Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Hospitali kubwa ya wagonjwa wenye changamoyo ya akili iliyopo mjini Dodoma inaitwa Mirembe. Mkurugenzi wake amesema iliitwa Mirembe kutokana na miongoni mwa wagonjwa wake wa kwanza aliiitwa Mirembe, alienda Dodoma mwaka 1927 akitokea kanda ya ziwa kumfata mganga maarufu wa wakati huo aliyekuwa karibu na hospitali hiyo, na baadae alihamishiwa hospitalini hapo.
Kwasasa 70% ya wagonjwa wa hospitali hiyo wanatokea Dodoma ikiaminika ni kutokana kuwa na ukaribu na hospitali hiyo huku mikoa mingine ikitoa 30% ya wagonjwa.
Kulingana na takwimu za kidunia, katika kila watu 8 basi mmoja anayo changamoto ya akili
Mabadiliko ya jina yanakuja kutokana na fikra iliyojengeka kwenye jamii juu ya jina lililopo sasa japo mkurugenzi amesema ipo changamoto kwenye fikra za ugonjwa wenyewe/ huduma zaidi.
Sababu zinazojitokeza mara kwa mara na kupelekea matatizo ya akili ni majanga ya kimaisha yanayojumuisha kuanguka biashara, kupoteza ajira, madeni, migogoro ya kifamilia na matumizi ya vilevi kupita kiasi (vilevi vinaweza kusababishwa na sababu zilizotanguliwa).
Wagonjwa wanaotokana na sheria(wanaofanya matukio ya kijinai) ni wengi zaidi(mfano mtu alieua na kupata changamoto ya kiakili) kuliko wagonjwa wa kijamii wanaotokea majumbani kwao.
Gharama za matibabu Mirembe zinafata sera ya afya ambapo mpaka 1990 gharama zote zilikuwa ninabebwa na Serikali, mwaka 2001 ilianzishwa bima ya afya na utaratibu wa kuchangia huduma. Hivyo huduma ya akili wagonjwa huchangia lakini kutokana na wao kutoweza kuzalisha kuna nafuu pale ikishindikana waweze kutibiwa bila malipo japo huwa haitokei mara nyingi.
Kwa hisani ya Bonge, PB