndoa ni muungano wa watu wawili tu wa jinsia tofauti. Sasa unaponasibisha na Muungano sawa na Nddoa je nani mke na nani mme na umetumia vigezo gani kujua kuwa huyu ni mume na huyu mke.

Muungano wenu kama mvungano ni muungano uliounganisha nchi mbili huru tena pasu kwa pasu. Kila mtu ana haki ya kufaidi na kuumia pasu kwa pasu bila mmoja kumbeba au kumlalia mwenzake kama ilivyo sasa.

Dhana muhimu katika muungano ni KUHISHIMIANA NA SIO KUVUMILIANA KATIKA MAMBO SAHIHI NA WALA SIO MAMBO MAZURI.

Paskali

Mkuu Barubaru, kuna kitu kimenikumbusha uzi huu, kumbe last post yako sikujibu!, hivyo tunapoelekea maadhimisho ya Mapinduzi ya Zanzibar, kama hayatafutwa na Mshirika wa Mtumbua majipu, ili kufanania na huku!, na kama sherehe za Muungano hazitafutwa, sio vibaya tukitafakari kidogo!.

Kwanza nakubaliana na wewe muungano wetu haukupaswa kunasibishwa na dhana ya ndoa, kwasababu ulipaswa kuwa ni muungano wa nchi mbili sawa zenye majukumu sawa!. Ndoa za wenzetu wa ulaya, mke na mume wana haki sawa!, hakuna anayelipa posa ya hata tano!, wala hazina mahari. Lakini ndoa za Kiafrika kuna anayeposa, ni pesa, analipa posa!, kisha analipia mahari ndipo anapewa mke!. Hivyo mke ni mali ya mume.

Ndani ya ndoa hizi, kuna different roles and responsibilities tofauti za wana ndoa hawa!, mmoja ni mtafutaji, mhangaikaji na mchumaji, mwingine ni mpokeaji, mtumiaji na mdakaji tuu kama golikipa !. Ni jukumu la mume kumvisha, kumlisha, kumtunza na kumgharimia mkewe!, wakati jukumu la mke ni kupika, kulea watoto, kutunza nyumba na kumhudumia mumewe huduma za kwenye ndoa hiyo, kula bure, kulala bure na kuvishwa na kupewa matunzo ni haki yake kwa huduma anazotoa kwenye ndoa hiyo!.

Tukija kwenye muungano wetu, zile hati za muungano zilitamka bayana, tungekuwa na mfuko wa muungano ambapo kila nchi ingechangia sawa gharama za kuuendesha huu muungano!, amini usiamini anayelipia gharama zote za uendeshaji huu muungano ni mshirika mmoja tuu!, hali hii inaondoa ule usawa uliotakiwa kwenye muungano wetu, kumfanya mshirika mmoja kuwa ndiye mtafutaji na mwingine golikipa na hapa ndipo dhana ya ndoa inapoibukia!.

Mzigo wote wa kuzibeba gharama zote kaachiwa mshirika mmoja tuu, tena kama hiyo haitoshi, bado tunapaswa kumega asilimia 4.5 % ya misaada yote kutoka Tanzania inayopokea na kuwajibika kuimegea Zanzibar!, licha ya yote haya, bado umeme bure!, michango yote ya taasisi za kimataifa, tunalipa sisi!, ndani ya set up hii Zanzibar inakuwa kama mke!, kazi yake ni kupokea tuu, na Bara ndie mume!, kinacholeta manung'uniko upande mmoja ni kuwa kwenye ndoa halisi ni kweli mke anatunzwa na kuhudumiwa, ila na yeye huyu mke, anahudumu kwenye zile huduma za ndoa!, lakini kwenye ndoa hii ya kimuungano wetu huyu mke wetu tunayemghaimikia, ana hudumu nini in return?!.

Paskali
 
Pale kwenye picha ya kuchanganya udongo kuashiria muungano, baba wa taifa alishika udongo peke yake. Mkono mmoja alishika udongo wa Zanzibar na mkono mwingine akashika wa Tanganyika halafu akauchanganya. (Picha inaonyesha). Karume amesimama pembeni anatabasam tu. Kwanini wa zanzibar hakuumwaga yeye pale ulipokuwa unachanganyiwa? (Ni observation tu!)
 
Wanabodi,

Kufuatia chokochoko ya kuuchokoa Muungano ilioanzishwa na kikundi cha Uamsho huko Zanzibar, zimeanza kutolewa hoja mbalimbali ikiwemo Watanzania tupewe fursa kuujadili Muungano na ikibidi ipigwe kura ya maoni kuwauliza Watanzania na Wanzanzibari kama wanautaka muungano, jee wanataka muungano wa aina gani, na endapo hawautaki, process ya kuuvunja rasmi aianze.

Wako wengi wanaupenda muungano na wangependa uendelee ila uboreshwe!. Pia wako wanao ona sasa imetosha na muungano uvunjwe!.

Maudhui ya mada hii ni kuwaeleza wanabodi, jambo muhimu liitwalo "kuridhia" ambapo serikali zote zilipaswa kuuriidhia huo muungano kwa utaratibu unaoitwa "RATIFICATION" ambapo ni serikali ya Tanganyika pekee ndio iliyofanya process rasmi ya "ratification", Zanzibar, haikufanya process bali ilitamka tuu kwa maneno ya mdomo bila tamko lolote rasmi la maandishi, na badala yake, hati ya ratification ya Zanzibar, iliwasilishwa kwenye bunge la Tanganyika na dunia kutangaziwa muungano uliridhiwa pande zote!.

Kwa vile Zanzibar, haikuuridhia rasmi Muungano, kama ni kweli hizi chokochoko za Uamsho ni uthibitisho kuwa sasa Zanzibar inataka kujitoa katika muungano wetu huu adhimu, kisheria, mlango uko wazi, yaani wide open for Zanzibar to just walk out, with no regret and no strings attached kwa sababu hawakuuridhia ule mkataba wa muungano in then first place!, hivyo mkataba huo hauko binding kwao!.

Mada yangu hii inakuwa na sehemu zifuatazo.

1. Kuridhia ni Nini (Ratification).
2. Rafication Hufanyikaje.
3. Mikataba ya Kimaifa ni nini? na Jee Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar ni Mkataba wa Kimataifa?.
4. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
5. Process ya Ratification kwa Upande wa Tanganyika.Process ya Ratification kwa Upande wa Zanzibar.
6. Hadaa ya Ratification ya Zanzibar, ilipangwa na nani na kwa nini?.
7. Kukosekana kwa ratification upande wa Zanzibar kunamaanisha nini.
8. Pamoja na kutokuwepo ratification, Jee Muungano ni halali?
9. A Way Forward 1:Tudumishe Muungano?, Muungano wa Aina Gani?.
10. A Way Forward 2:Tuuvunje Muungano?. What are the Consequences?.

1. Kuridhia ni Nini (Ratification).
Kuridhia, au ratification, ni process inayofanywa kwa nchi husika kuridhia mikataba ya kimaifa ili kuipa uhalali wa kisheria kutumika katika nchi husika. Mfano mzuri ni mkataba wa Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar, Tanganyika ni nchi, na Zanzibar ni nchi, hivyo ule mkataba wa muungano ni mkataba wa kimataifa.

Jee kila mkataba wa kimataifa ni lazima uridhiwe?. Jibu ni hapana, sio kila mkataba wa kimataifa ni lazima uridhiwe, ili mkataba wa kimataifa uridhiwe lazima mkutaba husika uwe na kipengele kinacholazimisha mkataba huo kuridhiwa. Tukirudi kwenye mfano wetu wa mkataba wa muungano, kipengele cha VIII cha Articles of Union, kinalazimisha process ya ratification lazima ifanyike ili kuuhalalisha mkataba ule.

(viii) These Articles shall be subject to the enactment of laws by the Parliament of Tanganyika and by the Revolutionary Council of the Peoples' Republic of Zanzibar in conjunction with the Cabinet of Ministers thereof, ratifying the same and providing for the Government of the united Republic and of Zanzibar in accordance therewith.

Nyerere na Karume wangeweza kuamua wakishasaini makubali yale iishie hapo, ingekuwa hivyo hivyo hitaji la kuridhia lisingekuwepo!.

2. Rafication Hufanyikaje?.
Kwa vile mikataba yote ya kimataifa ni lazima iwe ni ya maandishi, vivyo hivyo, ratifikation lazima ifanyike kwa maandishi na sio kwa kauli.

Kwa bunge letu, masharti ya kuridhia hufanywa kwa mujibu wa kifungu cha 63(3)(e) cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kinachotamka kuwa, Bunge litajadili na kuridhia Mikataba yote inayohusu Jamhuri ya Muungano na ambayo kwa masharti yake inahitaji kuridhiwa na kwa mujibu wa Kanuni za Bunge, Kanuni ya 114(11) ya 2007.
1. Waziri husika huwasilisha mezani kwa spika mkataba husika
2. Spika ataipa kamati husika kupata maoni yake
3. Kambi ya upinzani itapewa fursa ya kuandaa maoni yake.
4. Mkataba huo utatangazwa rasmi kwenye order paper ya siku ya kuwasilishwa
5. Waziri atawasilisha, kisha maoni ya kamati, maoni ya kambi ya upinzani na majadiliano.
6. Bunge litakaa kama kamati kupitia kifungu kwa kifungu
7. Bunge litarudi kama bunge na kuridhia mkataba husika
8. Mkataba huo unakuwa sehemu ya sheria za nchi,
9. Unasainiwa na rais na kutangazwa katika gazeti za serikali GN.
10.Ndio unakuwa umeridhiwa, yaani ratified!.

3. Mikataba ya Kimaifa ni nini? na Jee Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar ni Mkataba wa Kimataifa?.
Mkataba wa Kimataifa, ni mkataba kati nchi moja na nchi nyingine, au mikataba yote ya jumuiza za kimataifa ambayo nchi ama hutakiwa kuridhia, au kulazimishwa kuiheshimu hata kama haikuridhia. Mikataba hii au itifaki mbalimbali (protocals), hupaswa kuridhiwa kabla haijawa sheria kwa nchi husika.

Mfano Tanzania iliridhia mkataba wa mahakama ya kimataifa ya Biashara, ICC. Dowans iliposhinda ile kesi, imepaswa kuisajili hukumu hiyo kwenye mahakama zetu (ratification), ili hukumu hiyo igeuke sheria zetu, (domestic law) na kutekelezwa. Watu humu walipiga sana kelele, nilipouangalia mkataba ule humu jf, nikawaambia wana jf wenzangu, hatuna pa kutokea, tozo ile italipwa tuu mara baada ya tozo hiyo kusajiliwa, kinachoendelea sasa ni delaying tactics ambayo nayo tutailipia dearly!.

Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar, ni mkataba halali wa kimataifa wenye sifa muhimu za mkataba, japo una mapungufu mengi kubwa likiwa ni kitu kinachoitwa "Privity of Contrac" ambapo mkataba ulikuwa kwa lugha ya Kiingereza na signatory mmoja alikuwa msomi anaejua kusoma na kuandika kiingereza, wakati signatory wa pili hakujua kusoma, kuandika wala kiingereza, hivyo alisaini kwa dole gumba!.

Ufafanuzi zaidi kuhusu Muungano kuwa ni mkataba wa kimataifa, unapatikana pia katika ukurasa wa kwanza wa andiko la
Prof. Shivji kwenye kitabu cha "The Legal Foundation of the Union in Tanzania and Zanzibar Constitution, DUP, 1990.

Kwa faida ya wasoma kimombo, tembelea
THE UNION BETWEEN TANGANYIKA AND ZANZIBAR

4. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Kila mtu anaelewa Mkataba wa Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar, ulitiwa saini na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Abeid Amani Karume, Aprili 22, 1964, Mjini Zanzibar Hapa nitawapa tuu ilivyokuwa kabla na kilichofuata.
Baada ya Mapinduzi ya Zanzibar, na Nyerere kumsaidia Karume kumshughulikia Johh Okello, Karume alikuwa bado ana wasiwasi wa kudumu kwake kama Mwenyekiti wa BLM, kwa kuzingatia Karume hakushiriki mapinduzi yale, Kiongozi wa mapinduzi alikuwa ni John Okello, Karume alikimbilia bara kujificha! (Japo ilikuja kutangazwa ati alikuwa akiwapeleka wanae Amani na Ali waliokuwa wakisoma kwao Karume (Malawi). Okelo ndie alikuwa Mwenyekiti wa BLM na alimuita Karume kuwa mtangazaji kufuatio kuwa na Kiswahili safi. Karume akamzunguka Okello na kwa kusaidiwa na Nyerere, Okello alishughulikiwa na Karume kuitwaa nafasi ya Mwenyekiti wa BLM!.Kwa vile Karume hakushiriki actively kwenye mapinduzi halisi, alikuwa na wasiwasi wakati wote kuwa wale makamanda wangemrudi!, thanks kwa ulinzi wa askari 300 wa Nyerere, vinginevyo hata hiyo 1971, asingefika!.

Mwezi Machi, 1964, Nyerere alizungumza na Karume kuhusu Muungano, Karume alikubali hapo hapo na kutaka Press Conference iitishwe siku hiyo hoyo watangaze kuwa wameshaungana na kuwa nchi moja, Nyerere Rais, Karume Makamo. Mwalimu alimgomea Karume na kumwambia afanye siri ili taratibu zifuatwe.

Mwanzoni mwa Aprili, Mwalimu alimuita AG waTanganyika, Rowland Brown na kumwambia aandae mkataba wa muungano na uwe siri. Kule Zanzibar, Karume akampa likizo AG wa Zanzibar, Wolfgang Dourado ili isitie kauzibe. Akatafutwa Mwanasheria wa Uganda, Daniel Wadada Nabudere (kakaye mwandishi mashuhuri, David Wadada Nabudere) kutoa ushauri kwa Karume kuhusu muungano.

Tarehe, 22 April, 1964 Nyerere aliyeandamana na Rashidi Kawawa, Oscar Kambona na Job Lusinde walitua ghafla Zanzibar na kwenda moja kwa moja Ikulu ya Zanzibar, wakiwa na hati za muungano na Karume alitakiwa azisaini. Wakati wa utiaji saini huo, ulishuhudiwa pia na Abdallah Kassim Hanga, Abdul-Aziz Ali Twala na Salim Rashidi.

Karume alitaka kumtumia mwanasheria huyo wa Uganda kusaini kwa niaba ya mwanasheria mkuu wa Zanzibar, ila Nabudere akakataa na kusisitiza lazima zisainiwe na Mwanasheria wa Zanzibar!. Ndipo Rowland Brown akatinga na Solicitor General wa Tanganyika, PRN Fifoot aliyesimama nafasi ya Dourado!. Hati za muungano zikasainiwa!. Baada ya hapo Nyerere na ujumbe wake wakawaa pipa lao na kurejea Dar!.

Mkumbuke mpaka Karume anasaini, hajaliambia chochote BLM, siku hiyo jioni Aboud Jumbe aliyekuwa Pemba, ndipo akaelezwa na Karume kilichotokea asubuhi, akashangaa sana!. Jambo kubwa kama hilo limefanyika vipi, BLM, hawajui kitu!.

Ni baada ya kusainiwa, Bunge la Tanganyika likatunga sheria ya Muungano, ili kuuthibitisha hati zile, 'ratification', na BLM nalo lilipaswa kukaa na kuridhia hati zile!.

Muungano Ulithibitishwa rasmi na Bunge la Tanganyika kwa kutungiwa sheria na na ikatolewa uthibitisho mwingine uliosainiwa na Fifffoot kuonyesha kuwa BLM liliketi na kuridhia, lakini kiukweli BLM halikukaa, kujadili, wala kupitisha chochote kule Zanzibar!. Kila kitu kilifanywa bara!.

Aprili 27, 1964 Nyerere na Karume, walitinga katika ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Dalaam kubadilishana hati za Muungano zilizosainiwa na Nyerere na Karume, na documents za ratification na tangu hapo Tanganyika na Zanzibar kuwa dola moja kwa misngi inayotambulika kimataifa. Baada ya kuungana, Mwalimu Nyerere alikuwa rais wa kwanza na Karume alikuwa makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Siku hiyo ya Aprili 27, 1964 ndio siku wajumbe saba wa Baraza la Mapinduzi waliapishwa kuwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Watanganyika na Zanzibar ambao ni Amani Karume, Kassim Abdallah Hanga, Abdulrahman Babu, Hassan Nassor Moyo, Aboud Jumbe, Hasnu Makame na Idris Abdul Wakil. Kati yao, Aboud Jumbe na Hassan Nassor Moyo wangali hai. Baada ya hapo, Bunge la Muungano likakamata madaraka yote!.

5. Process ya Ratification kwa Upande wa Tanganyika.Process ya Ratification kwa Upande wa Zanzibar.
1. Msingi mkuu wa ratification mkataba wa muungano ni kifungu hiki kwenye hati za muungano.
Article VIII of the Articles of Union provides:" These Articles shall be subject to the enactment of laws by the Parliament of Tanganyika and by the Revolutionary Council of the Peoples Republic of Zanzibar in conjunction with the cabinet of ministers thereof, ratifying the same and providing for the Government of United Republic and of Zanzibar in accordance therewith2. Lengo la kifungu hicho, ni kwa vile muungano ni mkataba wa kimataifa, ili mkataba huo upate uhalali wa kisheria katika nchi husika, lazima mkataba huo uridhiwe na nchi husika, hivyo kifungu hicho kilimaanisha bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi, walipaswa waridhie mkataba huo kwa kuutungia sheria mahsusi ili kuuhalalisha kisheria ndani ya nchi zao!.

2. Kuridhia au kutoridhia, hakuondoi uhalali wa mkataba, bali unaondoa uhalali wa kisheria, pale yule ambaye alikosa uhalali wa kisheria pale mwanzo, akiamua hautaki tena ule mkataba, hawajibiki kuuvunja mkataba, but he can just walk away!.

3. Baada tuu ya hati za Muungano kutiwa saini ile Aprill 22 kule Zanzibar, Mwanasheria Mkuu Tanganyika enzi hizo, Rowland Brown aliandaa ratification na kupelekwa kwenye kikao cha bunge la Tanganyika, likapitisha ratification ile asubuhi ya Aprili 26, 1964 kwa kutunga sheria No. 243 ambayo ilitangazwa kwenye gazeti la serikali ya Tanganyika, GN No. hivyo kutimiza matakwa ya kile kifungu namba viii cha mkataba wa muungano.

4. Wakati hayo yakiendelea huku Tanganyika, Zanzibar nao kupitia Mwanasheria Wake Mkuu, Wolfgang Dourado, alipaswa kuandaa hiyo sheria ya ratification kule ikiitwa Decree, ili Baraza la Mapinduzi likae na kuipitisha hivyo kuutambua rasmi muungano kisheria. Hili halikufanyika lkwa sababu Dourado alipewa likizo ya siku 7 akapumzike nje ya nchi!. Aliporudi, seven day leter, akakuta game over!. Akaishia kulalamika kichini chini maana angetoa sauti, sijui kama hata unywele ungepatikana!. Ushahidi ni kauli ya Dourado Mwenyewe "I myself have been the Zanzibar Attorney General and Minster responsible for justice between 1984 and 1989. At that time I managed to peruse all the statute books of Zanzibar from 1964 and 1979 when the Revolutionary Council was acting as a legislative Assembly cum the Cabinet. No ratification law or any law to that effect is there. I was not myopic, but even if I was, the first Attorney General of Zanzibar after the Revolution had also testified the same that no law ratifying the Articles of unionexists on the Statute Books of Zanzibar." Dourado aliyasema hayo katika andiko lake la "The Consolidation of Union" alilowasilisha kwenye semina ya Tanhanyika Law Society, Julai 7, 1983 hapa jijini Dar es Salaam.

5. Mpaka Mungu amemuita Dourado mbele ya haki, msimamo wake ulikuwa "No law ratifying the Articles of the union of 1964 exists on the statute books of Zanzibar., I as a Principal Legal adviser to the Zanzibar government was not consulted ……… Zanzibar therefore did not have legal or constitutional advice from its Principal Legal adviser."

6. Badala yake, Solicitor General wa Tanganyika, PRN Fifoot ndiye alieandaa ratification document ya Zanzíbar ambayo aliisaini yeye na kumpatia Karume ile April, 27, 1964, Karume aiwasilishe kwenye bunge la Tanganyika ile siku Nyerere na Karume walibadilishana hati pale Karimjee. Hati ya aliyoiwasilisha Nyerere was a genuine ratified document iliyokuwa ratified na bunge la Tanganyika!. Hati aliyowasilisha Karume, was a fake one as if ni BLM ndilo nalo limefanya hiyo rafication kama lilivyofanya bunge la Tangayika!, It was just a make belive, kuizuga jumuiya ya kimataifa na hapo ndipo hata hao CIA na iteligensia yao wakaingizwa chaka na kubaki kupiga tarumbeta ya ratification kuwa ilifanyika!.

7. Hata kama Fifoot aliiandaa hiyo ratification ya Zanzibar, kwa nini hakumpa Douradau naibu wake, ili aisaini na kuipitisha kwenye kikao cha BLM ili angalau ionekane ilipitishwa Zanzibar?!.Kwa vile Zanzibar hawakuwa na bunge, Baraza la Mapinduzi ndilo lililokuwa Bunge, Baraza la Mawaziri na Mahakama, kwanini ile ratification iliyoandaliwa bara, isipelekwe tuu na kupigwa rubber stamp kwenye BLM ili kuipa uhalali kuwa ni kweli BLM waliridhia na kuratify?!.

8. Siku ile ya April 27, 1964, wakati Nyerere na Karume walipotinga ndani ya bunge la Tanganyika, kubadilishana hati za muungano zilizo kuwa ratified,Nyerere aliwasilisha hati halali ya muungano ilikuwa ratified kihalali na bunge la Tanganyika na kutangazwa rasmi kwenye gazeti la serikali, GN lakini Karume aliwasilisha ile hati iliyosainiwa na Fifoot alijifanya Dourado na kuziwasilisha hati za muungano kwenye bunge la Tanganyika as if ni kweli BLM lilikaa likajadili na kuridhia hizo hati za muungano, na Karume sio tuu amesaini hizo ratification bila kuzipitishia BLM, bali pia amezitungia Decree na kuitangaza katika GN hiyo hiyo ya Tanganyika japo kwenye GN ya Zanzibar sheria hiyo haipo!.

9. Kisheria, kwenye sheria ya mikataba, place of contact maters much as far as domestic laws are concerned, Ule mkataba wa muungano ni international contract, unaweza kusainiwa popote ndio maana Mwalimu Nyerere na time yake, walifunga safari kwenda Zanzibar. Process ya ratification sio international contact, ni domestic contact kutumia domestic laws (municipal) ambapo ratification hupaswa kufanywa na bunge husika likiwa nchi husika. Bunge la Tanganyika lilitimiza wajibu wake hivyo ratification ya Tanganyika ni legal. Kitendo cha ratification ya Zanzibar kuandaliwa na Fifoot wa Tanganyika na kusainiwa nae, halafu Karume kukabidhiwa sheria hiyo wakati sgeria za Zanzibar kwa wakati huo zilikuwa Decrees na kuiwasilisha bunge la Tanganyika, tangazo la ratification kutolewa kwenye GN ya Tanganyika na sio ya Zanzibar, ni mambo yanaifanya hiyo ratification kuwa voidable na sio void!

10. Hoja ya "privity' to contract na "capacity" to contract pia ipo kwa Karume kama Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, alikuwa na capacity to contact kama Karume kwenye zile articles of union, lakini kwenye Ratification, Karume hakuwa na Capacity ya kusaini sheria ambayo haikutungwa na BLM, na kusainiwa na Fifoot badala ya Dourado, na sheria hiyo kutopitishwa na BLM lakini akaiwasilisha as if imeridhiwa na BLM!, na Fifoot hakuwa na capacity to contract kwa niaba ya Dourado!, tena (ninahisi Fifoot alifanya "misrepresentation kujifanya Dourado ndio maana kuna uwezekano mkubwa, Karume hakupewa tena zile original documents!, alikuja mikono mitupu, na kurudi mikono mitupu ndio kule Zanzibar, hizo documents are no where to be seen!!). Emphasis mine!
11. Hata hivyo, kuna mabishano makubwa kati wanazuoni na wasomi mbalimbali wa sheria kuhusiana na hii issue ya ratification. Mwalimu wangu, Prof. Shivji amesema japo hakuna kumbukumbu zozote kuwa BLM liliridhia, kwa vile BLM limeipitisha sheria ya muungano, huko ndiko kuridhia kwenyewe!, kwa hiyo kwa Shivji, muungano uliridhiwa!.

12. Aliyekuwa kiongozi wa kambi ya upinzani kwenye BLW, Hon. Abubakar Khamis Bakary ambaye ndie aliyetoa posa ya ndoa na CCM kule BLW na kuunda SUK ambapo kama mshenga, amezawadiwa uwaziri wa sheria anapingana na Prof. Shivji kwa kusema kuwa sheria ambayo haikutungwa na BLM wala haikupitishwa na BLM, sio sheria halali kwa Zanzibar!.

13. Pamoja na Kutofautiana na Shivji kuhusu uhalali wa ratification, lakini Mhe. Bakari anakubaliana na Shivji kuwa muungano ni halali, kwa sababu, licha yakutokuwepo official ratification kutoka Zanzíbar, hakuna Wanzanzibari wowote waliochukua hatua zozote za kupinga au kulalamika, hivyo hiyo ni dalili kuwa Wanzanzibari wameukubali muungano impliedily not expressly!.

14. Mwanasheria mwingine wa Zanzibar, al maaruf, Ali Salehe, mwandishi na mtangazaji wa BBC, yeye anashikilia, kwa kwa vile muungano haukuridhiwa, lazima uridhiwe ili kuupa nguvu ya kisheria Zanzibar!. Hivyo anasema ratification ifanyike!. Na hapa ndipo na mimi niliposimamia kuwa Wanzanzibari wafanye ratification kama kweli hawautaki tena muungano, BLW likatae ku ratify ili mlango wa kutokea uwe wazi, wide open!.

15. Prof. Haroub Othman ametofautiana na Shivji kwa kusema wajumbe wawili wa BLM, Abrahman Mohamed Babu na Khamis Abudulah Ameir, walimweleza kuwa BLM walijadilili hati za muungano na kuridhia! (bila maandishi wala kumbukumbu?). Prof. Haroub anadai siku anaelezwa hayo walikuwa club ya YASU akiwa anacheza na katoto fulani ambacho kalikuwa bado hata hajabalehe, kakiitwa Ali Juma Shamhuna!.

16. Kufuatia uwepo wa document ya ratification huku bara, na Zanzibar kimataifa ilikufa rasmi siku ile ya April, 26, 1964, hakuna tena anaejali kama hizo ratification documents zili fojiwa huku bara, ndio maana hata tume ya Nyalali, ilizihalalisha na kimataifa everthing is ok na humo humo ndimo hao majasusi wa Marekani, walikolalia na wote wanaoamini muungano uliridhiwa, japo ni kweli kwa bara muungano uliridhiwa kwa kauli na matendo, kwa Zanzibar, uliridhiwa kwa kauli bila matendo!, na sasa tunasikia kauli za kupinga na matendo ya akufukuzaye!.

17. Kiukweli Karume aliliendesha BLM kibabe sana, yeye kama Rais, Jaji Mkuu na Spika, wale wote waliopingana naye, hakuna ajuaye kilichowakuta ili walishughulikiwa kimya kimya na hata miili yao haikubahatika kuonekena (inasemekana walining'inizwa jiwe shingoni na kutoswa baharini!. Kina Babu kuona hivyo, wakajitimkia zao kabla ya kuwakuta, hayajawakuta. Uvumilivu ulipowashinda waliobaki, nao wakamshughulikia Karume!. (Naamini inteligensia ya Mwalimu alishauona mwelekeo wa Karume kwenye majaaliwa ya muungano, hivyo nae akaacha ya kumkuta yamkute, muungano udumu!.

18. Baada ya Karume, Aboud Jumbe akaukwaa urais. Dourado akamjulisha Jumbe kuhusu kukosekana kwan proper ratification na iliyopelekwa UN is fake!, wakaandaa document kuujulisha ulimwengu kuhusu hilo!. Seif Sharif akamtonya Nyerere, Jumbe akashughulikiwa ipaswavyo, huku Dourado akaozea jela!. Tukatangaziwa "kuchafuka kwa hali ya hewa Zanzibar" bila kuelezwa kisa ni absence ya proper ratification!.

19. Wanzanzibar ni watu wazito sana kujifunza, licha ya kujua kilichomkuta Jumbe kilihusu kuutishia muungano, Dr. Salmini nae akataka kucheza karata yake zile siku zake za mwisho mwisho alinukuliwa akisema, wao wanayatambua yale mambo 11 tuu ndio ya halali, hivyo akajenga hoja kubadili katiba aongeze kipindi cha tatu ili ayashughulikie!. Tiss ilimshughulikia yeye na timu yake yote wakatupwa kando!. Hamshaghai kwa nini Salmin baada ya kustaafu hakuitwa popote kuwa mgeni rasmi kwenye shughuli rasmi?, na yule dada yetu naye akaporwa!.

20.Kupitia hoja hizo na nyingine ambazo sikuzitaja, Mimi Pasco wa JF, kwa Mamlaka niliopewa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Chini ya Kifungu cha "Freedom of Expressions", Sasa Natamka Wazi kuwa Muungano Kati ya Tanganyika na Zanzibar, Haukuwa Ratified Properly in Zanzibar!. Ila pia Nasisitiza, Muungano Huu ni Halali, japo ulikosa uhalali kwa njia ya Expressly in Zanzibar, umepata uhalali huo Impliedly!.

Angalizo.
Unaruhusiwa kucoment chochote wakati mada hii ikiteremka, just coments tuu ila naomba sana, maswali juu ya kuhusu hii mada kabla sijafika mwisho, maana sitakujibu mpaka nimalise, ila nikishamaliza sura zote kumi, nitapokea maswali, maoni au mapendekezo. Endepo uliuliza swali kabla sijafika mwisho, na hatimaye ulikuja jibu la swali lako kwenye mada za mbele, sitakujibu upya bali nitakurefer kwenye majibu ya swali lako.

Hii mada siyo accademic paper, naishusha kwa level ya mwananchi wa kawaida wa Tanzania ambaye ni darasa la saba!. Hata hivyo kwa faida ya wasomi ambao wangependa kuzama deep, mwisho, nitawawekea, references za kusoma zaidi.

Natanguliza shukrani.

Pasco.
Nawatakia mapumziko mema ya leo siku ya Muungano.

Pasco
 
PASCO SIJAKUELEWA KABISA ULIPOSEMA KIONGOZI WA MAPINDUZI ALIKUWA OKELLO
NIMELETA MAKALA KUTOKA GAZETI LA RAIA MWEMA
TOLEO 227
LA TAREHE 22 FEBRUARY 2012
MWANDISHI AHMED RAJABU.

YAFUATAYO ni masimulizi mafupi ya kipindi kifupi cha Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari, 1964 yaliyoipindua serikali ya ubia ya chama cha Zanzibar Nationalist (maarufu Hizbu) na kile cha Zanzibar and Pemba Peoples Party (ZPPP). Tunaangazia nini hasa kilitokea usiku wa Jumamosi Januari 11, yaliyojiri siku ya pili yake na mwezi mzima wa Januari, mwaka 1964 .
Tumeyakusanya masimulizi haya baada ya kuzungumza na walioshiriki katika Mapinduzi hayo ambao baadaye walisaidia kudhibiti madaraka na kuunda taasisi zilizoziba pengo la Serikali iliyopinduliwa ya Waziri Mkuu, Muhammed Shamte Hamadi.
Usiku wa manane wa Januari 11, makada wapatao 200 wa Umoja wa Vijana wa Afro-Shirazi (Afro-Shirazi Youth League) walielekea kwenye kambi ya polisi ya Ziwani, nje kidogo ya mji huko Unguja.
Wakiongozwa na Yusuf Himid wapinduzi hao hawakukabiliwa na upinzani walipofika Ziwani ila waliikuta ghala ya silaha iko wazi na wakazinyakua silaha na kukimbia nazo hadi kwenye uwanja ulio nje ya jengo la Raha Leo.
Hapo ndipo palipokuwa makao makuu ya Mapinduzi kwa siku chache na ndipo wapinduzi walikokuwa wakipewa silaha. Studio za redio ya Serikali pia zilikuwa hapo.
Moja ya sababu zilizoyafanya Mapinduzi yafanikiwe haraka ni uamuzi wa viongozi wa Serikali iliyopinduliwa Sheikh Muhammed Shamte na Sheikh Ali Muhsin Barwani — kuwataka wafuasi wao wasitumie nguvu kuyapinga.
Hivyo, mbali na mapigano yaliyozuka saa za asubuhi ya Jumapili Januari 12, mbele ya Steshini ya Polisi Malindi, hapajazuka mapigano Unguja kati ya waliopindua na waliopinduliwa. Pemba nako pia hakukuwa na upinzani ijapokuwa kisiwa hicho kilikuwa ngome ya vyama vya ZNP na ZPPP.
Wengi wa wapiganaji waliokuwa kwenye Stesheni ya Polisi ya Malindi walikuwa wakuu wa polisi Wakiingereza. Wakipigana na makada wa Umma Party ambao ndio pia waliouteka uwanja wa ndege, bandari pamoja na kituo cha mawasiliano ya nje cha Cable Wireless, kilichokuwa kwenye jengo ambalo sasa ni Hoteli ya Serena Mji Mkongwe
Kwa hakika, kinyume cha baadhi ya watu walivyoandika hapakutokea mauaji ya kimbari. Aliyeanzisha uvumi huo alikuwa John Okello aliyeandika kwenye kitabu chake kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar kwamba watu zaidi ya elfu kumi waliuliwa. Okello aliongeza kwamba aliamrishwa na Yesu Kristo kuwakomboa Waafrika wa Zanzibar kutoka kwa wageni
Tutamrejelea Okello na wengine waliokuwa Raha Leo baadaye. Kwanza tukumbushe kwamba mkesha wa Januari 12, mwaka 1964, Zanzibar haikuwa na jeshi.  Kulikuwa polisi waliokuwa wakiongozwa na Waingereza. Wengi wa askari polisi walikuwa raia wa Tanganyika. Serikali iliyopinduliwa ilikataa kuandikiana mkataba wa kijeshi na Uingereza kwa sababu ikihisi mkataba kama huo utaonekana kuwa wa kikoloni.
Hatuwezi kusema ni nani hasa aliyepiga risasi ya mwanzo au ya mwisho katika Mapinduzi. Naitoshe tusemapo kwamba kwa vile hakukuwa na upinzani, Serikali iliyokuwa madarakani iliporomoka kama ‘nyumba ya karata
Tuwarejelee sasa waliokuwa Raha Leo, makao makuu ya Mapinduzi kwa siku chache. Kwanza tumuangalie Okello ambaye sauti yake ndiyo iliyokuwa ikivuma kwenye Redio Zanzibar.
Hatuna uhakika nani alimpeleka Okello Raha Leo. Wengine wanasema ni Yusuf Himidi. Wengine wanasema ni Seif Bakari aliyetoa rai atumiwe kutoa matangazo kwenye redio kwa vile sauti yake ilikuwa na lafudhi ngeni ya kutisha.
Uhakika tulio nao ni kwamba Okello alipotokea Raha Leo na mabastola yake, Aboud Jumbe alishtuka na akauliza: Nani huyu? Katokea wapi?
Kijana huyo aliyekuwa na umri wa miaka 27 hakujulikana kabla ya Mapinduzi. Alikuwa mtu asiyejua kuandika wala kusoma na akili zake zikimtosha mwenyewe. Hakuwa na sifa za uongozi na wala hakushiriki katika vuguvugu lolote la kisiasa.
Akijibandika cheo cha kijeshi cha Field Marshall ni yeye aliyetangaza kwamba serikali ya ZNP/ZPPP imepinduliwa.
Kwa hakika, kazi hiyo ya kutangaza kufanikiwa kwa Mapinduzi kwanza alipewa Ramadhan Haji, mmoja wa wapinduzi. Lakini alikataa. Jina la Okello lisingelisikika lau Ramadhan Haji angekubali kutangaza kwamba Serikali imepinduliwa na  kwamba wapinduzi waliidhibiti nchi.
Waliokuwa wakiongoza mambo Raha Leo tangu Mapinduzi yaanze, hadi Jumatatu Januari 13, walikuwa Aboud Jumbe, mmoja wa viongozi wa chama cha Afro-Shirazi (ASP), Thabit Kombo (Katibu Mkuu wa ASP) na Badawi Qullatein wa Umma Party. Muda wote huo, Sheikh Abeid Amani Karume (kiongozi wa ASP), Abdulrahman Babu (mwenyekiti wa Umma Party) na Abdalla Kassim Hanga (ASP) walikuwa Dar es Salaam.
Mnamo siku hizo hizo liliundwa Baraza la Mapinduzi na Baraza la Mawaziri lililokuwa na mamlaka kamili ya kuiendesha Zanzibar. Mabaraza hayo mawili yalikuwa taasisi kuu za Serikali ya kimapinduzi ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Na sio ile iitwayo ‘Kamati ya Watu Kumi na Nne’ ambayo baadhi ya watu wanasema kuwa ndiyo iliyoandaa Mapinduzi.
Okello akipenda kujigamba kwamba ndiye aliyeyapanga na kuyaongoza Mapinduzi. Alikuwa akitoa matamshi ya kushtusha na ya ajabu-ajabu kwenye Redio Zanzibar. Kwa mfano, siku moja alidai kwamba alipwe mshahara mkubwa zaidi ya aliokuwa akilipwa Rais Karume. Siku nyingine akasema kwamba kasri zote alizokuwa akitumia sultani kupumzikia apewe yeye.
Kuna siku aliyotoa hukumu kwamba mzee mmoja wa zaidi ya miaka 60 afungwe kwa miaka 99. Alisema kama huyo bwana atakufa gerezani basi mwanawe afungwe ili kuendeleza kifungo na mwanawe akifa basi mjukuu wake afungwe mpaka itimie miaka 99.
Nyakati nyingine aliwaonya watu wazitie moto familia zao na wao wenyewe mpaka wafe kabla ya majeshi yangu kuja.’ Alikuwa akitoa vitisho visivyowahi kamwe kusikika Zanzibar.
Kuna siku alitangaza kwamba wakazi wa eneo moja ambako alikuwa apite, wajipange foleni barabarani wakiwa wamevaa chupi tu.
Okello alikuwa ni adha, kitisho, kichekesho na fedheha kwa Zanzibar. Viongozi wapya wa nchi walichoka naye na wakaamua kumchukulia hatua. Salim Rashid, mmoja wa viongozi wa Umma Party aliyekuwa katibu wa Baraza la Mapinduzi anasema kwamba, kwanza alilizungumza suala la Okello na Sheikh Karume. Halafu akalizungumza na Brigadia Yusuf Himid na mwisho yeye, Yusuf Himid na Kanali Ali Mahfoudh wakalitafutia dawa.
Ilisadifu kuwa siku moja Okello alisafiri kwenda Dar es Salaam akifuatana na Jaha Ubwa, aliyekuwa katibu wake. Walipokuwa wanatarajiwa kurudi Zanzibar, Karume, Yusuf Himid, Salim Rashid na Ali Mahfoudh walikwenda uwanja wa ndege kumsubiri.
Siku hiyo anaikumbuka vizuri Luteni Hashil Seif aliyekuwa ofisa wa zamu kwenye kambi ya jeshi huko Migombani karibu na uwanja wa ndege. Alipigiwa simu akitakiwa aende kwa haraka uwanja wa ndege.  Hakuambiwa anaitiwa nini.
Alipofika ndipo alipoambiwa kwamba kuna ndege ya Shirika la Ndege la Afrika ya Mashariki iliyokuwa inakuja kutoka Dar es Salaam ndani yake wakiwemo pia Okello na Jaha Ubwa. Akaelezwa kwamba awaruhusu abiria wote pamoja na Ubwa washuke, lakini amzuie Okello asishuke. Halafu amwambie rubani ampeleke Okello Kenya.
Hashil naye akampigia simu komredi mwenzake Luteni Amour Dugheshina kumwita aende uwanja wa ndege amsaidie. Maluteni wote wawili walikuwa na bunduki za aina ya machine gun
Ndege ilipotua walipanda ndani ya ndege, wakampokonya silaha Okello na  kutekeleza amri waliopewa. Rubani wa ndege alikasirika sana.Uso wake ulighadhibika, utafikiri mnyama aliyekosewa risasi, alieleza Hashil.
Lakini rubani hakuwa na la kufanya ila kuiwasha ndege na kuelekea Kenya.
Huku nyuma Salim Rashid akampigia simu Oginga Odinga, Makamu wa Rais wa Kenya, kumuarifu kwamba wamemfukuza Okello na wanamrejesha Kenya. Alifanya hivyo kwa makosa kwa sababu kutokana na jina lake akifikiri kuwa Okello ni Mjaluo kutoka Kenya.
Kumbe alikuwa mtu wa kabila la  Acholi aliyezaliwa Uganda na alikwenda Unguja kabla ya kuhamia Pemba ambako alikuwa mwashi, mtiaji rangi nyumba na mpasuaji mawe.
Swali la kujiuliza hapa ni; je, iwapo kweli Okello alikuwa ‘kiongozi mpendwa wa Mapinduzi’ ilikuwaje wafuasi wake na wanamapinduzi wenzake wasimtetee alipoadhiriwa uwanja wa ndege na kufukuzwa nchini? Ilikuwaje akafukuzwa kwa urahisi hivyo?
Kuna uzushi mwingi kuhusu kipindi hiki kifupi cha historia ya Zanzibar. Kwa mfano, kuna filamu ya kubuni ya Wataliana inayoonyesha maiti chungu nzima za watu waliopigwa risasi. Filamu hiyo ilikuwa na lengo moja tu; kuonyesha ukatili na unyama wa Waafrika.
Hakuna ithibati  yoyote kwamba watu waliouawa katika siku za mwanzo za Mapinduzi walifika elfu kumi. Ukweli ni kwamba jumla ya watu waliouawa siku hizo haipindukii 200, katika sehemu za mjini hawazidi 25.
Uzushi mwingine ni kwamba walipelekwa Watanganyika, Zanzibar wakiwa na silaha kwenda kupindua. Na si kweli kwamba Mapinduzi yalikuwa na msisitizo wa kikabila. Katika kipindi cha mwanzo cha Mapinduzi msisitizo ulikuwa wa kitabaka. Nyimbo zilizokuwa zikiimbwa kwenye Redio Zanzibar zikiwazungumzia wakwezi na wakulima na wafanyakazi kwa jumla na si makabila.
Mapinduzi ya Zanzibar yalianzisha taasisi mpya za utawala zikiwa pamoja na Baraza la Mapinduzi, Baraza la Mawaziri na ofisi ya Rais. Taasisi hizo zilikuwa zifanye kazi kwa muda wa mwaka mmoja tu kwa vile ilikwishaamuliwa kwamba Januari 1965 pafanywe uchaguzi wa kulichagua Bunge la Katiba, lililokuwa litunge Katiba ya kudumu ya Zanzibar.Baraza la Mapinduzi la Zanzibar pamoja na Serikali mpya zilianza kwa ubia baina ya chama cha ASP na Umma Party. Ingawa wanachama wa ASP ndio waliofanya Mapinduzi waliutambua mchango wa wafuasi wa Umma Party na hasa mchango wa makada wao waliopata mafunzo ya kijeshi nchini Cuba.
Vijana hao wa Umma walizitia wasiwasi serikali za Marekani na Uingereza na kuzifanya ziamini kuwa utawala mpya wa Zanzibar ulikuwa wa kikomunisti Dhana hiyo ndiyo iliyosababisha kuchukuliwa hatua ya kuyachimba na kuyagandamiza Mapinduzi ya Zanzibar yaliyodumu kutoka Januari 12, hadi 26 Aprili, mwaka 1964.
 
Wakati tukijiandaa kusherekea miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, natafuta muda kuendelea na hii mada.

Paskali
 
Leo siku ya Muungano sio vibaya Tukijikumbusha mambo ya Muungano wetu adhimu ambao tutaulinda kwa gharama yoyote.

Nawatakia Muungano mwema.
P.
 
Leo Tarehe 26 April, 2020 ni sikukuu ya Muungano, sikukuu hii ndio sikukuu muhimu kuliko hata uhuru kwasababu hii ni siku JMT ilipozaliwa. Lakini kutokana na janga hili la Corona, siku hii inaadhimishwa kimya kimya.
Naawatakia Muungano mwema huku nikisisitiza
Nautakia huu muungano wetu adhimu udumu milele na hivyo kukitokea yoyote anayetaka kuuchokoa muungano, namshauri chokochoko amchokoe pweza, muungano hutauweza kwasababu tutaulinda kwa gharama yoyote.
Nawatakia muungano mwema.
P
 
Wanabodi,

Kufuatia chokochoko ya kuuchokoa Muungano ilioanzishwa na kikundi cha Uamsho huko Zanzibar, na kuungwa mkono na Wazanzibari wasioutakia mema huu Muungano wetu adhimu, zimeanza kutolewa hoja mbalimbali za kuhatarisha huu Muungano wetu ikiwemo hoja ya Watanzania tupewe fursa kuujadili Muungano na ikibidi ipigwe kura ya maoni kuhusu Muungano kwa kuwauliza Watanzania na Wanzanzibari kama bado wanautaka huu muungano, na kwa watakao sema ndio, waulizwe jee wanataka muungano wa aina gani, (union, unitary, federation, mkataba nk) na endapo hawautaki, process ya kuuvunja rasmi aianze.

Wako wengi wanaupenda muungano na wangependa uendelee ila uboreshwe!. Pia wako wanaoona huu muungano kwao ni kero tuu na hapa tulipofika sasa imetosha na muungano uvunjwe kila mtu na lwake.

Maudhui ya mada hii ni kuwaeleza wanabodi, process muhimu sana katika muungano iitwayo "kuridhia" (ratification) ambapo serikali zote mbili ya Tanganyika na ya Zanzibar zilipaswa kufanya kwa kuuriidhia huu muungano ili kuupa nguvu ya kisheria, uwe legal na binding kwa utaratibu unaoitwa "RATIFICATION" ambapo ni serikali ya Tanganyika pekee ndio iliyofanya process hii rasmi ya "ratification", kwa upande wa Zanzibar, process hii haikufanyika inavyopaswa bali ilitamka tuu kwa maneno ya mdomo na Karume bila tamko lolote rasmi la maandishi, na badala yake, hati ya ratification ya Zanzibar, iliwasilishwa kwenye Bunge la Tanganyika pekee na hazikuwasilishwa kwenye Baraza la Mapinduzi, bali Karume mwenyewe ndie alijigeuza Baraza la Mapinduzi kwa kuridhia kwa kauli tuu, kisha dunia kutangaziwa Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar umeridhiwa na pande zote!.

Kwa vile Zanzibar, haikuuridhia rasmi Muungano, expressly bali imeridhia impliedly hivyo hizi chokochoko za kikundi cha Uamsho ni uthibitisho kuwa sasa kuna baadhi ya Wazanzibar wanataka Zanzibar kujitoa katika huu muungano wetu adhimu ila sio kwa njia halali bali kwa njia haramu. Nashauri hawa watu sio washughulikiwe bila huruma, bali waelekezwe njia halali za kufuata ili Zanzibar ijitoe kwenye huu muungano kihalali.

Hivyo kama ni kweli Wanzanzibari wote katika umoja wao wameuchoka huu Muungano wetu adhimu, kwa kutumia hoja za kisheria, mlango uko wazi kabisa , yaani the exit door is wide open for Zanzibar just to walk out, with no regret and no strings attached kwa sababu hawakuuridhia ule mkataba wa muungano in the first place!, hivyo mkataba huo hauko binding kwao!, ila hili lifanyike, ni kwanza waishinikize SMS kuutisha kura ya maoni kwa upande wao, wakishapata matokeo kuwa Wazanzibari wengi hawautaki muungano, then wamtume rais wao, kumuomba rais wa JMT ai constitute Mahakama ya Katiba, wapeleke matokeo ya kura yao ya maoni na hoja kujitoa, tuachane kwa amani.

Mada yangu hii inakuwa na sehemu zifuatazo.

1. Kuridhia ni Nini (Ratification).
2. Rafication Hufanyikaje.
3. Mikataba ya Kimaifa ni nini? na Jee Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar ni Mkataba wa Kimataifa?.
4. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
5. Process ya Ratification kwa Upande wa Tanganyika.
6.Process ya Ratification kwa Upande wa Zanzibar.
7. Hadaa ya Ratification ya Zanzibar, ilipangwa na nani na kwa nini?.
8. Jee Kukosekana kwa ratification upande wa Zanzibar kunamaanisha nini.
9. Pamoja na kutokuwepo ratification, Jee Muungano ni halali?
10. A Way Forward 1:Tudumishe Muungano?, Muungano wa Aina Gani?.
11. A Way Forward 2:Tuuvunje Muungano?.
Tuuvunjeje?.

12. A Way Forward 3: What are the Consequences za kuvunjika Muungano?. Winners & Looses

1. Kuridhia ni Nini (Ratification).
Kuridhia, au ratification, ni process inayofanywa kwa nchi husika kuridhia mikataba ya kimataifa ili kuipa uhalali wa kisheria kutumika katika nchi husika. Mfano mzuri ni mkataba wa Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar, Tanganyika ni nchi, na Zanzibar ni nchi, hivyo ule mkataba wa muungano ni mkataba wa kimataifa.

Jee kila mkataba wa kimataifa ni lazima uridhiwe?. Jibu ni hapana, sio kila mkataba wa kimataifa ni lazima uridhiwe, ili mkataba wa kimataifa uridhiwe lazima mkataba huo uwe na kipengele kinacholazimisha mkataba huo kuridhiwa. Tukirudi kwenye mfano wetu wa mkataba wa muungano, kipengele cha VIII cha Articles of Union, kinalazimisha process ya ratification lazima ifanyike ili kuuhalalisha mkataba ule.

(viii) These Articles shall be subject to the enactment of laws by the Parliament of Tanganyika and by the Revolutionary Council of the Peoples' Republic of Zanzibar in conjunction with the Cabinet of Ministers thereof, ratifying the same and providing for the Government of the united Republic and of Zanzibar in accordance therewith.

Nyerere na Karume wangeweza kuamua wakishasaini makubali yale iishie hapo, ingekuwa hivyo hivyo hitaji la kuridhia lisingekuwepo!.

2. Rafication Hufanyikaje?.
Kwa vile mikataba yote ya kimataifa ni lazima iwe ni ya maandishi, vivyo hivyo, ratification zote ni lazima zifanyike kwa maandishi na sio kwa kauli.

Kwa Bunge letu, masharti ya kuridhia hufanywa kwa mujibu wa kifungu cha 63(3)(e) cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kinachotamka kuwa, Bunge litajadili na kuridhia Mikataba yote inayohusu Jamhuri ya Muungano na ambayo kwa masharti yake inahitaji kuridhiwa na kwa mujibu wa Kanuni za Bunge, Kanuni ya 114(11) ya 2007.
1. Waziri husika huwasilisha mezani kwa spika mkataba husika
2. Spika ataipa kamati husika kupata maoni yake
3. Kambi ya upinzani itapewa fursa ya kuandaa maoni yake.
4. Mkataba huo utatangazwa rasmi kwenye order paper ya siku ya kuwasilishwa
5. Waziri atawasilisha, kisha maoni ya kamati, maoni ya kambi ya upinzani na majadiliano.
6. Bunge litakaa kama kamati kupitia kifungu kwa kifungu
7. Bunge litarudi kama Bunge na kuridhia mkataba husika
8. Mkataba huo unakuwa sehemu ya sheria za nchi,
9. Unasainiwa na rais na kutangazwa katika gazeti za serikali GN.
10.Ndio unakuwa umeridhiwa, yaani ratified!.

3. Mikataba ya Kimaifa ni nini? na Jee Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar ni Mkataba wa Kimataifa?.
Mkataba wa Kimataifa, ni mkataba kati nchi moja na nchi nyingine, au mikataba yote ya jumuiza za kimataifa ambayo nchi ama hutakiwa kuridhia, au kulazimishwa kuiheshimu hata kama haikuridhia. Mikataba hii au itifaki mbalimbali (protocals), hupaswa kuridhiwa kabla haijawa sheria kwa nchi husika.

Mfano Tanzania iliridhia mkataba wa mahakama ya kimataifa ya Biashara, ICC. Dowans iliposhinda ile kesi, imepaswa kuisajili hukumu hiyo kwenye mahakama zetu (ratification), ili hukumu hiyo igeuke sheria zetu, (domestic law) na kutekelezwa. Watu humu walipiga sana kelele, nilipouangalia mkataba ule humu jf, nikawaambia wana jf wenzangu, hatuna pa kutokea, tozo ile italipwa tuu mara baada ya tozo hiyo kusajiliwa, kinachoendelea sasa ni delaying tactics ambayo nayo tutailipia dearly!.

Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar, ni mkataba halali wa kimataifa wenye sifa muhimu za mkataba, japo una mapungufu mengi kubwa likiwa ni kitu kinachoitwa "Privity to Contract" ambapo mkataba ulikuwa kwa lugha ya Kiingereza na signatory mmoja alikuwa msomi anaejua kusoma na kuandika kiingereza, wakati signatory wa pili hakujua kusoma, kuandika wala kiingereza, hivyo alisaini kwa dole gumba!.

Ufafanuzi zaidi kuhusu Muungano kuwa ni mkataba wa kimataifa, unapatikana pia katika ukurasa wa kwanza wa andiko la
Prof. Shivji kwenye kitabu cha "The Legal Foundation of the Union in Tanzania and Zanzibar Constitution, DUP, 1990.

Kwa faida ya wasoma kimombo, tembelea

4. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Kila mtu anaelewa Mkataba wa Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar, ulitiwa saini na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Abeid Amani Karume, Aprili 22, 1964, Mjini Zanzibar Hapa nitawapa tuu ilivyokuwa kabla na kilichofuata.
Baada ya Mapinduzi ya Zanzibar, na Nyerere kumsaidia Karume kumshughulikia Johh Okello, Karume alikuwa bado ana wasiwasi wa kudumu kwake kama Mwenyekiti wa BLM, kwa kuzingatia Karume hakushiriki mapinduzi yale physically, Kiongozi wa mapinduzi alikuwa ni John Okello, Karume alikimbilia bara kujificha! (Japo ilikuja kutangazwa ati alikuwa akiwapeleka wanae Amani na Ali waliokuwa wakisoma kwao Karume (Malawi).

Okelo ndie alikuwa Mwenyekiti wa BLM na alimuita Karume kuwa mtangazaji kufuatia kuwa na Kiswahili safi. Karume akamzunguka Okello na kwa kusaidiwa na Nyerere, Okello alishughulikiwa ipasavyo na Karume akaitwaa nafasi ya Mwenyekiti wa BLM!.

Kwa vile Karume hakushiriki actively kwenye mapinduzi halisi, alikuwa na wasiwasi wakati wote kuwa wale makamanda wangemrudi!, thanks kwa ulinzi wa askari 300 wa Nyerere, vinginevyo hata hiyo 1971, asingefika!.

Mwezi Machi, 1964, Nyerere alizungumza na Karume kuhusu Muungano, Karume alikubali hapo hapo na kutaka Press Conference iitishwe siku hiyo hiyo watangaze kuwa wameshaungana na kuwa nchi moja, Nyerere Rais, Karume Makamo. Mwalimu alimgomea Karume na kumwambia afanye siri ili taratibu za kisheria zifuatwe.

Mwanzoni mwa Aprili 1964, Mwalimu Nyerere alimuita AG waTanganyika, Rowland Brown na kumwambia aandae mkataba wa muungano na uwe siri. Kule Zanzibar, Karume akampa likizo AG wa Zanzibar, Wolfgang Dourado ili isitie kauzibe. Akatafutwa Mwanasheria wa Uganda, Daniel Wadada Nabudere (kakaye mwandishi mashuhuri, David Wadada Nabudere) kutoa ushauri kwa Karume kuhusu muungano.

Tarehe, 22 April, 1964 Nyerere aliyeandamana na Rashidi Kawawa, Oscar Kambona na Job Lusinde walitua ghafla Zanzibar na kwenda moja kwa moja Ikulu ya Zanzibar, wakiwa na hati za muungano na Karume alitakiwa azisaini. Wakati wa utiaji saini huo, ulishuhudiwa pia na Abdallah Kassim Hanga, Abdul-Aziz Ali Twala na Salim Rashidi.

Karume alitaka kumtumia mwanasheria huyo wa Uganda kusaini kwa niaba ya mwanasheria mkuu wa Zanzibar, ila Nabudere akakataa na kusisitiza lazima zisainiwe na Mwanasheria wa Zanzibar!. Ndipo AG wa Tanganyika Rowland Brown akatinga Zanzibar akiwa ameandamana na Solicitor General wa Tanganyika, PRN Fifoot aliyesimama nafasi ya Dourado!. Hati za muungano zikasainiwa!.

Baada ya hapo Mwalimu Nyerere na ujumbe wake wakakwaa pipa lao na kurejea Dar!.

Mkumbuke mpaka Karume anasaini hati zile za muungano, hajaliambia chochote BLM, siku hiyo jioni Aboud Jumbe aliyekuwa Pemba, ndipo akaelezwa na Karume kilichotokea asubuhi, akashangaa sana!. Jambo kubwa kama hilo limefanyika vipi, huku BLM, hawajui kitu?!.

Ni baada ya kusainiwa, Bunge la Tanganyika likatunga sheria ya Muungano, ili kuuthibitisha zile hati kwa process ya 'ratification', na BLM nalo lilipaswa kukaa na kuthibitisha kwa kuridhia hati zile na kuzitungia sheria.

Muungano ulithibitishwa rasmi na Bunge la Tanganyika kwa kutungiwa sheria na na ikatolewa uthibitisho mwingine uliosainiwa na Fifffoot kuonyesha kuwa BLM liliketi na kuridhia, lakini kiukweli BLM halikukaa, kujadili, kuridhia wala kupitisha chochote kule Zanzibar!. Kila kitu kilifanywa bara!.

Aprili 26 zikafanyika sherehe za muungano kwa kuchanganya udongo.

Aprili 27, 1964 Nyerere na Karume, walitinga katika ukumbi wa Bunge la Tanganyika, Karimjee Hall jijini Dar es Dalaam na kubadilishana hati za Muungano zilizosainiwa na Nyerere na Karume, na documents za ratification na tangu hapo Tanganyika na Zanzibar kuwa dola moja kwa misingi inayotambulika kimataifa. Baada ya kuungana, Mwalimu Nyerere alikuwa rais wa kwanza na Karume alikuwa makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (baadae Tanzania).

Siku hiyo ya Aprili 27, 1964 ndio siku wajumbe saba wa Baraza la Mapinduzi waliapishwa kuwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Watanganyika na Zanzibar ambao ni Amani Karume, Kassim Abdallah Hanga, Abdulrahman Babu, Hassan Nassor Moyo, Aboud Jumbe, Hasnu Makame na Idris Abdul Wakil. Kati yao, Aboud Jumbe na Hassan Nassor Moyo wangali hai. Baada ya hapo, Bunge la Muungano likakamata madaraka yote!.

5. Process ya Ratification kwa Upande wa Tanganyika.Process ya Ratification kwa Upande wa Zanzibar.
1. Msingi mkuu wa ratification mkataba wa muungano ni kifungu hiki kwenye hati za muungano.
Article VIII of the Articles of Union provides:" These Articles shall be subject to the enactment of laws by the Parliament of Tanganyika and by the Revolutionary Council of the Peoples Republic of Zanzibar in conjunction with the cabinet of ministers thereof, ratifying the same and providing for the Government of United Republic and of Zanzibar in accordance therewith
2. Lengo la kifungu hicho, ni kwa vile muungano ni mkataba wa kimataifa, ili mkataba huo upate uhalali wa kisheria katika nchi husika, lazima mkataba huo uridhiwe na nchi husika, hivyo kifungu hicho kilimaanisha Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi, walipaswa waridhie mkataba huo kwa kuutungia sheria mahsusi ili kuuhalalisha kisheria ndani ya nchi zao!.

3. Kuridhia au kutoridhia, hakuondoi uhalali wa mkataba, bali unaondoa uhalali wa kisheria, pale yule ambaye alikosa uhalali wa kisheria, akiamua kuwa hautaki tena ule mkataba, hawajibiki kuuvunja mkataba, but he/she can just give a notification and walk out or walk away!.

4. Baada tuu ya hati za Muungano kutiwa saini ile Aprill 22 kule Zanzibar, Mwanasheria Mkuu Tanganyika enzi hizo, Rowland Brown aliandaa ratification na kupelekwa kwenye kikao cha Bunge la Tanganyika, likapitisha ratification ile asubuhi ya Aprili 26, 1964 kwa kutunga sheria No. 243 ambayo ilitangazwa kwenye gazeti la serikali (GN) ya Tanganyika. hivyo kutimiza matakwa ya kile kifungu namba viii cha mkataba wa muungano.

4. Wakati hayo yakiendelea huku Tanganyika, Zanzibar nao kupitia Mwanasheria Wake Mkuu, Wolfgang Dourado, alipaswa kuandaa hiyo sheria ya ratification kule ikiitwa Decree, ili Baraza la Mapinduzi likae na kuipitisha hivyo kuutambua rasmi muungano kisheria. Hili halikufanyika kwa sababu Dourado alipewa likizo ya siku 7 akapumzike nje ya nchi!. Aliporudi, seven day later, akakuta the game is over!. Muungano umeishafanyika, akaishia kulalamika tuu kichini chini maana enzi hizo angetoa sauti, sijui kama hata unywele wake ungepatikana!. Ushahidi ni kauli ya Dourado Mwenyewe "I myself have been the Zanzibar Attorney General and Minster responsible for justice between 1984 and 1989. At that time I managed to peruse all the statute books of Zanzibar from 1964 and 1979 when the Revolutionary Council was acting as a legislative Assembly cum the Cabinet. No ratification law or any law to that effect is there. I was not myopic, but even if I was, the first Attorney General of Zanzibar after the Revolution had also testified the same that no law ratifying the Articles of unionexists on the Statute Books of Zanzibar." Dourado aliyasema hayo katika andiko lake la "The Consolidation of Union" alilowasilisha kwenye semina ya Tanganyika Law Society, Julai 7, 1983 hapa jijini Dar es Salaam.

5. Mpaka Mungu amemuita Dourado mbele ya haki, msimamo wake ulikuwa "No law ratifying the Articles of the union of 1964 exists on the statute books of Zanzibar., I as a Principal Legal adviser to the Zanzibar government was not consulted &[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG]; Zanzibar therefore did not have legal or constitutional advice from its Principal Legal adviser."

6. Badala yake, Solicitor General wa Tanganyika, PRN Fifoot ndiye alieandaa ratification document ya Zanzíbar ambayo aliisaini yeye na kumpatia Karume ile April, 27, 1964, Karume aiwasilishe kwenye Bunge la Tanganyika as if imetokea BLM ile siku Nyerere na Karume walibadilishana hati pale Karimjee. Hati ya aliyoiwasilisha Nyerere was a genuine one ratified na Bunge la Tanganyika lakini Hati aliyowasilisha Karume, was a fake one as if ni BLM ndilo nalo limefanya hiyo rafication kama lilivyofanya Bunge la Tangayika!, It was just a make belive, kuizuga jumuiya ya kimataifa na hapo ndipo hata hao CIA na iteligensia yao yote walipoingizwa chaka na kubaki kupiga tarumbeta ya kuwa ratification process ilifanyika Zanzibar! .

7. Hata kama Fifoot aliiandaa hiyo ratification ya Zanzibar, kwa nini hakumpa Dourado, ili aisaini na kuipitisha kwenye kikao cha BLM ili angalau ionekane ilipitishwa Zanzibar?!.Kwa vile Zanzibar hawakuwa na bunge, Baraza la Mapinduzi ndilo lililokuwa Bunge, Baraza la Mawaziri na Mahakama, kwanini ile ratification iliyoandaliwa bara, isipelekwe tuu na kupigwa rubber stamp kwenye BLM ili kuipa uhalali kuwa ni kweli BLM kama walivyompelekea Karume hati za Muungano?!.

8. Siku ile ya April 27, 1964, wakati Nyerere na Karume walipotinga ndani ya Bunge la Tanganyika, pale Karimjee Hall, kubadilishana hati za muungano zilizo kuwa ratified, Nyerere aliwasilisha hati halali ya muungano zilizokuwa ratified kweli na kihalali na Bunge la Tanganyika na kutangazwa rasmi kwenye gazeti la serikali, GN lakini Karume aliwasilisha ile hati iliyosainiwa na Fifoot on behalf of Zanzibar AG, Dourado na kuziwasilisha hati za muungano kwenye Bunge la Tanganyika as if ni kweli BLM lilikaa likajadili na kuridhia hizo hati za muungano, na Karume sio tuu amesaini hizo ratification bila kuzipitishia BLM, bali pia amezitungia Decree na kuitangaza katika GN hiyo hiyo ya Tanganyika japo kwenye GN ya Zanzibar sheria hiyo haipo!.

9. Kisheria, kwenye sheria ya mikataba, place of contact maters much as far as domestic laws are concerned, Ule mkataba wa muungano ni international contract, unaweza kusainiwa popote ndio maana Mwalimu Nyerere na time yake, walifunga safari kwenda Zanzibar. Process ya ratification sio international contact, ni domestic contact kutumia domestic laws (municipal) ambapo ratification hupaswa kufanywa na bunge husika likiwa nchi husika. Bunge la Tanganyika lilitimiza wajibu wake hivyo ratification ya Tanganyika ni legal. Kitendo cha ratification ya Zanzibar kuandaliwa na Fifoot wa Tanganyika na kusainiwa nae, halafu Karume kukabidhiwa sheria hiyo wakati sheria za Zanzibar kwa wakati huo zilikuwa Decrees na kuiwasilisha Bunge la Tanganyika, tangazo la ratification kutolewa kwenye GN ya Tanganyika pekee na sio ya Zanzibar, ni mambo yanaifanya hiyo ratification kuwa voidable na sio void!

10. Hoja ya "privity' to contract na "capacity" to contract pia ipo kwa Karume kama Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, alikuwa na capacity to contact kama Karume kwenye zile articles of union, lakini kwenye Ratification process Karume hakuwa na The Capacity ya kusaini sheria ambayo haikutungwa na BLM, na kusainiwa na Fifoot badala ya Dourado, na sheria hiyo kutopitishwa na BLM lakini akaiwasilisha as if imeridhiwa na BLM!, na Fifoot hakuwa na capacity to contract kwa niaba ya Dourado!, tena (ninahisi Fifoot alifanya "misrepresentation kujifanya Dourado ndio maana kuna uwezekano mkubwa, Karume hakupewa tena zile original documents!, alikuja mikono mitupu, na kurudi mikono mitupu ndio kule Zanzibar, hizo documents are no where to be seen!!). Emphasis mine!
11. Hata hivyo, kuna mabishano makubwa kati wanazuoni na wasomi mbalimbali wa sheria kuhusiana na hii issue ya ratification. Mwalimu wangu, Prof. Shivji amesema japo hakuna kumbukumbu zozote kuwa BLM liliridhia, kwa vile BLM limeipitisha sheria ya muungano, huko ndiko kuridhia kwenyewe!, kwa hiyo kwa Shivji, muungano uliridhiwa!.

12. Aliyekuwa kiongozi wa kambi ya upinzani kwenye BLW, Hon. Abubakar Khamis Bakary ambaye ndie aliyetoa posa ya ndoa na CCM kule BLW na kuunda SUK ambapo kama mshenga, amezawadiwa uwaziri wa sheria anapingana na Prof. Shivji kwa kusema kuwa sheria ambayo haikutungwa na BLM wala haikupitishwa na BLM, sio sheria halali kwa Zanzibar!.

13. Pamoja na Kutofautiana na Shivji kuhusu uhalali wa ratification, lakini Mhe. Bakari anakubaliana na Shivji kuwa muungano ni halali, kwa sababu, licha yakutokuwepo official ratification kutoka Zanzíbar, hakuna Wanzanzibari wowote waliochukua hatua zozote za kupinga au kulalamika, hivyo hiyo ni dalili kuwa Wanzanzibari wameukubali muungano impliedily not expressly!.

14. Mwanasheria mwingine wa Zanzibar, al maaruf, Ali Salehe, mwandishi na mtangazaji wa BBC, yeye anashikilia, kwa kwa vile muungano haukuridhiwa, lazima uridhiwe ili kuupa nguvu ya kisheria Zanzibar!. Hivyo anasema ratification ifanyike!. Na hapa ndipo na mimi niliposimamia kuwa Wanzanzibari wafanye ratification kuuhalalisha muungano kwa kupewa haki ya kupiga kura ya maoni kuhusu muungano na kama ni kweli wengi wao hawautaki tena huu muungano, then BLW likatae ku ratify muungano hivyo kuufungua mlango wa muungano na kuuacha wazi kwa kukaa, wide open kwa Zanzibar kuwa free just to walk out any moment!.

15. Prof. Haroub Othman ametofautiana na Shivji kwa kusema wajumbe wawili wa BLM, Abrahman Mohamed Babu na Khamis Abudulah Ameir, walimweleza kuwa BLM walijadilili hati za muungano na kuridhia! (bila maandishi wala kumbukumbu?). Prof. Haroub anadai siku anaelezwa hayo walikuwa club ya YASU akiwa anacheza na katoto fulani ambacho kalikuwa bado hata hajabalehe, kakiitwa Ali Juma Shamhuna!.

16. Kufuatia uwepo wa document ya ratification huku bara, na Zanzibar kimataifa ilikufa rasmi siku ile ya April, 26, 1964, hakuna tena anaejali kama hizo ratification documents zili fojiwa huku bara, ndio maana hata tume ya Nyalali, ilizihalalisha na kimataifa everthing is ok na humo humo ndimo hao majasusi wa Marekani, walikolalia na wote wanaoamini muungano uliridhiwa, japo ni kweli kwa bara muungano uliridhiwa kwa kauli na matendo, kwa Zanzibar, uliridhiwa kwa kauli bila matendo!, na sasa tunasikia kauli za kupinga na matendo ya akufukuzaye!.

17. Kiukweli Karume aliliendesha BLM kibabe sana, yeye kama Rais, Jaji Mkuu na Spika, wale wote waliopingana naye, hakuna ajuaye kilichowakuta ili walishughulikiwa kimya kimya na hata miili yao haikubahatika kuonekena (inasemekana walining'inizwa jiwe shingoni na kutoswa baharini!). Kina Babu kuona hivyo, wakajitimkia zao kabla ya kuwakuta, hayajawakuta. Uvumilivu ulipowashinda waliobaki, nao wakamshughulikia Karume!. (Naamini inteligensia ya Mwalimu alishauona mwelekeo wa Karume kwenye majaaliwa ya muungano), hivyo nae akaacha ya kumkuta yamkute, ili muungano udumu!.

18. Baada ya Karume, Aboud Jumbe akaukwaa urais. Dourado akamjulisha Jumbe kuhusu kukosekana kwa proper ratification process na iliyopelekwa UN is fake!, wakaandaa document kuujulisha ulimwengu kuhusu hilo!. Seif Sharif akamtonya Nyerere, Jumbe akashughulikiwa ipaswavyo, huku Dourado akaozea jela!. Tukatangaziwa "kuchafuka kwa hali ya hewa ya kisiasa Zanzibar" bila kuelezwa kisa ni absence ya proper ratification!.

19. Wanzanzibar ni watu wazito sana kujifunza, licha ya kujua kilichomkuta Jumbe kilihusu kuutishia huu muungano, Dr. Salmini nae akataka kucheza karata yake zile siku zake za mwisho mwisho alinukuliwa akisema, wao wanayatambua yale mambo 11 tuu ndio ya halali, hivyo akajenga hoja kubadili katiba aongeze kipindi cha tatu ili ayashughulikie!. Tiss ilimshughulikia yeye na timu yake yote wakatupwa kando!. Hamshaghai kwa nini Salmin baada ya kustaafu hakuitwa popote kuwa mgeni rasmi kwenye shughuli rasmi?, na yule dada yetu naye akaporwa!.

20.Kupitia hoja hizo na nyingine ambazo sikuzitaja, Mimi Paskali wa JF, kwa Mamlaka niliopewa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Chini ya Kifungu cha "Freedom of Expressions", Sasa Natamka Wazi kuwa Muungano Kati ya Tanganyika na Zanzibar, Haukuwa Ratified Properly in Zanzibar!. Ila pia Nasisitiza, Muungano Huu ni Halali, japo ulikosa uhalali kwa njia ya Expressly in Zanzibar, umepata uhalali huo Impliedly!.

Angalizo.
Unaruhusiwa kucoment chochote wakati mada hii ikiteremka, just coments tuu ila naomba sana, usiniulize swali lolote juu ya kuhusu hii mada kabla sijafika mwisho, maana sitakujibu mpaka nikamilishe, ila nikishamaliza sura zote kumi, nitapokea maswali, maoni au mapendekezo. Endepo uliuliza swali kabla sijafika mwisho, na hatimaye ulikuja jibu la swali lako kwenye mada za mbele, sitakujibu upya bali nitakurefer kwenye majibu ya swali lako.

Hii mada siyo accademic paper, naishusha kwa level ya mwananchi wa kawaida wa Tanzania ambaye ni darasa la saba!. Hata hivyo kwa faida ya wasomi ambao wangependa kuzama deep, mwisho, nitawawekea, references za kusoma zaidi.

Itaendelea

Paskali

Nawatakia maadhimisho mema ya sikukuu ya muungano.
Paskali
 
Wanabodi,

Kufuatia chokochoko ya kuuchokoa Muungano ilioanzishwa na kikundi cha Uamsho huko Zanzibar, na kuungwa mkono na Wazanzibari wasioutakia mema huu Muungano wetu adhimu, zimeanza kutolewa hoja mbalimbali za kuhatarisha huu Muungano wetu ikiwemo hoja ya Watanzania tupewe fursa kuujadili Muungano na ikibidi ipigwe kura ya maoni kuhusu Muungano kwa kuwauliza Watanzania na Wanzanzibari kama bado wanautaka huu muungano, na kwa watakao sema ndio, waulizwe jee wanataka muungano wa aina gani, (union, unitary, federation, mkataba nk) na endapo hawautaki, process ya kuuvunja rasmi aianze.

Wako wengi wanaupenda muungano na wangependa uendelee ila uboreshwe!. Pia wako wanaoona huu muungano kwao ni kero tuu na hapa tulipofika sasa imetosha na muungano uvunjwe kila mtu na lwake.

Paskali
Wanabodi,
Leo sikukuu ya Muungano, nafanya mapitio ya baadhi ya mabandiko ya muungano.

Japo waasisi wa muungano wetu huu adhimu ni Nyerere na Karume, muungano ni kama ndoa, kuna mtu ana proposes, mwingine anakubali, ndoa inafungwa. Kwenye muungano wetu huu adhimu, aliye proposes ni Nyerere, Karume akakubali. Nia ya Nyerere ni kwenda kwenye serikali moja. Wito kwa viongozi wetu, kama nia ya kweli ni kudumisha muungano, twende kwenye serikali moja. Tumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kuyaishi maono yake!. Nawatakia Muungano Mwema.

Leo ni Sikukuu ya Muungano, nachukua fursa hii kuutafakari Muungano wetu adhimu, kupitia hoja mbalimbali za kimuungano.

Nawatakia maadhimisho mema ya muungano na mapumziko mema.
P
 
Leo tunapo adhimisha miaka 60 ya huu muungano wetu adhimu, nafanya tafakuri, niliwahi kuandika nini humu kuhusu muungano wetu.
Nawatakia maadhimisho mema ya miaka 60 ya muungano wetu adhimu.
Ujumbe wangu ni muungano wetu adhimu udumu milele, na sasa ni muda muafaka tuachane na huu muungano wa kimaghumashi, wa union na federation, sasa twende kwenye muungano wa kweli wa union wa nchi moja, serikali moja, na rais mmoja!.
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Tusaidie
P
 
Kwa vile Muungano haukupata ridhaa ya Wananchi ni muda sasa umefika tuuamua kama kweli tunautaka muungano au hatuutaki. Kama tunautaka basi tuamue ni muungano wa aina gani ....!!

Hata huko UK, Wascotland walipozidisha kelele ..... Wananchi wa Scotland walipewa nafasi ya kuaamua kama wanautaka muungano au la ingawa wamekuwa ndani ya muungano kwa zaidi ya miaka 300.
Naunga mkono hoja, kuhusu kuitishwa kwa kura ya maoni, watuwaulizwe, ila sii kweli muungano haukupata ridhaa ya wananchi, Tanganyika tuliridhia, Zanzibar ndio haikuridhia, ila mwanzo ilibiruzwa kisha ikaridhia!.

Muungano ni kama ndoa, Mwanamke kama hakutaki, mwache!. Usimbake!. Muungano wa bila upande mmoja kuridhia ni sawa na ubakaji. Ila aliyebakwa, ameendelea kuishi na mbakaji, akitoa huduma zote, hivyo anahesabika ni kuridhia by performance.

Japo Zanzibar haiku ratified muungano, lakini imetekeleza muungano, hivyo ni imeridhia impliedly. Je, wajua kuwa Zanzibar haikuridhia Muungano? Ina Maana Gani?

Tanzania hatuna sheria ya kura ya maoni, Zanzibar mnayo, pigeni!. Wanzanzibar amueni moja, ama acheni kelele za muungano!, ama pigeni Kura ya Maoni, muamue moja
P.
 
Mwana JF, Paskali, anakutakia wewe na familia yako HERI YA SIKUKUU YA MAPINDUZI MATUKUFU
YA ZANZIBAR!
Paskali
 
Back
Top Bottom