ichumu lya
JF-Expert Member
- Aug 11, 2016
- 2,651
- 2,790
Mnamo miaka ya 1988 Mkoa wa Kagera ulikumbwa na janga la UKIMWI, wakati huo hakukua na elimu yoyote juu ya maambukizi na jinsi ya kujikinga, hakukuwa na kindomu hata watu waliotahiliwa walikuwa wachache, matumizi ya vifaa kama sindano, pini na nyembe vilitumika hovyo ungekuta mashuleni pini moja inatumika kutoa funza darasa zima muingiliano wa damu ulikuwa mkubwa.
Walitokea wafanya biashara waliosafiri mipakani kutafuta pesa hasa kwenye magulio makubwa kama Rukunyu na Kikomera, Katerero nk. Huko magulioni yalifanyika mengi ikiwamo ulevi uzinzi na mengine mengi ndio hapo wengi wao walijikuta wakiambukizwa UKIMWI. Watu hao waliporudi makwao walirudi na mali pamoja na UKIMWI nakumbuka miaka hiyo UKIMWI ilijulikana kama JULIANA AU SILIMU kwa Kihaya.
Maambukizi yalifika vijijini nakumbuka vijiji kama Kanyigo, Buyango, Bugandika, Kiziba, Kyamutwara na maeneo mengine nyumba zilifungwa baada ya familia nzima kufariki ukipita kwenye maeneo tajwa utadhani ni makaburini.
Utamaduni wa Kihaya ulichangiaje maambukizi ya UKIMWI?
Ikumbukwe Wahaya wanatamaduni nyingi ikiwamo ya mtu anapofariki wanazika baada ya mazishi wanakaa siku mbili mpaka nne basi ndugu watoto wazazi na jamaa wa karibu hunyolewa nywere miaka hiyo walitumia wembe ungekuta kikundi cha watu 20 wananyolewa na mtu mmoja tena kwa wembe mmoja mpaka ukikatika kibaya zaidi walinyolewa vipara kitendo kilichopelekea damu kuingiliana kutokana na maumbile au na magonjwa ya ngozi unakuta mtu ana vipere kichwani na mwingine na wembe haukuoshwa baada ya Kumaliza mtu mmoja badala yake walipangusa kwenye kitambaa na kuendelea.
Kwa hiyo kwa siku moja watu zaidi ya 20 walijikuta wanambukizwa UKIMWI pasipokujua.
Misiba ilikuwa ni mingi kufika miaka ya 1992 watu wengi walikuwa wameathirika sana na ndipo taadhari ilianza kuchukuliwa.
Tafiti nyinyi sana tena za wasomi wakiwemo kina NSHOMILE Maprofesa na madakitari wote waliangukia pua kwa kutueleza kuwa marehemu wengi waliendekeza ngono zembe bila kufafanua watoto walifanya ngono na kina nani.
Kwa uzembe huu wa Wizara ya afya wahanga wana kila sababu ya kudai fidia na serikali kuwajibika kwa kushindwa kutimiza majukumu yao.
Nina ushahidi na mifano hai jinsi ambavyo Wahaya waliangamia kwa kukosa maarifa.
Ni mambo mengi sana yanyohusu UKIMWI Wahaya na serikali lakini niombee nikamilishe kitabu chenye utafiti wa kina kitakachozua maswali mengi kwa wanazuoni.
======
Upungufu wa Kinga Mwilini (kwa kifupi UKIMWI; kifupisho cha Kiingereza AIDS) ni ugonjwa unaotokana na virusi ambavyo kwa Kiswahili vinaitwa kifupi VVU ("Virusi vya UKIMWI"; kwa Kiingereza: HIV, yaani "Human Immunodeficiency Virus") na vinashambulia mwili kwa kuondoa nguvu zake za kupambana na maradhi.
Ukimwi ni ugonjwa hatari sana katika maisha ya binadamu kwa kuwa husababisha vifo (yaani kupotea kwa uhai wa watu hao). Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, kufikia mwaka 2014 ugonjwa huu umeua watu milioni 39, hasa kati ya wanaoishi barani Afrika upande wa kusini kwa Sahara. Kwa mwaka 2015 pekee wamefariki watu milioni 1.2 na kati yao watoto wengi.
UKIMWI umekuwa na madhara makubwa katika jamii, kama ugonjwa wa mwili na kama chanzo cha ubaguzi. Kuna sintofahamu kuhusu UKIMWI kama vile kwamba eti, unaweza kusambazwa kwa kugusana tu bila ngono.
Ugonjwa huu pia unasababisha madhara ya kiuchumi ambayo ni makubwa, hasa kwa nchi maskini.
UKIMWI hadi hivi sasa haina chanjo wala tiba, lakini tunaweza kuuepuka ugonjwa huu kwa kuachana na ngono ambayo huweza kusababisha ugonjwa huo, pia tunaweza kujikinga nao kwa kuepuka kuchangia vifaa au vitu vyenye ncha kali.
Kimsingi zaidi ni kwamba ugonjwa huo umetokana na kuenezwa hasa na maadili mabovu. Dhidi yake watu wanahitaji kuelewa tangu utotoni na ujanani maana ya jinsia na maisha kwa jumla, kwamba vinadai upendo, nidhamu na uwajibikaji, si kufuata tamaa tofautitofauti daima[1].
Tarehe 1 Desemba kila mwaka ni siku ya UKIMWI duniani.

Sio hiyo tu miaka iyo kulikuwa na funza wengi sana watu wa miaka iyo wengi wao hawana kucha miguuni na wengine miguu iligeukia upande kutokana na vidonda vilivyosababishwa na funza hao anaeleza " tulitumia pini moja darasa zima uku tukisimamiwa na Waalimu kwa viboko mgongoni hatukupewa muda wa kusafisha izo pini matokeo yake tulijikuta tuchangia kusambaza magonjwa Paspokujua".
Kwakweli Serkali hii ilitenga mkoa wa Kagera tangia zamani ndio maana ata waathirika wa vita vya Idd Amini hawakupewa fidia wakati serkali ndio ilimchokoza nakusababisha vita iliyoathiri Mkoa wa Kagera mpaka leo.
Wakati mwingine nikifikiri jinsi serkali hii sikivu inavyotenda kazi kwaubaguzi nabaki namlilia Mungu. Tukiorodhesha majanga ya Kagera na jinsi yilivyoshughlikiwa najua kila mtu atashika mdomo.
NB: HUJUMA HIZI ZINA MWISHO NA MWISHO WA MNAFIKI NI AIBU.