Je Wajua Kwanini Bara zinaitwa Shule lakini Zanzibar zinaitwa Skuli?

Je Wajua Kwanini Bara zinaitwa Shule lakini Zanzibar zinaitwa Skuli?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi
Kuna baadhi ya maneno hiku Bara yanatamkwa vingine na Zanzibar vingine mfano neno Shule kwa huku bara, kwa Zanzibar zinaitwa skuli.

Sikuwahi kujiuliza Kwanini, ila leo ndio nimejua kwanini bara zinaitwa shule lakini Zanzibar zinaitwa Skuli.

Kupitia live Mubashara ya TBC kwenye tamasha la Kizimkazi, uzinduzi wa skuli fulani ya awali hapo Kizimkazi, iliyojengwa na NMB kwa gharama za TZS milioni 800, mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo Rais Samia ndiye ametupiga somo la skuli na shule.

Tanganyika ilitawaliwa na Wajerumani hivyo shule ni neno la Kijerumani wakati Zanzibar imetawaliwa na Waingereza shule kwa kiingereza ni school hivyo wakaita skuli.

Kabla ya leo, jee wangapi mlijua neno shule ni neno la Kijerumani?. Wangapi mlifahamu neno skuli limetokana na school?.

Kiukweli Mama wa Kizimkazi ni mzuri sana kwa lugha ya Kiswahili, kwenye event ya leo, amenifurahisha jinsi alivyomtambulisha mwanae aitwae Dotto Magari aliposema nimemuona na manywele yake mwanangu Dotto Magari "na hapa ipo" pia akamtaja Mwijaku.

Mkurugenzi Mtendaji wa NMB Ruth Zaipuna amesema NMB imetenga asilimia 1 ya faida yake baada ya kodi, kwa ajili ya huduma za jamii (CSR)

Kwa vile faida kubwa ya NMB inatokana na deposits za huku bara, tutafutilia wamejenga shule ngapi za milioni 800 huku bara, isije kuwa ni deflected grand corruption kumhonga mtu kwa kumjengea shule ya nursery yenye AC, kijijini kwa naniliu!. Wenye data NMB wamejenga shule gani huku bara yenye AC?.

Bi Zaipuna pia akatangaza habari njema ya kujenga bonge la shule la bilioni 2.5 Bahi Dodoma. I bet shule hiyo itapewa jina la SSH School.

Kwenye ukuzaji wa Kiswahili, Mama Kizimkazi anastahili maua yake, Usiyoyajua Kuhusu Samia UN: Kumbe alitaka kuhutubia Kiswahili! Baada ya Kiswahili kuwa Lugha ya Afrika, Rais Samia kukipaisha kuwa Lugha ya Dunia

Tumemshauri Katika Kukuza Lugha Yetu Adhimu ya Kiswahili Kimataifa, Mnaonaje Rais Samia, Atumie Kiswahili, Kulihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa?.

Tamasha la Kizimkazi linaendelea Kizimkazi Zanzibar, kijiji alichozaliwa Rais wetu Samia.

Paskali
 
hilo ni raisi bara Wakoloni walikuwa Wajerumani, Zanzibar ni Uingereza hivyo wamechukuwa (zanzibar) kutoka school wakati bara shule ni neno la kijerumani …
 
Back
Top Bottom