Je, wajua kuwa Zanzibar haikuridhia Muungano? Ina Maana Gani?


Hapa kuna ndoa ya wawili wapendanao, tatizo sio wanandoa bali ndugu wa mume na jamaa wa mke. Ndugu wa mume wanalalamika na kuwa fedha na rasilimali zao, zinateketezwa kwa mke na jamaa zake, umeme bure!, mishahara bure, na bado wanapewa mgao wa asilimia 4.5 ya fedha zote za misaada!. Jamaa za mke wanalalamika kuwa dada yao amenyimwa uhuru wa kupokea vijizawadi kutoka nje, amenyimwa uhuru wa kuzurura atakavyo, na uhuru wa kujichanyanya na watu atakavyo!.

Maadam wanandoa wenyewe, wanapatana na wanaelewana, then hizi kelele za ndugu na jamaa ni kelele tuu za mlango.

Japo ndoa ilifungwa kwa ghilba na ulangai, maadamu mke kajituliza tuli ndani ya ndoa, then inahesabika ameridhia!.

Pasco
 

Pasco,

Nilitaka kukukosoa kidogo kuhusu hiyo dhana yako ya Muungano wenu na kuinasibisha na Ndoa.

Kumbuka kuwa zilizoungana hapo ni Nchi mbili huru kwa maana Serikali Mbili zilizokuwa zinaongoza nchi hizo mbili huru. Na ukipata Maana ya Serikali utakuja kuona kuwa Serikali ni Watu. Bila watu hakuna Sirikali.

Ndoa ni muungano wa watu wawili tu wa jinsia tofauti. Sasa unaponasibisha na Muungano sawa na Nddoa je nani mke na nani mme na umetumia vigezo gani kujua kuwa huyu ni mume na huyu mke.

Muungano wenu kama mvungano ni muungano uliounganisha nchi mbili huru tena pasu kwa pasu. Kila mtu ana haki ya kufaidi na kuumia pasu kwa pasu bila mmoja kumbeba au kumlalia mwenzake kama ilivyo sasa.

Dhana muhimu katika muungano ni KUHISHIMIANA NA SIO KUVUMILIANA KATIKA MAMBO SAHIHI NA WALA SIO MAMBO MAZURI.

 



Mkuu Barubaru, kuna kitu kimenikumbusha uzi huu, kumbe last post yako sikujibu!, hivyo tunapoelekea maadhimisho ya Mapinduzi ya Zanzibar, kama hayatafutwa na Mshirika wa Mtumbua majipu, ili kufanania na huku!, na kama sherehe za Muungano hazitafutwa, sio vibaya tukitafakari kidogo!.

Kwanza nakubaliana na wewe muungano wetu haukupaswa kunasibishwa na dhana ya ndoa, kwasababu ulipaswa kuwa ni muungano wa nchi mbili sawa zenye majukumu sawa!. Ndoa za wenzetu wa ulaya, mke na mume wana haki sawa!, hakuna anayelipa posa ya hata tano!, wala hazina mahari. Lakini ndoa za Kiafrika kuna anayeposa, ni pesa, analipa posa!, kisha analipia mahari ndipo anapewa mke!. Hivyo mke ni mali ya mume.

Ndani ya ndoa hizi, kuna different roles and responsibilities tofauti za wana ndoa hawa!, mmoja ni mtafutaji, mhangaikaji na mchumaji, mwingine ni mpokeaji, mtumiaji na mdakaji tuu kama golikipa !. Ni jukumu la mume kumvisha, kumlisha, kumtunza na kumgharimia mkewe!, wakati jukumu la mke ni kupika, kulea watoto, kutunza nyumba na kumhudumia mumewe huduma za kwenye ndoa hiyo, kula bure, kulala bure na kuvishwa na kupewa matunzo ni haki yake kwa huduma anazotoa kwenye ndoa hiyo!.

Tukija kwenye muungano wetu, zile hati za muungano zilitamka bayana, tungekuwa na mfuko wa muungano ambapo kila nchi ingechangia sawa gharama za kuuendesha huu muungano!, amini usiamini anayelipia gharama zote za uendeshaji huu muungano ni mshirika mmoja tuu!, hali hii inaondoa ule usawa uliotakiwa kwenye muungano wetu, kumfanya mshirika mmoja kuwa ndiye mtafutaji na mwingine golikipa na hapa ndipo dhana ya ndoa inapoibukia!.

Mzigo wote wa kuzibeba gharama zote kaachiwa mshirika mmoja tuu, tena kama hiyo haitoshi, bado tunapaswa kumega asilimia 4.5 % ya misaada yote kutoka Tanzania inayopokea na kuwajibika kuimegea Zanzibar!, licha ya yote haya, bado umeme bure!, michango yote ya taasisi za kimataifa, tunalipa sisi!, ndani ya set up hii Zanzibar inakuwa kama mke!, kazi yake ni kupokea tuu, na Bara ndie mume!, kinacholeta manung'uniko upande mmoja ni kuwa kwenye ndoa halisi ni kweli mke anatunzwa na kuhudumiwa, ila na yeye huyu mke, anahudumu kwenye zile huduma za ndoa!, lakini kwenye ndoa hii ya kimuungano wetu huyu mke wetu tunayemghaimikia, ana hudumu nini in return?!.

Paskali
 
Pale kwenye picha ya kuchanganya udongo kuashiria muungano, baba wa taifa alishika udongo peke yake. Mkono mmoja alishika udongo wa Zanzibar na mkono mwingine akashika wa Tanganyika halafu akauchanganya. (Picha inaonyesha). Karume amesimama pembeni anatabasam tu. Kwanini wa zanzibar hakuumwaga yeye pale ulipokuwa unachanganyiwa? (Ni observation tu!)
 
Nawatakia mapumziko mema ya leo siku ya Muungano.

Pasco
 
PASCO SIJAKUELEWA KABISA ULIPOSEMA KIONGOZI WA MAPINDUZI ALIKUWA OKELLO
NIMELETA MAKALA KUTOKA GAZETI LA RAIA MWEMA
TOLEO 227
LA TAREHE 22 FEBRUARY 2012
MWANDISHI AHMED RAJABU.


YAFUATAYO ni masimulizi mafupi ya kipindi kifupi cha Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari, 1964 yaliyoipindua serikali ya ubia ya chama cha Zanzibar Nationalist (maarufu Hizbu) na kile cha Zanzibar and Pemba Peoples Party (ZPPP). Tunaangazia nini hasa kilitokea usiku wa Jumamosi Januari 11, yaliyojiri siku ya pili yake na mwezi mzima wa Januari, mwaka 1964 .
Tumeyakusanya masimulizi haya baada ya kuzungumza na walioshiriki katika Mapinduzi hayo ambao baadaye walisaidia kudhibiti madaraka na kuunda taasisi zilizoziba pengo la Serikali iliyopinduliwa ya Waziri Mkuu, Muhammed Shamte Hamadi.
Usiku wa manane wa Januari 11, makada wapatao 200 wa Umoja wa Vijana wa Afro-Shirazi (Afro-Shirazi Youth League) walielekea kwenye kambi ya polisi ya Ziwani, nje kidogo ya mji huko Unguja.
Wakiongozwa na Yusuf Himid wapinduzi hao hawakukabiliwa na upinzani walipofika Ziwani ila waliikuta ghala ya silaha iko wazi na wakazinyakua silaha na kukimbia nazo hadi kwenye uwanja ulio nje ya jengo la Raha Leo.
Hapo ndipo palipokuwa makao makuu ya Mapinduzi kwa siku chache na ndipo wapinduzi walikokuwa wakipewa silaha. Studio za redio ya Serikali pia zilikuwa hapo.
Moja ya sababu zilizoyafanya Mapinduzi yafanikiwe haraka ni uamuzi wa viongozi wa Serikali iliyopinduliwa Sheikh Muhammed Shamte na Sheikh Ali Muhsin Barwani — kuwataka wafuasi wao wasitumie nguvu kuyapinga.
Hivyo, mbali na mapigano yaliyozuka saa za asubuhi ya Jumapili Januari 12, mbele ya Steshini ya Polisi Malindi, hapajazuka mapigano Unguja kati ya waliopindua na waliopinduliwa. Pemba nako pia hakukuwa na upinzani ijapokuwa kisiwa hicho kilikuwa ngome ya vyama vya ZNP na ZPPP.
Wengi wa wapiganaji waliokuwa kwenye Stesheni ya Polisi ya Malindi walikuwa wakuu wa polisi Wakiingereza. Wakipigana na makada wa Umma Party ambao ndio pia waliouteka uwanja wa ndege, bandari pamoja na kituo cha mawasiliano ya nje cha Cable Wireless, kilichokuwa kwenye jengo ambalo sasa ni Hoteli ya Serena Mji Mkongwe
Kwa hakika, kinyume cha baadhi ya watu walivyoandika hapakutokea mauaji ya kimbari. Aliyeanzisha uvumi huo alikuwa John Okello aliyeandika kwenye kitabu chake kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar kwamba watu zaidi ya elfu kumi waliuliwa. Okello aliongeza kwamba aliamrishwa na Yesu Kristo kuwakomboa Waafrika wa Zanzibar kutoka kwa wageni
Tutamrejelea Okello na wengine waliokuwa Raha Leo baadaye. Kwanza tukumbushe kwamba mkesha wa Januari 12, mwaka 1964, Zanzibar haikuwa na jeshi.  Kulikuwa polisi waliokuwa wakiongozwa na Waingereza. Wengi wa askari polisi walikuwa raia wa Tanganyika. Serikali iliyopinduliwa ilikataa kuandikiana mkataba wa kijeshi na Uingereza kwa sababu ikihisi mkataba kama huo utaonekana kuwa wa kikoloni.
Hatuwezi kusema ni nani hasa aliyepiga risasi ya mwanzo au ya mwisho katika Mapinduzi. Naitoshe tusemapo kwamba kwa vile hakukuwa na upinzani, Serikali iliyokuwa madarakani iliporomoka kama ‘nyumba ya karata
Tuwarejelee sasa waliokuwa Raha Leo, makao makuu ya Mapinduzi kwa siku chache. Kwanza tumuangalie Okello ambaye sauti yake ndiyo iliyokuwa ikivuma kwenye Redio Zanzibar.
Hatuna uhakika nani alimpeleka Okello Raha Leo. Wengine wanasema ni Yusuf Himidi. Wengine wanasema ni Seif Bakari aliyetoa rai atumiwe kutoa matangazo kwenye redio kwa vile sauti yake ilikuwa na lafudhi ngeni ya kutisha.
Uhakika tulio nao ni kwamba Okello alipotokea Raha Leo na mabastola yake, Aboud Jumbe alishtuka na akauliza: Nani huyu? Katokea wapi?
Kijana huyo aliyekuwa na umri wa miaka 27 hakujulikana kabla ya Mapinduzi. Alikuwa mtu asiyejua kuandika wala kusoma na akili zake zikimtosha mwenyewe. Hakuwa na sifa za uongozi na wala hakushiriki katika vuguvugu lolote la kisiasa.
Akijibandika cheo cha kijeshi cha Field Marshall ni yeye aliyetangaza kwamba serikali ya ZNP/ZPPP imepinduliwa.
Kwa hakika, kazi hiyo ya kutangaza kufanikiwa kwa Mapinduzi kwanza alipewa Ramadhan Haji, mmoja wa wapinduzi. Lakini alikataa. Jina la Okello lisingelisikika lau Ramadhan Haji angekubali kutangaza kwamba Serikali imepinduliwa na  kwamba wapinduzi waliidhibiti nchi.
Waliokuwa wakiongoza mambo Raha Leo tangu Mapinduzi yaanze, hadi Jumatatu Januari 13, walikuwa Aboud Jumbe, mmoja wa viongozi wa chama cha Afro-Shirazi (ASP), Thabit Kombo (Katibu Mkuu wa ASP) na Badawi Qullatein wa Umma Party. Muda wote huo, Sheikh Abeid Amani Karume (kiongozi wa ASP), Abdulrahman Babu (mwenyekiti wa Umma Party) na Abdalla Kassim Hanga (ASP) walikuwa Dar es Salaam.
Mnamo siku hizo hizo liliundwa Baraza la Mapinduzi na Baraza la Mawaziri lililokuwa na mamlaka kamili ya kuiendesha Zanzibar. Mabaraza hayo mawili yalikuwa taasisi kuu za Serikali ya kimapinduzi ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Na sio ile iitwayo ‘Kamati ya Watu Kumi na Nne’ ambayo baadhi ya watu wanasema kuwa ndiyo iliyoandaa Mapinduzi.
Okello akipenda kujigamba kwamba ndiye aliyeyapanga na kuyaongoza Mapinduzi. Alikuwa akitoa matamshi ya kushtusha na ya ajabu-ajabu kwenye Redio Zanzibar. Kwa mfano, siku moja alidai kwamba alipwe mshahara mkubwa zaidi ya aliokuwa akilipwa Rais Karume. Siku nyingine akasema kwamba kasri zote alizokuwa akitumia sultani kupumzikia apewe yeye.
Kuna siku aliyotoa hukumu kwamba mzee mmoja wa zaidi ya miaka 60 afungwe kwa miaka 99. Alisema kama huyo bwana atakufa gerezani basi mwanawe afungwe ili kuendeleza kifungo na mwanawe akifa basi mjukuu wake afungwe mpaka itimie miaka 99.
Nyakati nyingine aliwaonya watu wazitie moto familia zao na wao wenyewe mpaka wafe kabla ya majeshi yangu kuja.’ Alikuwa akitoa vitisho visivyowahi kamwe kusikika Zanzibar.
Kuna siku alitangaza kwamba wakazi wa eneo moja ambako alikuwa apite, wajipange foleni barabarani wakiwa wamevaa chupi tu.
Okello alikuwa ni adha, kitisho, kichekesho na fedheha kwa Zanzibar. Viongozi wapya wa nchi walichoka naye na wakaamua kumchukulia hatua. Salim Rashid, mmoja wa viongozi wa Umma Party aliyekuwa katibu wa Baraza la Mapinduzi anasema kwamba, kwanza alilizungumza suala la Okello na Sheikh Karume. Halafu akalizungumza na Brigadia Yusuf Himid na mwisho yeye, Yusuf Himid na Kanali Ali Mahfoudh wakalitafutia dawa.
Ilisadifu kuwa siku moja Okello alisafiri kwenda Dar es Salaam akifuatana na Jaha Ubwa, aliyekuwa katibu wake. Walipokuwa wanatarajiwa kurudi Zanzibar, Karume, Yusuf Himid, Salim Rashid na Ali Mahfoudh walikwenda uwanja wa ndege kumsubiri.
Siku hiyo anaikumbuka vizuri Luteni Hashil Seif aliyekuwa ofisa wa zamu kwenye kambi ya jeshi huko Migombani karibu na uwanja wa ndege. Alipigiwa simu akitakiwa aende kwa haraka uwanja wa ndege.  Hakuambiwa anaitiwa nini.
Alipofika ndipo alipoambiwa kwamba kuna ndege ya Shirika la Ndege la Afrika ya Mashariki iliyokuwa inakuja kutoka Dar es Salaam ndani yake wakiwemo pia Okello na Jaha Ubwa. Akaelezwa kwamba awaruhusu abiria wote pamoja na Ubwa washuke, lakini amzuie Okello asishuke. Halafu amwambie rubani ampeleke Okello Kenya.
Hashil naye akampigia simu komredi mwenzake Luteni Amour Dugheshina kumwita aende uwanja wa ndege amsaidie. Maluteni wote wawili walikuwa na bunduki za aina ya machine gun
Ndege ilipotua walipanda ndani ya ndege, wakampokonya silaha Okello na  kutekeleza amri waliopewa. Rubani wa ndege alikasirika sana.Uso wake ulighadhibika, utafikiri mnyama aliyekosewa risasi, alieleza Hashil.
Lakini rubani hakuwa na la kufanya ila kuiwasha ndege na kuelekea Kenya.
Huku nyuma Salim Rashid akampigia simu Oginga Odinga, Makamu wa Rais wa Kenya, kumuarifu kwamba wamemfukuza Okello na wanamrejesha Kenya. Alifanya hivyo kwa makosa kwa sababu kutokana na jina lake akifikiri kuwa Okello ni Mjaluo kutoka Kenya.
Kumbe alikuwa mtu wa kabila la  Acholi aliyezaliwa Uganda na alikwenda Unguja kabla ya kuhamia Pemba ambako alikuwa mwashi, mtiaji rangi nyumba na mpasuaji mawe.
Swali la kujiuliza hapa ni; je, iwapo kweli Okello alikuwa ‘kiongozi mpendwa wa Mapinduzi’ ilikuwaje wafuasi wake na wanamapinduzi wenzake wasimtetee alipoadhiriwa uwanja wa ndege na kufukuzwa nchini? Ilikuwaje akafukuzwa kwa urahisi hivyo?
Kuna uzushi mwingi kuhusu kipindi hiki kifupi cha historia ya Zanzibar. Kwa mfano, kuna filamu ya kubuni ya Wataliana inayoonyesha maiti chungu nzima za watu waliopigwa risasi. Filamu hiyo ilikuwa na lengo moja tu; kuonyesha ukatili na unyama wa Waafrika.
Hakuna ithibati  yoyote kwamba watu waliouawa katika siku za mwanzo za Mapinduzi walifika elfu kumi. Ukweli ni kwamba jumla ya watu waliouawa siku hizo haipindukii 200, katika sehemu za mjini hawazidi 25.
Uzushi mwingine ni kwamba walipelekwa Watanganyika, Zanzibar wakiwa na silaha kwenda kupindua. Na si kweli kwamba Mapinduzi yalikuwa na msisitizo wa kikabila. Katika kipindi cha mwanzo cha Mapinduzi msisitizo ulikuwa wa kitabaka. Nyimbo zilizokuwa zikiimbwa kwenye Redio Zanzibar zikiwazungumzia wakwezi na wakulima na wafanyakazi kwa jumla na si makabila.
Mapinduzi ya Zanzibar yalianzisha taasisi mpya za utawala zikiwa pamoja na Baraza la Mapinduzi, Baraza la Mawaziri na ofisi ya Rais. Taasisi hizo zilikuwa zifanye kazi kwa muda wa mwaka mmoja tu kwa vile ilikwishaamuliwa kwamba Januari 1965 pafanywe uchaguzi wa kulichagua Bunge la Katiba, lililokuwa litunge Katiba ya kudumu ya Zanzibar.Baraza la Mapinduzi la Zanzibar pamoja na Serikali mpya zilianza kwa ubia baina ya chama cha ASP na Umma Party. Ingawa wanachama wa ASP ndio waliofanya Mapinduzi waliutambua mchango wa wafuasi wa Umma Party na hasa mchango wa makada wao waliopata mafunzo ya kijeshi nchini Cuba.
Vijana hao wa Umma walizitia wasiwasi serikali za Marekani na Uingereza na kuzifanya ziamini kuwa utawala mpya wa Zanzibar ulikuwa wa kikomunisti Dhana hiyo ndiyo iliyosababisha kuchukuliwa hatua ya kuyachimba na kuyagandamiza Mapinduzi ya Zanzibar yaliyodumu kutoka Januari 12, hadi 26 Aprili, mwaka 1964.
 
Wakati tukijiandaa kusherekea miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, natafuta muda kuendelea na hii mada.

Paskali
 
Leo siku ya Muungano sio vibaya Tukijikumbusha mambo ya Muungano wetu adhimu ambao tutaulinda kwa gharama yoyote.

Nawatakia Muungano mwema.
P.
 
Leo Tarehe 26 April, 2020 ni sikukuu ya Muungano, sikukuu hii ndio sikukuu muhimu kuliko hata uhuru kwasababu hii ni siku JMT ilipozaliwa. Lakini kutokana na janga hili la Corona, siku hii inaadhimishwa kimya kimya.
Naawatakia Muungano mwema huku nikisisitiza
Nautakia huu muungano wetu adhimu udumu milele na hivyo kukitokea yoyote anayetaka kuuchokoa muungano, namshauri chokochoko amchokoe pweza, muungano hutauweza kwasababu tutaulinda kwa gharama yoyote.
Nawatakia muungano mwema.
P
 

Nawatakia maadhimisho mema ya sikukuu ya muungano.
Paskali
 
Wanabodi,
Leo sikukuu ya Muungano, nafanya mapitio ya baadhi ya mabandiko ya muungano.

Japo waasisi wa muungano wetu huu adhimu ni Nyerere na Karume, muungano ni kama ndoa, kuna mtu ana proposes, mwingine anakubali, ndoa inafungwa. Kwenye muungano wetu huu adhimu, aliye proposes ni Nyerere, Karume akakubali. Nia ya Nyerere ni kwenda kwenye serikali moja. Wito kwa viongozi wetu, kama nia ya kweli ni kudumisha muungano, twende kwenye serikali moja. Tumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kuyaishi maono yake!. Nawatakia Muungano Mwema.

Paskali
 
Wanabodi,
Leo sikukuu ya Muungano, nafanya mapitio ya baadhi ya mabandiko ya muungano.

Japo waasisi wa muungano wetu huu adhimu ni Nyerere na Karume, muungano ni kama ndoa, kuna mtu ana proposes, mwingine anakubali, ndoa inafungwa. Kwenye muungano wetu huu adhimu, aliye proposes ni Nyerere, Karume akakubali. Nia ya Nyerere ni kwenda kwenye serikali moja. Wito kwa viongozi wetu, kama nia ya kweli ni kudumisha muungano, twende kwenye serikali moja. Tumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kuyaishi maono yake!. Nawatakia Muungano Mwema.

Paskali
 
Leo ni Sikukuu ya Muungano, nachukua fursa hii kuutafakari Muungano wetu adhimu, kupitia hoja mbalimbali za kimuungano.

Nawatakia maadhimisho mema ya muungano na mapumziko mema.
P
 
Leo tunapo adhimisha miaka 60 ya huu muungano wetu adhimu, nafanya tafakuri, niliwahi kuandika nini humu kuhusu muungano wetu.
Nawatakia maadhimisho mema ya miaka 60 ya muungano wetu adhimu.
Ujumbe wangu ni muungano wetu adhimu udumu milele, na sasa ni muda muafaka tuachane na huu muungano wa kimaghumashi, wa union na federation, sasa twende kwenye muungano wa kweli wa union wa nchi moja, serikali moja, na rais mmoja!.
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Tusaidie
P
 
Naunga mkono hoja, kuhusu kuitishwa kwa kura ya maoni, watuwaulizwe, ila sii kweli muungano haukupata ridhaa ya wananchi, Tanganyika tuliridhia, Zanzibar ndio haikuridhia, ila mwanzo ilibiruzwa kisha ikaridhia!.

Muungano ni kama ndoa, Mwanamke kama hakutaki, mwache!. Usimbake!. Muungano wa bila upande mmoja kuridhia ni sawa na ubakaji. Ila aliyebakwa, ameendelea kuishi na mbakaji, akitoa huduma zote, hivyo anahesabika ni kuridhia by performance.

Japo Zanzibar haiku ratified muungano, lakini imetekeleza muungano, hivyo ni imeridhia impliedly. Je, wajua kuwa Zanzibar haikuridhia Muungano? Ina Maana Gani?

Tanzania hatuna sheria ya kura ya maoni, Zanzibar mnayo, pigeni!. Wanzanzibar amueni moja, ama acheni kelele za muungano!, ama pigeni Kura ya Maoni, muamue moja
P.
 
Mwana JF, Paskali, anakutakia wewe na familia yako HERI YA SIKUKUU YA MAPINDUZI MATUKUFU
YA ZANZIBAR!
Paskali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…