Je, wajua mila na desturi vilivyochangia ongezeko kubwa la UKIMWI Kagera?

Je, wajua mila na desturi vilivyochangia ongezeko kubwa la UKIMWI Kagera?

Anachosema huyo mdau kuhusu kuchangia wembe au kisu kwenye kunyoa au tohara ni kosa lililokuwa linafanyika ktk jamii nyingi hapa Tanzani hadi mwanzoni mwa miaka ya 2000.

Swali ni kwanini huo wembe na visu viuwe zaidi mkoa wa Kagera tu?
Kuna sababu nyingine naomba uendelee na utafiti wako.

Mikoa ya kusini walikuwa wananyoa nywele watoto wakitoka jando/unyago au wakifiwa wananyolewa kama Kagera lakini hakukutokea shida ya UKIMWI kubwa kama Kagera.

Tena kusini kisu au wembe mmoja walikuwa wanatahiria watoto hata 20 huku kifaa kikiwa na damu mbichi, ile kata weka pembeni lete mwingine kata.

Hapa Tanzania kuna jamii zingine walikuwa wana azimana nyembe kunyolea ndevu na kutolea mwiba au pini kutolea mwiba.
Mkuu sitaki ukubaliane na mimi kwa %100 lakini historia iko wazi kwamba maambukizi ya UKIMWI yalitokea ukanda wa DRC yakaja Uganda mpaka Kagera,kwahiyo sitegemei UKIMWI kuruka kutoka uko hadi Mtwara. Swala la wembe,pini na vifaa vingine halina ubishi kumbuka maeneo unayotaja hayakuwa na wajasiriamali wakutoka eneo moja kwenda eneo jingine kama Kagera miaka iyo.

Taadhali haikuchukuliwa mwanzoni Tanzania walifanya mizaha kama Trump alivyokuwa anachukulia Covid19 akidhani yuko salama lakini ona wanavyopukutika kama parachichi.Ata sisi ilikuwa hivyo matokeo yake ata watawala wenyewe walikuja kuonja joto la UKIMWI mpaka leo.

NB:Usipoziba ufa....................



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom