Tate Mkuu
JF-Expert Member
- Jan 24, 2019
- 33,092
- 96,127
Hizo sababu zinazosababisha huo ugonjwa ni za kweli kabisa. Ila kuna sababu nyingine zimesahaulika! Imani za kishirikina, na pia matumizi ya madawa ya kulevya. Mfano Bangi, nk.Hospitali kubwa ya wagonjwa wenye changamoyo ya akili iliyopo mjini Dodoma inaitwa Mirembe. Mkurugenzi wake amesema iliitwa Mirembe kutokana na mgonjwa wake wa kwanza aliyeitwa Mirembe, alienda Dodoma mwaka 1927 akitokea kanda ya ziwa kumfata mganga maarufu wa wakati huo aliyekuwa karibu na hospitali hiyo, na baadae alipelekwa hospitalini hapo.
Kwasasa 70% ya wagonjwa wa hospitali hiyo wanatokea Dodoma ikiaminika ni kutokana kuwa na ukaribu na hospitali hiyo huku mikoa mingine ikitoa 30% ya wagonjwa.
Mabadiliko ya jina yanakuja kutokana na fikra iliyojengeka kwenye jina lililopo sasa japo mkurugenzi amesema ipo changamoto kwenye fikra za ugonjwa wenyewe zaidi.
Sababu zinazojitokeza mara kwa mara na kupelekea matatizo ya akili zinajumuisha kuanguka biashara, kupoteza ajira, madeni, migogoro ya kifamilia na matumizi ya vilevi kupita kiasi (vilevi vinaweza kusababishwa na sababu zilizotanguliwa)