Je, wajua? Kwa mujibu wa Sheria, viraka vya barabarani vinapaswa kuzibwa ndani ya saa 48

Je, wajua? Kwa mujibu wa Sheria, viraka vya barabarani vinapaswa kuzibwa ndani ya saa 48

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Najiuliza kama sheria inasema hivi, inakuwaje viraka vingine huwa vinaachwa kwa muda mrefu mpaka vinageuka kuwa mashimo makubwa yasiyopitika.. Mfano mzuri barabara ya Keko

=============

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, ameitaka Bodi ya mfuko wa Barabara (RfB) kutumia vifungu vya sheria vitakavyowabana watumiaji wa barabara wanaoegesha magari kwenye mabega ya barabara, wanaoiba alama za barabarani pamoja na wanaopitisha mifugo kwenye barabara.

Aidha, amewataka Mameneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) na wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kuhakikisha wanaziba mashimo barabarani ndani ya masaa 48 kama sheria inavyoelekeza ili kupunguza ajali zinazoweza kutokea kutokana na uwepo wa mashimo hayo.

Meneja wa Bodi ya Mfuko wa Barabara Eliud Nyauhenga, pamoja na mambo mengine amemueleza Naibu Waziri huyo kuwa Mfuko unafanya shughuli mbalimbali ikiwemo kukusanya fedha, kugawa fedha kwa Taasisi husika pamoja na kufuatilia matumizi ya fedha hizo.
 
Hili ni tatizo kubwa mno na hata barabara zetu hazina kabisa alama za barabarani, msafiri ukiwa temeke mwisho huwezi kabisa kujua barabara kuu ya kwenda Morogoro utaipata vipi, its crazy
 
Hapo mtaa wa pemba kipande na bonde
Yaani kama mahandaki leo ni zaidi ya mwaka
 
Sasa kama sheria wanazijua mbona hawazibi maandaki maana siyo viraka tena ni maandaki. Hilo ni jukumu lao wenyewe kufanya au raia anaweza kuwashtaki hao wenye kusimamia hizo.

Barabara

Ova
 
Serikali ndio wavunja sheria namba moja kwenye hii nchi
 
Back
Top Bottom